Umoja wa wazalishaji wa sukari Tanzania (TSPA) Wajitetea kuhusu kupanda kwa Sukari. Hawajawahi kuficha Sukari, Si kazi yao kuagiza Sukari nje
Hivi viwanda kiutaratibu kipindi cha low season hupewa vibali na serikali waagize sukari ije nchini kutoka nchi nyingine.

Lakini kwa wakati huo hawakupewa vibali kwa wakati. Bila shaka hili lilisababisha pia upotevu wa sukari sokoni. Ila wao kwa kutumia ukubwa wao, kuna meli ilikuwa inapeleka sukari nchi nyingine, hivyo wakajiongeza ilete hapa nchini wakati wakiendelea kufuatilia vibali.

Sisi kuuza nje sio rahisi, maana nchi jiran kwanza wanasukari bei nafuu.
hivi viwanda vinazalisha hand to mouth au? kwanini wasiweke stock kubwa itakayotumika wakati wa law season? azam waliomba wajengewe bwawa la kinga maji ambalo lingetumika pia kwa umwagiliaji na kunyweshea ngombe za wamasai simba jike akapotezea then leo tunaletewa blah blah za shortage, kimsingi viwanda vizalishe hawana bidhaa traders wa import,
 
Mpaka sasa nimewasikiliza jwa dakika 30, naendelea kuwasikiliza lakini cha kusikifisha wanaongelea siasw na porojo nyingi. Kuwa "watazalisha" sukari ya kutosha kuanziq mwaka huu.

Pambaf kabisa, walikuwa wapi siku zote mpaka Bashe kaja kuwatia vidole vya masikio ndiyo wanasikia kuwa Watanzania wameathiriwa na bei za sukari?

Hawa wazalishaji hawatakiwi kutupigia porojo, wanatakiwa wazalishe sukari ishuke bei.

Ujinga mtupu.
Hujawasikiliza na kwa hiyo hata hujawaelewa kabisa...!!!

Uthibitisho ni hiki ulichokiandika na ni kwa sababu tu, wewe ni mtu mwenye upande tayari ambaye hata kifanyike kitu gani mtu hawezi kubadilisha msimamo wako...

Kwa lugha rahisi ni kuwa, wewe FaizaFoxy si mtu huru kimawazo na kimtazamo
 
sijaelewa, kwenye maelezo yako unaelezea ishue za ujinga, upi? nani unaona ni mjinga mie au nani?

Hata wewe unaweza kuwa miongoni mwao, pengine...

Mwenzio amefafanua hoja zilizotolewa na TSPA kwa kirefu sana...

Hoja ya "ujinga" kwa maelezo ya ndugu Richard inamhusu yeyote ambaye hajawaelewa hawa TSPA. Which means hata wewe unaweza kuwa miongoni mwao..

Personally, nimefuatilia PC ya hawa TSPA mwanzo mwisho. They were very calm and genuine kwa kila hatua ya ufafanuzi wao juu ya sakata la sukari hapa nchi...

Whether we like it or not, Wizara ya Kilimo na Hussein Bashe (waziri wake) hawakui - handle situation ya sugar gap wisely...

Bahati mbaya sana kuwa, Bunge nalo ignorantly likaingizwa mkenge na mawaziri hawa wawili (Mwigulu - Fedha na Bashe - Kilimo) kiasi cha kushindwa kulisimamia jambo kwa ukamilifu wake..
 
Kwanini hizi taarifa hazikutoka mwishoni mwa 2023,
Na bado mtatajana wote wezi nyie
 
Huyu mzee namfahamu sana kama balozi na nguli wa diplomasia.

Ameeleza uzuri mambo mengi ambayo watanzania wengi hawayafahamu.

Ila hii video imechakachuliwa kwenye dakika ya 6 pale anapozungumzia udhibiti wa sukari ulianza rasmi lini.

Hapo Michuzi ameharibu na hii yazidi kunithibitishia mashaka na uadilifu wa hawa watu wa media ya Tanzania.
Inasikitisha sana
 
Angalia video iliyopostiwa utaelewa ninachosema bwashee!
Hapana.
Hizo 'dots' unazoziona wewe hazipo. Jambo hili la sukari halina utata tena juu yake, kwa sababu maelezo ya kujitosheleza kabisa yamekwisha wasilishwa.
Ukitaka 'kuziumba' hizo 'dots' kufurahisha akili zako, hilo ni jambo jingine kabisa ambalo mimi sioni nishiriki vipi kuzijadili hizo 'dots' za kufikirika.
 
Hapana.
Hizo 'dots' unazoziona wewe hazipo. Jambo hili la sukari halina utata tena juu yake, kwa sababu maelezo ya kujitosheleza kabisa yamekwisha wasilishwa.
Ukitaka 'kuziumba' hizo 'dots' kufurahisha akili zako, hilo ni jambo jingine kabisa ambalo mimi sioni nishiriki vipi kuzijadili hizo 'dots' za kufikirika.
Sawa bwashee
 
Ammi Mpungwe
Habari za Mpungwe nilikuwa nazo siku nyingi sana wakati akiwa balozi South...
Nakumbuka vizuri ktk moja ya mageuzi yetu ya kiuchumi moja ya agenda kubwa ya chama CCM ilikuwa kuwatumia South Africa na hiyo SADC kuwa kiungo cha maendeleo ya nchi zetu kwa sababu wao walikuwa mbele na vitu vyote vinavyotakiwa ikiwa ni pamoja na uwezo wa kitechnologia.
Mpango huu ulianza wakati wa Mwinyi kama sikosei awamu yake ya pili na hata Mwalimu, Marehemu Nyerere aliupendekeza badala ya mazungumzo ya karibu na Mandela..
tatizo lilokuja ni kwamba badala ya kutumia SADC na kuunda benki ambayo ingeweza kusimama ktk mikopo ya miradi ya maendeleo na ujenzi wa infrastructure nchini kama walivyofanya wenzetu wa nchi za Asia kutokutegemea zaidi IMF na benki kuu ya Dunia, viongozi wetu walikuwa na agenda zao za binafsi.

Tatizo kama nilivyowahi kusema viongozi wetu ni watawala weusi sawa na wakoloni kimawazo na hutafuta mwanya wa kujitajirisha wao badala ya kufikiria maslahi ya nchi...
Hivyo, Makaburu wa kwanza kuingia nchini walijengwa na Ami Mpungwe ikiwa ni pamoja na kurudi kwa De Beers kule Mwadui. tatizo lililojitokeza ni kwamba hawa wote walikuwa opportunist na kila kampuni iliyoingia nchini walikuja kuchuma kutokana na udhaifu wa mikataba yetu ambayo kama kawaida viongozi wetu walitaka kukatiwa chao.. Mikataba mibovu iliingiwa ktk kipindi kifupi sana na hawa makaburu hadi likazuka sakata la Tanzanite yetu kule Marerani na wanunuzi wakubwa kama Zales kutokana na mbinu ya Wasouth kutaka kuchukua umilikaji wa migodi hiyo..Nadhani mtakumbuka jinsi report ya uuzaji wa Tanzanite ilivyotofautiana na ile report ya taifa ktk mauzo ya Tanzanite toka hapo tukaanza kuona vitu vingine vikiibuka toka NBC,TBL, TANESCO na kadhalika...
Kundi hilo walianza kugeukana yakazuka makundi kufikia wakati wa Mkapa kwa sababu SADC haikujengwa na kuimarishwa badala yake ilibomolewa na viongozi wa nchi zote zilizohusika kwa sababu wote hawa walikuwa na mipango nje ya jumuiya hiyo - Kujitajirisha wakati ndio huu.
Kwa hiyo, kama alivyosema FMES, viongozi wetu wote walikuwa na malengo yao na wakamtumia sana Ami Mpungwe kufunga ma -deal huko South..Ikifika wakati muafaka huyu jamaa anaweza kuwa dhamana kubwa ya serikali kiushahidi dhidi ya Mafisadi kwa wakati huo kabla viongozi wetu hawajajitanua zaidi kufikia nchi za Ulaya, US na Canada..
JF kwa mafaili!
 
Hujawasikiliza na kwa hiyo hata hujawaelewa kabisa...!!!

Uthibitisho ni hiki ulichokiandika na ni kwa sababu tu, wewe ni mtu mwenye upande tayari ambaye hata kifanyike kitu gani mtu hawezi kubadilisha msimamo wako...

Kwa lugha rahisi ni kuwa, wewe FaizaFoxy si mtu huru kimawazo na kimtazamo
Nimewasikiliza mwanzo mwisho, wamepiga porojo na wanataka kujiosha tu.

Wao kama wataalam wa sukari wako wapi mpaka sukari Tanzania inakuwa bei ya juu kuliko nchi zote zinazotuzunguka?

Wameliongelea hilo?
 
Wazungu wanasema waafrica wenyewe ndio wanao ruhusu kuwa exploited.

Huko kwa wazungu mbali hawa wazanzibari tu wanatuita watanwa.

Think
Hilo ni ukweli unaouma.

Tazama mijitu mizima imeitisha mkutano na waandishi wa habari kuja kupinga serikali kufanya njia za haraka kuagiza sukari ili mwananchi asiendelee kuumia.

Nilikuwa namuona Ame ni mtu wa maana sana, sasa nimeelewa kumbe ni mtwana kama watawana wengine.
 
Kwa mtazamo wangu, Bashe ameshinda hii Vita, amefanikisha kumtoa nyoka pangoni. Hii ni hofu ya financial bill, Mimi sijaona hoja yenye mashiko kwao, zaidi ya kujitetea kuwa wao sio maharamia Wala so mapapa. Ila kwangu Bashe amewashika pabaya. Amepiga kwenye mshono. Bashe anatakiwa kuungwa mkono na kupewa nguvu.
Wacha muneno
 
Wazalisha sukari wana mapungufu makubwa, kila mwaka ni Sugar Scarcity, Sugar Deficity, wakati hii ndio secta yao ya biashara.

Walitakiwa wazalishe sukari ya ziada ya kukabiliana na uhaba wa sukari kila unapojitokeza.

Ni kwamba kwa miaka mingi ya uzalishaji sukari, bado wameshindwa kutosheleza mahitaji ya ndani pekee achana na export.

Hapo ndipo muuza vocha anapo take advantage kwa kuwatumia watendaji wa Serikali.

Wazalisha sukari wangefikisha malengo tarajiwa huu mvutano wa kila mwaka usingejitokeza.
 
Wapigaji wameingia kwenye suala la kuagiza sukari kutoka nje.

Hilo bila shaka yoyote litawezesha kuingiza nchini sukari ilokwisha muda wake na isofaa kwa matumizi ya binadamu.

wauza vouchers ni wapigaji.

Wazalishaji wa sukari ni lazima walindwe na serikali wahitaji sana hiyo kinga ili kuwasidia kufanya biashara yao bila shida.

Huwezi kujenga kiwanda kama cha Bagamoyo Sugar ambacho mzee Balhresa kaamua kuwekeza na hapohapo wakandamiza wazalishaji wa ndani.
Shida ni hii bei za sukari ni kubwa mno ukilinganisha na majirani zetu.
Speaker juzi aliwauliza wabunge bei za sukali nchi majirani ni wastani wa sh 2000 kwetu ni sh 4000.licha ya kuwa na viwanda kibao.
Huyu Mzee Balozi tunamheshimu,lakini ummoja wa wazalishaji nchini wametengeneza Cartel ya kutunyonya wananchi.
Pili hawajifunzi wanaendesha uzalishaji kizamani.Wakati wazalishaji Brazil wanazalisha mazao(byproduct) zaidi ya 30 kwenye miwa hiyo hiyo.kwao sukari ni byproduct 1 kati ya byproducts zaidi ya 30,hivyo sukari ina bei ndogo sana sh 600 tu.

Kama hawezi kujitanua jembe la Brazil litapiga hodi kuzalisha sukari na mazao kibao yatokanayo na sukari,itapunguza gharama ya uzalishaji pammoja na kuongeza ajira,na kuna uwezekano wa kutoagiza madawa au spirit,mbolea itokanayo na miwa. Nisikilizie mziku huo wanaogopa hata kivuli cha Brazil.
 
Njia ipi ilitumika kuwapata waagizaji binafsi wa sukari kutoka nje ya nchi?

Kama haikuwepo njia ya kihalali ya kuwaruhusu waagizaji halali, je njia hiyo ilitengenezwa lini?

Kwa mfano, kampuni ya Zenj general merchandise ltd ilipewa kibali kuagiza tani za sukari 6000 April 2024 kwa misingi ipi?
Duuh ni hatar sana.

Watanzania tunakula vitu vingi vya ovyo kama unampa muuza vocha aagize sukari inayoenda kutumia na mamilion ya watu SI ajabu sukar yenyewe ikawa ime expire muda mrefu tu.
 
Maelezo haya yote ni mazuri, lakini cha kujiuliza ni nini kiliwaziba midomo kupelekea hadi akina Mpina kujeruhiwa kwa hila?

Kwanini wasingelitoa ushuhuda wa tamko hili mapema haraka iwezekanavyo ili kuuweka ukweli wa tuhuma hizo potofu mapema?

Tz imegawika kwa kunyamazia maneno haya kwa kushindwa kuyatoa kwa wakati.

Wengi wapo upande wa Waziri kwa namna walivyoaminishwa na maneno yake ya shobo juu ya tuhuma nzito kuhusu wenye viwanda kuweka mazingira ya uhaba.

Ni wachache tu wenye akili kubwa ndiyo wapo na Mpina baada ya kutumia jicho la tatu kuusaka ukweli wa mambo.

Mnakujaje kutoa ushahidi wa mtu aliyetuhumiwa kwa kesi ya mauwaji ya uongo na tayari alikwisha hukumiwa na adhabu ya kunyongwa ilishatekelezwa?
Mm mwenyewe nimejiuliza haya maswali naona kama watu wamezungukana kwenye madili.
 
Back
Top Bottom