Umoja wa wazalishaji wa sukari Tanzania (TSPA) Wajitetea kuhusu kupanda kwa Sukari. Hawajawahi kuficha Sukari, Si kazi yao kuagiza Sukari nje
Wanakuwaga wagumu hao kuelewa somo; kwa ule ushahidi wa Mpina hayuko peke yake nyuma yake kuna kundi.

Kwa kifupi Bashe ongea na ‘bi-tozo’ gurudumu la ufisadi kilimo ampe mtu mwingine akutoe hapo kwa usalama wako. Jamaa wamekuchoka na ujambazi unaofanya huko, uamini subiri.

Report ya CAG kila ikija imeja madudu ya upigaji sehemu zenyewe unakuta Bashe ndio alilazimisha hela zipelekwe huko.
 
Mjinga huyu, dalali anayetumiwa kufanya lobbying serikalini, alianzia Tanzanite. Hii kampuni ya Kilombelo ndio Mkapa aliichukua kwa mgongo wa wananchi.

Hawa wajinga ndio wamemuhonga Mpina na kulipia vyombo vya habari kila kimoja 10,000,000
 
Wanakuwaga wagumu hao kuelewa somo; kwa ule ushahidi wa Mpina hayuko peke yake nyuma yake kuna kundi.

Kwa kifupi Bashe ongea na ‘bi-tozo’ gurudumu la ufisadi kilimo ampe mtu mwingine akutoe hapo kwa usalama wako. Jamaa wamekuchoka na ujambazi unaofanya huko, uamini subiri.

Report ya CAG kila ikija imeja madudu ya upigaji sehemu zenyewe unakuta Bashe ndio alilazimisha hela zipelekwe huko.
Ndugu yangu Balozi Mpungwe kasema ukiona watoto wa Simba wanacheza pekee yao kuwa makini!,

Je unakijua kisa Adolf Mkenda kutolewa kwenye hiyo wizara huku akiitwa NOSENSE . Tafuta hiyo clip na ujiulize kwa nini alitukanwa tusi kubwa hivyo mbele ya wageni IKULU

Nchi hii sasa ni rasm inaongozwa na Magenge ya wahalifu watukutu kwa koti la siasa na Demokrsia.
Kwa hiyo Bashe ni KATAWI tu kwenye hiyo genge la WAHAINI wa nchi hii.
 
Mjinga huyu, dalali anayetumiwa na washenzi kufanya lobbying setikalini, alianzia Tanzanite, jinga kabisa huyu. Hii kampuni ya Kilombelo ndio Mkapa aliichukua kwa mgongo wa wananchi. Shenzi kabisa huyu.

Hawa wajinga ndio wamemuhonga Mpina na kulipia vyombo vya habari kila kimoja 10,000,000
Siku moja uwe na ujasiri wa kutueleza Abdul na genge wanatumia pesa kutoka wapi. Wafadhiri wa Kiarabu?

Wataweza kuwanunua waTanzania wote?
 
Madam ,hivi hili suala la Kampuni za Vocha n Vistationery ' kioewa kibali Cha kuuagiza Sukari wewe uknakizungunziaje,au ni uzushi wa kina Mpina na Lissu'"?
Kama wana fedha na wameweza kuleta tatizo nini?

Hata Azam ana mashamba ya sukari lakini anauza mandazi.

Ni poyoyo tu asiyeelewa kuwa moja ya biashara kubwa ni vocha Tanzania hii.
 
Tano, kasema Sukari bidhaa nyeti hivyo haiwezi kupakiwa tu kwenye meli yoyote iso na sifa ya kubeba chakula.

Na pia kawashauri watu wa media wakasome tena waelewe maana ya neno Cartel maana lina maana yake mtambuka.
Balozi hakunishawishi sana; isingekuwa maelezo ya ziada ya ufafanuzi yaliyo tolewa na huyo mwingine, ningeanza kuwa na mashaka juu ya huu ushirika wa hawa wenye viwanda. Hizi habari za "bidhaa nyeti na upatikanaji wa meli ni hoja hafifu sana..

"Cartel" haina maana ya zaidi ya ushirikiano wa wachache wanaotumia nafasi zao kujinufaisha dhidi ya kulinda maslahi ya watumiaji bidhaa husika.
Hawa watu wa sukari wanaweza sana kujenga 'cartel' kama udhibiti haupo.
 
Balozi hakunishawishi sana; isingekuwa maelezo ya ziada ya ufafanuzi yaliyo tolewa na huyo mwingine, ningeanza kuwa na mashaka juu ya huu ushirika wa hawa wenye viwanda. Hizi habari za "bidhaa nyeti na upatikanaji wa meli ni hoja hafifu sana..

"Cartel" haina maana ya zaidi ya ushirikiano wa wachache wanaotumia nafasi zao kujinufaisha dhidi ya kulinda maslahi ya watumiaji bidhaa husika.
Hawa watu wa sukari wanaweza sana kujenga 'cartel' kama udhibiti haupo.
Huwezi kuelewa kwa sababu unaangalia juu juu tu. Ni lazima uunganishe dots ili uelewe!
 
Ai
Hali ya Bashe sasa itadhidi kuwa mbaya baada ya Kilombero Sugar kutema cheche

View attachment 3031040
Wazalishaji sukari wavunja ukimya, wadai kutotendewa haki sakata la sukari

Aurea Simtowe

Muktasari:

Baada ya kushutumiwa kwa muda mrefu na kutajwa kuwa wao ndiyo chanzo cha kupanda kwa bei ya sukari nchini, umoja wazalishaji wa sukari Tanzania (TSPA) wavunja ukimya.

Dar es Salaam
. Umoja wa Wazalishaji wa sukari nchini (TSPA) umekanusha madai ya kuficha sukari ili kuongeza bei kwa faida yao binafsi.

Wamesema hawana nia ya kuwa waagizaji kwa sababu lengo lao ni kuzalisha zaidi, huku wakilalamika kwamba wametuhumiwa na kuhukumiwa bila kupewa nafasi ya kusikilizwa.

Wamesema wao hawana nia ya kuwa waagizaji wa sukari, kwa sababu lengo la biashara yao ni kuzalisha zaidi.

Akizungumza kwa niaba ya wazalishaji wa sukari leo Jumatatu, Julai 1, 2024, mbele ya vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Wazalishaji wa Sukari nchini, Ammi Mpungwe, amesema tangu utabiri wa hali ya hewa ulipotangazwa na kuonesha kwamba kutakuwa na mvua za El Nino, wazalishaji waliwasiliana na mamlaka za Serikali kuzitaarifu kwamba Desemba mwaka jana kungekuwa na tatizo.

Kwa hivyo, waliomba utaratibu wa uagizaji sukari uwekwe.

Licha ya ufafanuzi huo, itakumbukwa siku chache zilizopita, kulikuwa na mijadala sehemu mbalimbali ikiwamo kwenye Bunge lililoahirishwa Ijumaa Juni 28, 2024 iliyokuwa ikiwatuhumu wafanyabiashara hayo kuhusika katika kusababisha bei ya sukari kupanda bei.

Baadhi ya watu katika mijadala hiyo walidai wazalishaji wanatengeneza nakisi ya sukari kwa makusudi ili waweze kujinufaisha, jambo ambalo Mpungwe anasema si kweli.

“Kulikuwa na mawasiliano na si mara moja wala mbili, tulikuwa tunakumbushia na kweli ilipofika Desemba hali ikaanza kuwa vile tulivyosema,” amedai Mpungwe.

Amesema cha kushangaza, hadi Desemba vibali vya kuagiza sukari vilikuwa havijatoka na Kampuni ya Sukari Kilombero ikalazimika kuizuia meli yake iliyokuwa inapeleka tani 45,000 ya sukari nchi nyingine na kuagiza iingizwe nchini kwa lengo la kufidia upungufu mkubwa uliojitokeza.

Mpungwe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kilombero Sugar, amesema si kweli kwamba kampuni hizo zilipewa vibali vya kuagiza sukari na kuviuza.

Amesema kazi ya uagizaji sukari kutoka nje si yao, wao ni wazalishaji tu na hulazimika kuingilia kati kwenye usambazaji kama kuna uhaba nchini kama walivyofanya kwa lengo la kukabiliana na uhaba na vurugu kama zilizokuwepo.

“Sisi kama Kilombero hatutaki kuingia katika biashara ya kuagiza sukari, tuko katika biashara ya kuzalishaji sukari, hili wazo la kuweka chombo cha Serikali kuagiza sukari nadhani lingekuja tangu mwanzo tungeunga mkono,” amesema Mpungwe.

Amesema wazalishaji hao waliamua kukaa kimya pale waliporushiwa maneno kwa sababu walikuwa wakiwasiliana na Spika wa Bunge ili wapate nafasi ya kuzungumza na Kamati ya Kilimo na Viwanda, lakini walipangiwa kukutana Agosti, mwaka huu.

“Tulipewa nafasi ya kukutana na kamati ya uchumi na bajeti wiki iliyopita, lakini ilikuwa ni kuzungumzia muswada wa fedha, tulijitahidi kuwa na mawasiliano lakini uamuzi umetoka bila sisi kuhusishwa tumekuwa watuhumiwa hadi tumehukumiwa bila sisi kusikilizwa,” amesema Mpungwe.

Amesema kutuhumiwa kwamba hawawafikirii Watanzania zaidi ya milioni 60 si sawa, kwa sababu wamefanya uwekezaji mkubwa unaodumu kwa zaidi ya miaka 60.

“Tumeshutumiwa kuwa sisi ni cartel ni tuhuma nzito katika biashara, huwezi kuwa na mpango mkubwa wa kuwekeza ukajiingiza katika mambo haya na tuhuma hizi haziamriwi kisiasa,” amesema.

Amesema kama kuna hofu kuwa wawekezaji hawa wanacheza mchezo mchafu kwenye biashara, wapelekwe Tume ya Ushindani (FCC), wakajibu tuhuma zao huko.

Naye Mwakilishi wa Bagamoyo Sugar, Hussein Sufian amesema kauli ya kuvitaka viwanda vya sukari kutoficha sukari wakati hakuna kiwanda kilichowahi kuficha sukari, sio sahihi.

Amesema wamejengewa taswira mbaya isiyo na ukweli kwa washirika wa maendeleo ya sekta ya sukari na umma kwa jumla.

Kuhusu dhamira ya kuondokana na uzalishaji sukari nchini ili kuleta sukari ya nje na wakulima kuhamasishwa kulima mazao mbadala kama mpunga, amesema inadhoofisha jitihada zilizokwishafanyika za kuleta utulivu kwenye sekta ya sukari.

Wakati hayo yakisemwa, Sufian amesema pia sekta hiyo inaendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya gharama kubwa za uzalishaji.

“Gharama za mahitaji muhimu kwa kilimo cha miwa na uzalishaji sukari zimeongezeka sana katika miaka ya hivi karibuni pia uwepo wa sera zisizotabirika za soko la sukari ni tatizo,” amesema Sufian.

Mwananchi ilimtafuta Msemaji wa Serikali, Thobias Makoba kutaka kujua undani wa malalamiko hayo, akajibu kwa ujumbe wa maandishi kuwa; “Ningekushauri kwa hoja kama hizi ni vyema ukaanza na wizara ya sekta husika.”

Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi alipoulizwa kuhusu barua zilizoandikwa na TSPA aliomba kutumiwa ujumbe mfupi ambao haukujibiwa.

Kwa upande wa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na Naibu wake, Joseph Silinde na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, GeraldMweri simu zao ziliita bila kupokelewa.
Mkuu wa kundi kubwa la wahalifu wa Marekani na Italia (Mafia Cartel) huitwa Capo di Tuti Capi (boss wa maboss)
Ami Mpungwe ndiye alikuwa mwenyekiti wa Tanzanite One kipindi madini hayo ya kiuzwa duninia na Africa Kusini alipokuwa balozi kuliko Tanzania yanapo chimbwa hadi mgodi ulipokauka akasepa.
Sasa Don Ami kahamia kwenye mgodi

mwingine uitwao sukari na kampuni ya Africa Kusini pia. True definition of Capo .
Sufiani wa Bagamoyo ana jiingiza kichwa kichwa kwenye haya mambo ambapo Bagamoyo sugar bado hawana clue sugar Cartel kwa Ina muda mfupi .
 
Back
Top Bottom