Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Mkuu, nakupata.Shida ni hii bei za sukari ni kubwa mno ukilinganisha na majirani zetu.
Speaker juzi aliwauliza wabunge bei za sukali nchi majirani ni wastani wa sh 2000 kwetu ni sh 4000.licha ya kuwa na viwanda kibao.
Huyu Mzee Balozi tunamheshimu,lakini ummoja wa wazalishaji nchini wametengeneza Cartel ya kutunyonya wananchi.
Pili hawajifunzi wanaendesha uzalishaji kizamani.Wakati wazalishaji Brazil wanazalisha mazao(byproduct) zaidi ya 30 kwenye miwa hiyo hiyo.kwao sukari ni byproduct 1 kati ya byproducts zaidi ya 30,hivyo sukari ina bei ndogo sana sh 600 tu.
Kama hawezi kujitanua jembe la Brazil litapiga hodi kuzalisha sukari na mazao kibao yatokanayo na sukari,itapunguza gharama ya uzalishaji pammoja na kuongeza ajira,na kuna uwezekano wa kutoagiza madawa au spirit,mbolea itokanayo na miwa. Nisikilizie mziku huo wanaogopa hata kivuli cha Brazil.
Lakini wakulima wa sasa serikali yapaswa kuwasaidia kulima kisasa kwa vifaa na pembejeo za maana na si kulima kwa jembe na si kuwashawishi vibaya waachane na kilimo hicho walime mazao mengine kama mpunga yaani tuwe twala wali tuu?
Wazo hilo la kuachana na kilimo cha miwa ulime mazao mengine ni wazo la kifisadi.
Wakulima wakubwa siku zote ndo husaidiwa kulima kwa wingi ili kupata kiasi kingi cha mavuno.
Hivyo hata hao vijana walokwenda huko Kilombero mashambani wasaidiwe kwa kupewa misahama ya kodi kwenye mitambo, vifaa na kila kihusianacho na kilimo cha miwa ili tusiwe na tatizo la Sukari.
Hawa wakulima wa sehemu zingine duniani hutumia mbinu zipi ili hata wale wazungu kule Ulaya wasiwe na shida ya sukari?
Yaani miaka zaidi ya 60 ya uhuru bado twazozana kuhusu Sukari kweli?