Umri unaenda aisee, nachanganyikiwa! Samahani niliowatukana kwasababu umri mkubwa halafu hawana kitu

Tajiri wa matajiri

Senior Member
Joined
Apr 17, 2024
Posts
166
Reaction score
649
Kiukweli hapa nilipo nachanyikiwa Sana wakuu sijui nifanyeje kiukweli Kama ingewezekana kuna uwezo wa kurudisha siku nyuma ningefanya hivyo lakini ndiyo hivyo haiwezekani hata kidogo aisee ndugu zangu mniombee kabisa

Unajua kipindi Niko kijana barobaro kwenye mwanzoni mwa miaka 20 nilikuwa nawasema watu wenye miaka kuanzia 30 inakuaje mpaka sasa haeleweki kumbe weeeh nilikuwa natukana mamba kabla sijavuka mto wakuu wakati nakaribia miaka 30 bado miaka 3 niikaribie Mambo yameanza kuwa vice Versa sijui ni laana za wana daaah sijui nifanyeje

Kumbe maisha ni Safari ndefu hivi? Sikuwahi kujua kabisa ila ndiyo hivyo sina budi kukubali na hali wakuu 😭😭😭😀😀 samahanini niliowananga watu humu jamii forum Na huku street nimeanza kumtembelea kila mtu Na kuanza kuwaomba msamaha.
 
Usijali ndugu yangu.Mimi hapa nina miongo mingi tangu nizaliwe sina kitanda wala shuka.Pa kulala sina.Ninalala kwa shemeji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…