Yaani miaka 30-35 ujute???labda kama uko jela kwa kutia mimba mwanafunzi,au umekatwa mikono kwa wizi.
Huo ndio muda wa kutafakari na kuchukua hatua kwa yale ambayo hukuyafanya kwa wakati sahihi.
Huu sio muda wa kukesha club na bar tena,sio muda wa kuendesha magari kwa speed kuangalia ya nani ina nguvu,hapa macho ya wengi yameanza kukuangalia afya ya mwili na akili ni muhimu sana,sio wakati wa kutafuta wanawake wenye makalio makubwa au wanaobebeka kirahisi kitandani.
Waliosema maisha yanaanzia 40 hawakukosea,maana huo ndio muda wa tathmini pia bado sio majuto.
Majuto ktk umri huu yanatakiwa yawe katika mfumo wa kushtuka,sio kukata tamaa.