Bro hizi sababu zote ulizotaja ndio huwa zinanisumbua sana na mimi,naomba ushauri wako bro
Naam,kama hizi sababu unazo basi hili ni tatizo la kisaikolojia kwa asilimia mia
Sasa kwanza nikufahamishe kitu kimoja,ubongo wako huwa unazifanyia kazi taarifa ambazo wewe umeziamini kuwa ni tatizo,yaan kwa kawaida sehemu ya ubongo ambayo huweka kumbukumbu za kudumu unaitwa subconscous mind,sasa sehemu hii huweka kumbukumbu za matukio ambayo umeyafanya haijalishi ni mazur au mabaya
Kwahiyo huwa na kawaida ya kuleta taarifa hizo na kuzifanyia kazi kila mara pale ambapo tukio fulani hufanyika ambalo linafanana na lile ulilofanya awali
Sasa kila ukikutana na mwenza wako,ubongo wako unaleta kumbukumbu la tendo hilo na kuamini kwamba ni sahihi wewe uume wako kulala,ni sahihi kuwa na hofu,kumbuka sehemu hii ya ubongo haijui kama ni tatizo kwako bali hutekeleza tu jambo hilo
Kwahiyo suluhisho ni kutoa taarifa hizo za awali katika file lako huko ubongoni na kuweka taarifa mpya ambazo zitakuwa nzuri kwako na ambazo unataka zifanyiwe kazi
Je utawekaje taarifa mpya? Ni kwanza ujue hilo ni tatizo hivyo usipaniki jua linatibika na kuondoka kabisa
Cha kufanya mweleze mwenza wako tatizo zima kuhusu wewe,na umtake akusaidie upone hiyo shida yako,namna gani anaweza kukusaidia ni kuelewa changamoto yako,pili akuvumilie pale unapokojoa mapema au pale uume unaposhindwa kusimama, ikiwezekana mwambie akupe maneno ya matumaini kwamba utakuwa sawa
Na wewe usijihukumu na kujilaumu kwanini umekuwa hivyo,tambua upo katika mchakato wa kupona,hata ukishindwa kufanya wewe chukulia poa tu,baada ya mda fulani hizo taarifa hazitakuwa na nguvu na hazitafanyiwa kazi na ubongo wako,tambua kwamba ubongo unazifanyia kazi taarifa ambazo unaziwekea nguvu na zile zinazo puuzwa huachwa na kupotea kabisa
Baada ya mda ubongo wako utaweka taarifa mpya kutokana na uzoefu mpya na hatimaye shida yako itaisha kabisa,tambua kuwa itakuchukua mda kidogo kutoka lkn amini utapona,kikubwa jitahidi kutowaza kwamba utashindwa au kuhaibika,wewe usijali yaan jifanye kama hakuna kitu ambacho kimetokea,nasisitiza ukiwa na mwenza ambaye ataelewa shida yako atakusaidiq sana kwakuwa utakuwa huru naye
Hiyo shida yako ipo mawazoni kwako tu kwahiyo ukifanikiwa kuyabadilisha mawazo yako na kufikiria katika namna chanya hakika utapona na kuwa vizur kabisa
Kila la kheri