Mradi wa steiglers gorge ni unnecessary na ecological destructive, hilo halina mjadala.
Tuna gesi ambayo mpaka leo iko under utilised.
Tuna makaa ya mawe, the cheapest source of energy tunayoweza kutumia. Its destructive pia lakini on the good side yako kwenye maeneo ambayo ni remote and not in one of the largest protected reserve site in the world.
Tuna uwezo wakuproduce wind energy in a large quantity, ila mpaka leo hakuna any signs ya kuanzisha mradi huo.
Tuna a long coastline yenye uwezo wakutuwezesha kuproduce energy kupitia tidal waves.
Ila vyote hivyo hamna mpango navyo au hamtaki kuvitekeleza in full.
Juzi juzi a few years back serikali imetoka kuiomba UN kufanya boundary change ya selous kwa ajili ya uranium mining ambayo in the end itakuja kuproduce a ton of radioactive waste ambayo ita-affect the game reserve.
Hapo hapo kuna swala la ujangili humo kwenye hiyo reserve, kwenye idadi ya tembo wameshuka toka 60,000+ in 2009 mpaka 10,000 in 2013.
Tena sasa mnataka mjenge a hydro plant ambayo ita-flood a large area of the reserve na kuharibu the ecosystem ya eneo hilo,just from the construction alone.
Yani sisi ni kuharibu haribu tuu...
Hydro plants zetu nyingi if not all, zimetengenezwa wakati wa mkoloni, hivi mnadhani wangeshindwa kujenga hiyo hydro plant kwenye hiyo reserve. Mnadhani ni wajinga sana mpaka wakaamua kuachana na hiyo idea. Tena walikuwa na uwezo both financially na engineering wise, kwasababu kama waliweza kutekeleza a large project such as reli ya kati, project kama hii isingewashinda.
Muda mwingine tusiwe wabishi, natuangalie impact ya vitu tunavyotaka kufanya.
Mkuu wewe inaelekea ni kijana wa juzi juzi tu.
Miradi karibu yote ya Hydro imejengwa na Mwalimu.
Hata huu wa Stieglers Gorge ulikuwa kwenye drawing boards.
Mimi nimeingia ndani ya Kidatu na kuona zile 4 turbines zinazofua 200MW, cha mtoto.
Nimebahatika vile vile kuingia NDANI ya Nuclear Plant moja huko Ulaya, yenye ukubwa kama jengo la Yanga.
Hiyo Plant ilikuwa inatoa 900MW!
Sasa leo hao UN waambie wakusaidie ujenge plant kama hiyo hapa nchini , wataishia kukulisha studies kama unavyozionyesha za kwako hapa mtandaoni!
Tatizo kubwa watanzania mmeaminishwa na kulishwa maneno ambayo in principle ni defeatist, mwadhani maendeleo ni lelemama na yatakuja kwa feasibility studies.
Mrusi Yuri Gagarin, binadamu wa kwanza anga za juu, alifanyiwa feasibility study ipi kufanikiwa!
Na je ile Apollo mission iliyilipuka na kuua wanaanga karibu nane wa kimarekani, yenyewe haikufanyiwa any studies?
Maendeleo ni multifaceted.
Gesi tutaitumia, makaa ya mawe yatatumika.
Wengi wenu muishio Dar wala hamjui na hamjafika maeneo ya nishati hizo, zinatumika hata leo.
Tukitegemea maendeleo yetu yatakuja kwa kumfurahisha mzungu aliyekutawala, wengine hata kiakili, maendeleo yatachelewa sana.