Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,192
- 1,972
Nimesoma katika gazeti la The Guardian on sunday, tar 25 Feb 2018, ati UN(Umoja wa Mataifa), wanapinga kujengwa kwa kituo cha kuzalisha umeme kiasi cha 2,100MW ati kwa sababu za mazingira.
Huu ni uhujumu, full stop!
UN inatumiwa tu, ili ujumbe uonekane ati unatoka chombo ambacho ni fair, lakini ujumbe huo ni lazima unatoka nchi zinazofaidika na matatizo yetu ya nishati.
Kampuni za kimarekani kama AGGREKO, DOWANS na nyingine nyingi ni wazi zisingependa kuona mradi huu wa Stieglers Gorge ukifanikiwa, maana watakosa ulaji wanaofaidika nao leo.
Kama ingewapendeza UN, basi Three Gorges Dam ya China, Aswan Dam ya Misri, Akosombo Dam ya Ghana vyote visingejengwa kwa sababu za kimazingira.
Nampongeza sana Rais Magufuli na kumpa moyo kushika moyo ule ule , ili nchi ijitawale kinishati.
Ukiona Shetani anakupiga vita ujue uko sahihi, kaza mwendo! Ukiona Shetani anakuchekea ujiulize umekosea wapi! Pia ukiona UN na US wanakupiga vita ujue uko sahihi, kaza mwendo!
Ukiona hao watu wanakusifia ujue kuna mahali umekosea, tafuta hilo kosa jirekebishe, songa mbele!
Walianza na TAZARA, sasa hivi wamegeukia Umeme wetu wa SG!
Hivi na sisi tunaweza kuwapinga katika project zao zozote, km vita vya Iraq na Libya, hivyo vita haviharibu mazingira ukiachilia mbali vifo vya watu wasio na hatia?
Dr John P. J. Magufuli, usiwasikilize, sio watu wazuri hawa, wana uchungu wa makinikia uliyoyazuia Bandarini. Kaza mwendo baba!