UN kupinga mradi wa Steigler's Gorge ni uhujumu

UN kupinga mradi wa Steigler's Gorge ni uhujumu

Nani anayependa wazungu kuliko serikali ambayo ndio moja ya wakopaji na wafutiwa madeni wakubwa na wazungu afterall waliingia mikataba mibovu kuanzia gesi hadi madini na kusababisha hasara ya trillion zaidi ya 400 kwa mujibu wa ripoti za kamati zote 4!!!! Nani mpenda wazungu hapo
Hata wewe unakopa, kukopa unakopa popote.
 
Hapana hajapinga anashangaa tu serikali ilisema gesi ndio suluhu ghafla tena tunarudi kwenye umeme wa kutegemea maji!!!!

Yaani kwa kuwa umeme wa gesi tulishaanza kufua basi pesa hyo ya stiegler ielekezwe kwingine mfano kilimo au uvuvi n.k ili nchi isonge mbele maadam alternative ipo kuliko miradi miwili target moja wakati kuna watu wanategemea kilimo cha mvua bado na wapo karne ya 21.... Kwanni msiwekeze huko kila siku umeme umeme wakati gesi ipo
Ni rahisi kupinga kuliko kuimplement
 
Tujenge tu ...UN wakapambane na ISRAEL KUHUSU JERUSALEM
 
Hata wewe unakopa, kukopa unakopa popote.
Basi kama mnakopa na mnafutiwa madeni pamoja na kuomba msaada kwao ambao mpaka mwaka jana mlikuwa mmeshafutiwa madeni ya thamani ya trillion 20 je kiburi cha kuwatukana mnatoa wapi.... Kama hawawapendi wangewafutia madeni??
 
Yeah MLISEMA maana nachukulia wwe mtoa taarifa umechukua upande wa serikali kwenye kutetea mradi wa Stiegler's.... Hivyo serikali hiyo hiyo ambayo leo inasema SG ndio habari ya mujini ilisema miaka 4 iliopita kwamba Gesi ndio suluhu la nishati ya umeme hapa TZ hivyo nashangaa badala nyie wasomi mhoji hizo ahadi za gesi kama zimefikia malengo ndio kwanza mnatuminisha tena kwamba SG ndio mradi wa kumaliza shida ya umeme.... Hivi hizi ahadi mpaka lini?? Wasomi tunawategemea muhoji ndio kwanza mnasupport huu ujinga wa SG

Huoni tuna miradi mingi inahitaji funding hasa ya maji vijijini ama ya kilimo cha umwagiliaji au hata kuongeza ndege kwa ajili ya ATCL..... We have a way lot than switching lanes every now on then be it from hydro to coal to gas.... And then guess what!! We are talkin about hydro again???

Duh kazi ipo
Best solution ni wewe kuendelea kushangaa pembeni wakati watu wana piga kazi
No explanation will satisfy you.
 
Ni rahisi kupinga kuliko kuimplement
Hahahaha naona umekimbia mada yako kule kuhusu waarab na wazungu!!

nilichogundua unapenda kukariri.... Ssa wapi nmepinga?? Nachosema kwakuwa serikali ilishaanza kuwekeza umeme wa gesi basi hizi pesa za stiegler zielekezwe kwenye miradi mingine mfano ya maji vijijini ili waanze kilimo cha umwagiliaji sasa kwani kushauri ndio kupinga
 
Best solution ni wewe kuendelea kushangaa pembeni wakati watu wana piga kazi
No explanation will satisfy you.
Wana piga kazi!!! Kwani gesi hawakupiga kazi?? Mbona bado mgao upo na hauna dalili ya kuisha!!!

Nakukumbusha tu mwaka wa 3 huu bajeti ya maendeleo imetekeleza below 50% na kuna wizara imetekelezeka mpaka 10%.... Haya endeleeni kushabikia tu maneno ya wanasiasa huku uchumi unazidi kufa mkishauriwa mnaanza eti hujuma sijui wazungu cjui wapinzani!!! Hatutafika kokote ukileta mada uwe tayari kukosolewa na kurekebishwa sio unaleta mada unategemea tushabikie tu

Kwa staili hii kufikia uchumi wa viwanda itachukua miaka 200
 
Mradi wa steiglers gorge ni unnecessary na ecological destructive, hilo halina mjadala.

Tuna gesi ambayo mpaka leo iko under utilised.
Tuna makaa ya mawe, the cheapest source of energy tunayoweza kutumia. Its destructive pia lakini on the good side yako kwenye maeneo ambayo ni remote and not in one of the largest protected reserve site in the world.
Tuna uwezo wakuproduce wind energy in a large quantity, ila mpaka leo hakuna any signs ya kuanzisha mradi huo.
Tuna a long coastline yenye uwezo wakutuwezesha kuproduce energy kupitia tidal waves.
Tuna uwezo wa kupower miji mingi midogo Tanzania kwa kutumia umeme wa jua tu.

Ila vyote hivyo hamna mpango navyo au hamtaki kuvitekeleza in full.

Juzi juzi a few years back serikali imetoka kuiomba UN kufanya boundary change ya selous kwa ajili ya uranium mining ambayo in the end itakuja kuproduce a ton of radioactive waste ambayo ita-affect the game reserve.

Hapo hapo kuna swala la ujangili humo kwenye hiyo reserve, kwenye idadi ya tembo wameshuka toka 60,000+ in 2009 mpaka 10,000+ in 2013. Tumekaa tu, wala hakuna serious effort kukabiliana na hilo.

Tena sasa mnataka mjenge a hydro plant ambayo ita-flood a large area of the reserve na kuharibu the ecosystem ya eneo hilo,just from the construction alone.

Yani sisi ni kuharibu haribu tuu...

Hydro plants zetu nyingi if not all, zimetengenezwa wakati wa mkoloni, hivi mnadhani wangeshindwa kujenga hiyo hydro plant kwenye hiyo reserve. Mnadhani ni wajinga sana mpaka wakaamua kuachana na hiyo idea. Tena walikuwa na uwezo both financially na engineering wise, kwasababu kama waliweza kutekeleza a large project such as reli ya kati, project kama hii isingewashinda.

Muda mwingine tusiwe wabishi, natuangalie impact ya vitu tunavyotaka kufanya.
Tabia za Ki-Mugabe za kushutumu "weupe"ili kuonekana mzalendo.

Maendeleo hayana itikadi,ujanja ujanja,uhuni,visasi na misifa!

Kelele zote za Sizonje za "hela zipo" hata leo ni "defensive. Ukweli ni maji ya shingo , ndo maana wanaibuka n.a. buku 3 kwa sticker n.a. Mpango kukiri mambo so shwari!

Akubali kushauriwa n.a. aache "bigotry,arrogance".
 
View attachment 701335

Nimesoma katika gazeti la The Guardian on sunday, tar 25 Feb 2018, ati UN(Umoja wa Mataifa), wanapinga kujengwa kwa kituo cha kuzalisha umeme kiasi cha 2,100MW ati kwa sababu za mazingira.

Huu ni uhujumu, full stop!

UN inatumiwa tu, ili ujumbe uonekane ati unatoka chombo ambacho ni fair, lakini ujumbe huo ni lazima unatoka nchi zinazofaidika na matatizo yetu ya nishati.

Kampuni za kimarekani kama AGGREKO, DOWANS na nyingine nyingi ni wazi zisingependa kuona mradi huu wa Stieglers Gorge ukifanikiwa, maana watakosa ulaji wanaofaidika nao leo.

Kama ingewapendeza UN, basi Three Gorges Dam ya China, Aswan Dam ya Misri, Akosombo Dam ya Ghana vyote visingejengwa kwa sababu za kimazingira.

Nampongeza sana Rais Magufuli na kumpa moyo kushika moyo ule ule , ili nchi ijitawale kinishati.
Brother issue sio dam...bali dam iko sehemu gani na ina athari gani kwa ikolojia
 
Huo mradi ukifanikiwa naama nchi.... ..hakuna hata kimoja atafanikisha herode..... Maana kila kitu anadandia dandia tu hata plan hana
 
Mkuu wewe inaelekea ni kijana wa juzi juzi tu.
Miradi karibu yote ya Hydro imejengwa na Mwalimu.
Hata huu wa Stieglers Gorge ulikuwa kwenye drawing boards.

Mimi nimeingia ndani ya Kidatu na kuona zile 4 turbines zinazofua 200MW, cha mtoto.
Nimebahatika vile vile kuingia NDANI ya Nuclear Plant moja huko Ulaya, yenye ukubwa kama jengo la Yanga.
Hiyo Plant ilikuwa inatoa 900MW!
Sasa leo hao UN waambie wakusaidie ujenge plant kama hiyo hapa nchini , wataishia kukulisha studies kama unavyozionyesha za kwako hapa mtandaoni!

Tatizo kubwa watanzania mmeaminishwa na kulishwa maneno ambayo in principle ni defeatist, mwadhani maendeleo ni lelemama na yatakuja kwa feasibility studies.

Mrusi Yuri Gagarin, binadamu wa kwanza anga za juu, alifanyiwa feasibility study ipi kufanikiwa!
Na je ile Apollo mission iliyilipuka na kuua wanaanga karibu nane wa kimarekani, yenyewe haikufanyiwa any studies?

Maendeleo ni multifaceted.
Gesi tutaitumia, makaa ya mawe yatatumika.
Wengi wenu muishio Dar wala hamjui na hamjafika maeneo ya nishati hizo, zinatumika hata leo.

Tukitegemea maendeleo yetu yatakuja kwa kumfurahisha mzungu aliyekutawala, wengine hata kiakili, maendeleo yatachelewa sana.

Hii ndo shida yenu watu wakiwashauri jambo mnadhani mnahujumiwa.

Mradi wa steiglers gorge ulikuwepo tongea zamani, tena kwa different studies na mapping ya rufiji river and basin na wajerumani in 1904, 1907, 1909 na 1911. Major staudies of the basin tena zikafanyika in 1928, tena zikafanyika in 1954... Wajerumani walikuwa wafanya extensive survey ya Rufiji basin kwa ajili ya navigation(before they settled kwa reli ya kati), umeme na irrigation. Waingereza walifanya survey kwaajili development of rufiji basin ikuhusisha irrigation na hydro dam.

Mkuu usi-dismiss faida ya feasibility studies. Especially kwenye miradi mikubwa kama hii zina umuhimu wake.

Mkuu kabla ya binadamu wa kwanza kwenda angani, wanyama mbalimbali walirushwa, kuangalia impact yake. Hawakuanza tu na kurusha binadamu moja kwa moja. Kwahiyo point yako is moot. Hiyo ya ndege kuungua was an accident everyone knows it.

Yes maendeleo ni multi-faceted, lakini tusitumie hicho kigezo kuharibu nchi na mazingira tuliyonayo.
 
Ni kweli ila pia sio dalili nzuri sana kwa yanayotunyemelea maana inaonekana kana kwamba tunatengwa kiaina kimataifa. Huku UN kule US kwa issue ya ushirikiano na NK. Si busara kusema tu "shikilia hapo hapo"; wao wameshikilia mpini sisi makali. Busara ni kutafuta suluhu sahihi ya namna ya kutoka tuliponasa ili tusonge mbele bila mikwaruzano isiyo ya lazima na "wakubwa". Mwisho wa siku tutaumia sisi tukiendelea kushupaza shingo. Sina hakika kama utanielewa.

Pole mkuu lakini naona umepoteza muda wako kumjibu. Akikuelewa nijulishe!!!!
 
UN wanatushangaa kwani tuna nishati mbadala yaani gesi asilia LAKINI hiyo mikataba mfu kutumia gesi yetu tuliopewa bure na Mwenyezi Mungu ni aghali kwa sababu ya mikataba mibovu hatuna chetu,Hadi leo umeme wa Song gas ni wa gharama sana.Wazungu wanaona tuna njia nyingine nyingi za kufua umeme bila kuadhiri mazingira,lakini ndio tulishafulia na hao walioifilisi nchi bado mnawaita waheshimiwa!wanadunda,kazi yetu sasa ni kununua kununua "MALAIKA" wa kisasa.
Ni bora kwa hali ya sasa ili tusirudie makosa,miradi yote mikubwa ijadiliwe na wananchi hasa walimu wana weza wakawa bunge mbadala badala ya hao weheshimiwa wanaoleta miswaada muhimu kwa hati dharura bila kupata muda wa kutosha kuisoma wakaielewa ndio ijadiliwe kwa mapana.
 
Bro, mbona unaongea upuuz? Kwaakili yako unadhani upo uwezekano wa kuyafanya yote hayo kwa pamoja?...kijana jifunze siasa za kinataifa..... Na usijifnye unjua sanaaa? Kumbe mpuuz tu

Hii ndo shida ya kusoma vitu bila kuelewa, nani kasema lazima kutekelezwa vyote. Shida iliyopo hata ni kurukia rukia vitu halafu serikali haivitekelezi to the fullest na vilivyopo haziendelezwi. Tena the worst thing wamerukia kitu ambacho kina negative impact kubwa kimazingira.
 
View attachment 701335

Nimesoma katika gazeti la The Guardian on sunday, tar 25 Feb 2018, ati UN(Umoja wa Mataifa), wanapinga kujengwa kwa kituo cha kuzalisha umeme kiasi cha 2,100MW ati kwa sababu za mazingira.

Huu ni uhujumu, full stop!

UN inatumiwa tu, ili ujumbe uonekane ati unatoka chombo ambacho ni fair, lakini ujumbe huo ni lazima unatoka nchi zinazofaidika na matatizo yetu ya nishati.

Kampuni za kimarekani kama AGGREKO, DOWANS na nyingine nyingi ni wazi zisingependa kuona mradi huu wa Stieglers Gorge ukifanikiwa, maana watakosa ulaji wanaofaidika nao leo.

Kama ingewapendeza UN, basi Three Gorges Dam ya China, Aswan Dam ya Misri, Akosombo Dam ya Ghana vyote visingejengwa kwa sababu za kimazingira.

Nampongeza sana Rais Magufuli na kumpa moyo kushika moyo ule ule , ili nchi ijitawale kinishati.
Wangepinga alafu watoe mbadala sio kupinga tu for the sake of kupinga.
Kwa mfano wangesema instead tutawapa hela mjenge Geothermal au Gas Power Plants kufidia hizo MW 2000.
 
mkuu hakuna project ambayo mkoloni aliitekeleza bila kuna na faida kwake kiuchumi, as hakua na lengo la kuiendeleza nchi kiviwanda, large projects za umeme hazikua na maana kwake. Na si kisingizio cha mazingira. Maana wangekua wanajali mazingira wasingetoboa ozone layer, hadi leo wasingeumiza watu na viumbe Niger delta.

Mkuu wakoloni both wajerumani na waingereza walifanya assessment na survey kubwa katika rufiji basin kwa nia ya kuindeleza, tena aim ilikuwa kwaajili ya agricultural irrigation, navigation na umeme. Tena zilifanyika mara nyingi nyingi in different years. Steiglers gorge came up multiple times as a good place ya kujenga dam kwaajili ya irrigation, umeme na fishing, ila waliachana nayo kutokana na environmental impact. Sisi wenyewe idea ya kujenga dam tumeitoa kwao ila tunajidai vichwa ngumu hatutaki kuelewa impact yake kimazingira.
 
Marekani kabanwa sasa anaamua kuonesha sura yake ya kishetani hapa ulimwenguni, Americans are evils!
 
Naona hili Tundu lissu hajalipata vizuri. Ngoja tu! Atakuja na maneno makali hayo! Wazungu watatutenga! Watatunyima misaada! Umeme kitu gani bhana! Sheria za kimataifa zinazuia!, nk.
 
Back
Top Bottom