UN kupinga mradi wa Steigler's Gorge ni uhujumu

UN kupinga mradi wa Steigler's Gorge ni uhujumu

Una mawazo ya ujima, kwa vile umeshazoea na kuzoea kuishi kwenye nyumba za koroboi
Maji yanapopungua duniani ndio mradi mkubwa wa hydro unataka kuanzishwa.

Mtera miaka mingi sasa maji hayatoshi, na kama Mtera maji ni tatizo basi kidatu nayo itakuwa kwenye mkumbo huo huo

Mvua kadri miaka inaposonga inazidi kupungua tusije maliza kujenga kisha maji yakawa hayatoshi na hivyo return ikawa ni sawa na ziro

Study ya maji ya miaka ya 70 haiwezi kuwa sahihi kwa sasa kwani kumeshuhudiwa mabadiliko makubwa ya tabia nchi
 
Mkuu wewe inaelekea ni kijana wa juzi juzi tu.
Miradi karibu yote ya Hydro imejengwa na Mwalimu.
Hata huu wa Stieglers Gorge ulikuwa kwenye drawing boards.

Mimi nimeingia ndani ya Kidatu na kuona zile 4 turbines zinazofua 200MW, cha mtoto.
Nimebahatika vile vile kuingia NDANI ya Nuclear Plant moja huko Ulaya, yenye ukubwa kama jengo la Yanga.
Hiyo Plant ilikuwa inatoa 900MW!
Sasa leo hao UN waambie wakusaidie ujenge plant kama hiyo hapa nchini , wataishia kukulisha studies kama unavyozionyesha za kwako hapa mtandaoni!

Tatizo kubwa watanzania mmeaminishwa na kulishwa maneno ambayo in principle ni defeatist, mwadhani maendeleo ni lelemama na yatakuja kwa feasibility studies.

Mrusi Yuri Gagarin, binadamu wa kwanza anga za juu, alifanyiwa feasibility study ipi kufanikiwa!
Na je ile Apollo mission iliyilipuka na kuua wanaanga karibu nane wa kimarekani, yenyewe haikufanyiwa any studies?

Maendeleo ni multifaceted.
Gesi tutaitumia, makaa ya mawe yatatumika.
Wengi wenu muishio Dar wala hamjui na hamjafika maeneo ya nishati hizo, zinatumika hata leo.

Tukitegemea maendeleo yetu yatakuja kwa kumfurahisha mzungu aliyekutawala, wengine hata kiakili, maendeleo yatachelewa sana.
Hiyo nuclear plant unayosema am sure ipo kwenye nchi inayojitegemea kila kitu hivyo UN haina ubavu wa kuinterfere sana sasa nyie kila kitu kukopa kwa wazungu na worldbank alafu wakiwapangia hamtaki!! Kumbuka mikopo mingi ina masharti yake mengineyo yakitaka m-sign makubaliano ya issue za mazingira n.k sasa kwanini wakiisimamia mnaanza mapovu!! Jitegemeeni muone kama watawapangia mambo ila kopa kopa hii imefika trillion 80 alafu mkipangiwa mnalialia ndio nn ssa wakati mliyataka wenyewe

Kingine unasema makaa ya mawe na gesi na SG zitumike zote!!! Are you serious?? Ina maana kipaumbele cha Tanzania ni kufua umeme kwenye kila mradi tena hata kabla wa gesi haujakamilika??? Muhongo tulimsikia wote alisema Gesi ndio suluhu ya tatizo la umeme Tanzania na alisema ile ya kinyerezi itamaliza mgao rasmi ila mpaka leo maeneo mengi dar umeme wa kubangaiza..... Sasa kabla hamjamalizana na gesi ya lindi mshakimbilia Stiegler's gorge ina maana taifa mnakosa vipaumbele !!

Kwanini msimalizane na gesi kwanza alafu ndio muingie kwenye SG.... Au hizo pesa za SG mngewekeza kwenye kilimo hasa cha umwagiliaji ili maisha ya wakulima ambao ndio majority ya Tanzania yakuwe kiuchumi!!! Why hamtuliii mlisema gesi mtauza umeme mpaka DRC afu leo hii mnasema SG ndio kila kitu

Tuwaeleweje
 
Kwa Magu wataula wa chuya! Prezdaa Magu songa mbele baba, kurudi nyuma, mwiko!
Kwa mazuri unayofanya tuko nyuma yako, yale mengine hapana!
Hehehee wakati hao hao anawafuata wamkopeshe hela ya kujenga Reli!! Mnaleta kiburi wakati mnawategemea
 
Msitake kujifanya mnaipinga UN kuhusu kugomea huo mradi, ukweli kuhusu ujenzi wa huo mradi ni kukosa hela. Laiti hela zingekuwepo leo hii huo mradi ungekuwa umeshaanza. Awamu iliyopita kelele ilikuwa ni uchumi wa gas, leo hii hakuna anayeongelea gas na tunataka kurukia mradi mwingine huku hakuna hata cent kumi. Pata majibu ya msingi kwanza kwanini sio gas bali ni stiegler gorge?
Tungekuwa na Malengo yetu kama Taifa. Malengo hayo yasingekuwa yanabadilishwa na Political Leaders bali wao wangekuwa wanatakiwa kuyatekeleza kwa kupokezana vijiti. Imagine after 2025 anakuja Political Leader mwingine anaturudisha kwenye Umeme wa Gas wakati Umeme wa Stiglers Gorges haujapatiwa ufumbuzi.
 
Tusipende kutupia lawama kwa wengine pale tunaposhindwa kufanikisha mipango yetu.....nadhani kabla hatujaanza ujenzi wa hilo Bwawa, tuhoji kwanza matumizi ya Gesi.....zile ahadi kuwa kukatika kwa umeme kutakuwa historian kumeishia wapi?
Sipingi huo ujenzi, ninachotaka ni kuhakikishiwa matokeo ya Ujenzi, kule Mtwara watu walivunjwa Miguu, wengine kupoteza maisha kwa kisingizio cha wanazuia maendeleo.
Tumemkabidhi lori dereva kipovu na kiziwi twafwaaaaaaaa ?!!!!
 
Maji yanapopungua duniani ndio mradi mkubwa wa hydro unataka kuanzishwa.

Mtera miaka mingi sasa maji hayatoshi, na kama Mtera maji ni tatizo basi kidatu nayo itakuwa kwenye mkumbo huo huo

Mvua kadri miaka inaposonga inazidi kupungua tusije maliza kujenga kisha maji yakawa hayatoshi na hivyo return ikawa ni sawa na ziro

Study ya maji ya miaka ya 70 haiwezi kuwa sahihi kwa sasa kwani kumeshuhudiwa mabadiliko makubwa ya tabia nchi
Mkuu unayosema ndiyo mnayolishwa na wazungu myakariri ili msiendelee ku think outside the box.
Google The Roosevelt Dam huko Marekani lilojengwa miaka ya 1910.

Mkuu hilo ndo wazungu wanapenda ulikariri ili usiendelee daima.
Amka usingizini.
 
Mambo niliyosikia kuhusu gesi,Leo hakuna mtu atakayeniaminisha kuna mradi mwingine wowote eti utamaliza matatizo ya nishati!Wanasiasa ni waongo na matapeli wakubwa!
Tuongee mambo mengine na si utapeli tapeli sijui UN sijui umeme..suluhisho la nishati!Utapeli tu!
 
Mambo muhimu yanajadiliwa kisiasa na kiumbeaumbea no fact zozote zenye mashiko. Hebu mleta hoja unaye pinga ya UN njoo na point zenye mashiko za kuwapinga Hawa wakoloni UN.
NInavyohisi hakuna haja ya kuja na chochote. Hilo gazeti kama limeandika hayo, basi mwandishi hajitambui. Au, aliyesoma hajui walichokiandika. UN haijawahi kujihusisha na mambo kama hayo. UN chombo kipi? Baraza la usalama? Kitu gani kinachoitwa UN?
 
Mradi wa steiglers gorge ni unnecessary na ecological destructive, hilo halina mjadala.

Tuna gesi ambayo mpaka leo iko under utilised.
Tuna makaa ya mawe, the cheapest source of energy tunayoweza kutumia. Its destructive pia lakini on the good side yako kwenye maeneo ambayo ni remote and not in one of the largest protected reserve site in the world.
Tuna uwezo wakuproduce wind energy in a large quantity, ila mpaka leo hakuna any signs ya kuanzisha mradi huo.
Tuna a long coastline yenye uwezo wakutuwezesha kuproduce energy kupitia tidal waves.
Tuna uwezo wa kupower miji mingi midogo Tanzania kwa kutumia umeme wa jua tu.

Ila vyote hivyo hamna mpango navyo au hamtaki kuvitekeleza in full.

Juzi juzi a few years back serikali imetoka kuiomba UN kufanya boundary change ya selous kwa ajili ya uranium mining ambayo in the end itakuja kuproduce a ton of radioactive waste ambayo ita-affect the game reserve.

Hapo hapo kuna swala la ujangili humo kwenye hiyo reserve, kwenye idadi ya tembo wameshuka toka 60,000+ in 2009 mpaka 10,000+ in 2013. Tumekaa tu, wala hakuna serious effort kukabiliana na hilo.

Tena sasa mnataka mjenge a hydro plant ambayo ita-flood a large area of the reserve na kuharibu the ecosystem ya eneo hilo,just from the construction alone.

Yani sisi ni kuharibu haribu tuu...

Hydro plants zetu nyingi if not all, zimetengenezwa wakati wa mkoloni, hivi mnadhani wangeshindwa kujenga hiyo hydro plant kwenye hiyo reserve. Mnadhani ni wajinga sana mpaka wakaamua kuachana na hiyo idea. Tena walikuwa na uwezo both financially na engineering wise, kwasababu kama waliweza kutekeleza a large project such as reli ya kati, project kama hii isingewashinda.

Muda mwingine tusiwe wabishi, natuangalie impact ya vitu tunavyotaka kufanya.
Bro, mbona unaongea upuuz? Kwaakili yako unadhani upo uwezekano wa kuyafanya yote hayo kwa pamoja?...kijana jifunze siasa za kinataifa..... Na usijifnye unjua sanaaa? Kumbe mpuuz tu
 
Hiyo nuclear plant unayosema am sure ipo kwenye nchi inayojitegemea kila kitu hivyo UN haina ubavu wa kuinterfere sana sasa nyie kila kitu kukopa kwa wazungu na worldbank alafu wakiwapangia hamtaki!! Kumbuka mikopo mingi ina masharti yake mengineyo yakitaka m-sign makubaliano ya issue za mazingira n.k sasa kwanini wakiisimamia mnaanza mapovu!! Jitegemeeni muone kama watawapangia mambo ila kopa kopa hii imefika trillion 80 alafu mkipangiwa mnalialia ndio nn ssa wakati mliyataka wenyewe

Kingine unasema makaa ya mawe na gesi na SG zitumike zote!!! Are you serious?? Ina maana kipaumbele cha Tanzania ni kufua umeme kwenye kila mradi tena hata kabla wa gesi haujakamilika??? Muhongo tulimsikia wote alisema Gesi ndio suluhu ya tatizo la umeme Tanzania na alisema ile ya kinyerezi itamaliza mgao rasmi ila mpaka leo maeneo mengi dar umeme wa kubangaiza..... Sasa kabla hamjamalizana na gesi ya lindi mshakimbilia Stiegler's gorge ina maana taifa mnakosa vipaumbele !!

Kwanini msimalizane na gesi kwanza alafu ndio muingie kwenye SG.... Au hizo pesa za SG mngewekeza kwenye kilimo hasa cha umwagiliaji ili maisha ya wakulima ambao ndio majority ya Tanzania yakuwe kiuchumi!!! Why hamtuliii mlisema gesi mtauza umeme mpaka DRC afu leo hii mnasema SG ndio kila kitu

Tuwaeleweje
Mkuu usipende kubisha kwa sababu una hobby hiyo!
Usha wahi kusikia mpango wa msaada mkubwa kwa Ulaya toka Marekani baada ya WWII iitwayo Marshal Plan?
 
Nimesoma katika gazeti la The Guardian on sunday, tar 25 Feb 2018, ati UN(Umoja wa Mataifa), wanapinga kujengwa kwa kituo cha kuzalisha umeme kiasi cha 2,100MW ati kwa sababu za mazingira.

Huu ni uhujumu, full stop!

UN inatumiwa tu, ili ujumbe uonekane ati unatoka chombo ambacho ni fair, lakini ujumbe huo ni lazima unatoka nchi zinazofaidika na matatizo yetu ya nishati.

Kampuni za kimarekani kama AGGREKO, DOWANS na nyingine nyingi ni wazi zisingependa kuona mradi huu wa Stieglers Gorge ukifanikiwa, maana watakosa ulaji wanaofaidika nao leo.

Kama ingewapendeza UN, basi Three Gorges Dam ya China, Aswan Dam ya Misri, Akosombo Dam ya Ghana vyote visingejengwa kwa sababu za kimazingira.

Nampongeza sana Rais Magufuli na kumpa moyo kushika moyo ule ule , ili nchi ijitawale kinishati.
Soma vizuri uelewe ndo utusimulie. UN ni nini? Tangu lini UN ikafanya hayo? Ndani ya UN kuna vyombo vingi, ni kipi kilicholeta hayo?
 
Mkuu unayosema ndiyo mnayolishwa na wazungu myakariri ili msiendelee ku think outside the box.
Google The Roosevelt Dam huko Marekani lilojengwa miaka ya 1910.

Mkuu hilo ndo wazungu wanapenda ulikariri ili usiendelee daima.
Amka usingizini.
Mkuu tujadiliane kwa uhuru na amani bila kushutumiana au kukashfiana maana hatushindani

Kupungua kwa maji Mtera wanalisema wazungu?

Mito mingi ya zamani haipitishi maji tena nalo unataka kuwasingizia wazungu?

Tunahitaji kufanya study tena 2100Mw ya miaka ya 70 hauwezi kuwa leo, vitu vingi vimebadilika na vitaendelea kubadilika
 
image.jpeg
NInavyohisi hakuna haja ya kuja na chochote. Hilo gazeti kama limeandika hayo, basi mwandishi hajitambui. Au, aliyesoma hajui walichokiandika. UN haijawahi kujihusisha na mambo kama hayo. UN chombo kipi? Baraza la usalama? Kitu gani kinachoitwa UN?
Haya mzee hebu jinafasi, kwa wewe unayejua kila kitu!
 
View attachment 701334
Haya mzee hebu jinafasi, kwa wewe unayejua kila kitu!
Hiyo ni heading ya gazeti. Soma ndani uelewe wana maana gani? UN mkuu wake ni Secretary general. Baraza la usalama lina mkuu wake anaitwa rais. Ukisoma ndani lazima utagundua uzembe wa msomaji. UN as UN ni chombo cha kisiasa, haiwezi kuzungumzia ujenzi wa bwawa. Never! Au ni UNESCO, Au ni UNEP au nini????....
 
Mkuu usipende kubisha kwa sababu una hobby hiyo!
Usha wahi kusikia mpango wa msaada mkubwa kwa Ulaya toka Marekani baada ya WWII iitwayo Marshal Plan?
Usikimbilie mambo ya marekani kublack mail mataifa na vijimsaada uchwara ili yasiangukie Soviet union...hiyo haina uhusiano wowote na Tanzania kutokuwa na vipaumbele

Mlisema gesi itamaliza shida ya umeme tena mtauza mpaka DRC sasa kelele zile zimeishia wapi mpaka leo hii mseme SG ndio habari ya mujini???

Kingine unasema wazungu hivi wazungu vile..... Nachoshangaa mmesign mikataba mingi sana mkuu ambayo inawafanya muwe eligible kupata misaada flani sasa kwa kuwa nyie ni wakopaji miaka yote mmeshajifunga kwenye treaty za ajabu ajabu kuanzia za utawala bora mpaka mazingira sasa wakiisimamia kwanini mnaanza kelele??

Nilitegemea wwe kma mtu makini (i believe so) ungeweka hapa findings za UN kabla hujaconclude sio mnasema tu UN blah blah hku am sure taarifa kamili au ripoti hujaisoma mnalipeleka wapi taifa kila kitu kujifanya mnajua sana ilihali hao hao UN mnaowaponda ndio wanawafanya muwe eligible kupokea misaada ya mataifa makubwa na world bank!!!

Kama taifa tujikite kwenye mradi mmoja whether UN is right or wrong..... Gesi tumalizane nayo meanwhile tuinue kilimo na uvuvi etc uchumi ukuwe sio mkapa makaa ya mawe.. kikwete gesi.... Magu SG alafu awamu ya tano waseme SOLAR!!! Ndio nini hki sasa
 
Back
Top Bottom