UN kupinga mradi wa Steigler's Gorge ni uhujumu

UN kupinga mradi wa Steigler's Gorge ni uhujumu

Mkuu wakoloni both wajerumani na waingereza walifanya assessment na survey kubwa katika rufiji basin kwa nia ya kuindeleza, tena aim ilikuwa kwaajili ya agricultural irrigation, navigation na umeme. Tena zilifanyika mara nyingi nyingi in different years. Steiglers gorge came up multiple times as a good place ya kujenga dam kwaajili ya irrigation, umeme na fishing, ila waliachana nayo kutokana na environmental impact. Sisi wenyewe idea ya kujenga dam tumeiotoa kwao ila tunajidai vichwa ngumu hatutaki kuelewa impact yake kimazingira.
Naomba nijue hizo environmental impacts zilizozuia mradi huu kukubalika tangu enzi ya mjerumani, aliyeuza binadamau bila kujali social impacts.
 
Sikuwa najua kama chombo kama hiki kinaweza kuhujumu maendeleo ya nchi, sasa nimeamini,

Kumbe wanafurahia umaskini wetu
 
Tembelea Kinyerezi I ,150 MW kama uko Dar.
Kinyerezi II ,250MW iko under construction.
hahahahahaas wajinga wa CCM huwa mnanifurahisha sana hasa kwa.kupenda.kufurahia takwimu za.kwenye makaratasi na maneno ya majukwaani ya.waropokaji wenu huwa nawaona wapumbavu sana.nyie.watu unacho kiongea kuhusu kinyerezi sicho.kilichopo kinyerezi nimetoka huko tar 17 feb kwa kazi maalum hakuna haakuna hicho unavho kisema nyie watu ni wajinga sana aisee
 
Hahaha huwa mnawapiga risasi wanaowaambia ukweli mnasema eti ni vibaraka, muwapige risasi na hao UN sasa, au muwafukuze nchini.
 
Tusipende kutupia lawama kwa wengine pale tunaposhindwa kufanikisha mipango yetu.....nadhani kabla hatujaanza ujenzi wa hilo Bwawa, tuhoji kwanza matumizi ya Gesi.....zile ahadi kuwa kukatika kwa umeme kutakuwa historian kumeishia wapi?
Sipingi huo ujenzi, ninachotaka ni kuhakikishiwa matokeo ya Ujenzi, kule Mtwara watu walivunjwa Miguu, wengine kupoteza maisha kwa kisingizio cha wanazuia maendeleo.
Hakika.nakumbuka walivyo tulisha matango pori kuhusu gesi ya mtwara
 
Hapana hajapinga anashangaa tu serikali ilisema gesi ndio suluhu ghafla tena tunarudi kwenye umeme wa kutegemea maji!!!!

Yaani kwa kuwa umeme wa gesi tulishaanza kufua basi pesa hyo ya stiegler ielekezwe kwingine mfano kilimo au uvuvi n.k ili nchi isonge mbele maadam alternative ipo kuliko miradi miwili target moja wakati kuna watu wanategemea kilimo cha mvua bado na wapo karne ya 21.... Kwanni msiwekeze huko kila siku umeme umeme wakati gesi ipo
Mtu kama wewe ungekuwa ni mkutano wa kujiandikisha washiriki, nina hakika tusingekuwa chumba kimoja. Maelezo na maoni kama haya yanatakiwa yatolewe na mwanasiasa mwenye lengo la kudanganya wapiga kura. Mtendaji huwezi kutumia lugha ya kusema, mfano kilimo na uvuvi nk. ....

Ni kilimo gani kisichotegemea mvua ambacho hakihitaji umeme? Uvuvi gani wa maana usiotegemea umeme? Suala la umeme wa gesi haizuii kuwa na umeme wa maji. Duniani nani ana gesi kuliko Russia? Je umesikia wakiacha nuklia eti kwa sababu wana gesi? Afrika kusini walitumia nuklia kwa miaka mingi bila umeme wa maji je, kwa nini sasa hivi wamerudi kwenye maji?

Tutoe mawazo ya kiufahamu badala ya lugha ya wanaoomba kura.
 
Un hawataki tuwe na umeme wetu.Ttehe tehe tehe.
Mbona ulaya imetapakaa vinu vya nyukilia na viwanda vinavyotoa moshi unaoharibu mazingira hawasemi kitu
 
Sawa kabisa JPM ajenge Stieglers Gorge watake wasitake, jenga Udart Ubungo to Pugu na posta - mbagala au kongowe kabisa. Baada ya hapo atawale mpaka jina lake litakapoitwa.Mambo mengine yatajirekebisha yenyewe hatujaanza leo. Kwa hiyo Climate change inaathari zaidi kwa TZ kuliko wengine mbona Ethiopia wanajenga Bwawa kubwa Afrika nzima. Gesi waulizeni walioanza atapoteza muda sana ku deal na gesi mbele kwa mbele St.Gorge Ijengwe fasta.
 
Sikuwa najua kama chombo kama hiki kinaweza kuhujumu maendeleo ya nchi, sasa nimeamini,

Kumbe wanafurahia umaskini wetu
Mkuu kuna watu humu na hata wengine serikalini wanawahusudu wazungu na kuamini kila wanachopikiwa.
Huu ni mfano hai kuwa Watanzania tujiamini kwa maendeleo yetu.

Hapa Magufuli anatujengea heshima, na hao wazungu wataanza kuelewa kuwa hatuwezi kufuata vitu wanavyotaka wao visivyo na manufaa kwa nchi.
 
hahahahahaas wajinga wa CCM huwa mnanifurahisha sana hasa kwa.kupenda.kufurahia takwimu za.kwenye makaratasi na maneno ya majukwaani ya.waropokaji wenu huwa nawaona wapumbavu sana.nyie.watu unacho kiongea kuhusu kinyerezi sicho.kilichopo kinyerezi nimetoka huko tar 17 feb kwa kazi maalum hakuna haakuna hicho unavho kisema nyie watu ni wajinga sana aisee
Ulifika sehemu gani Kinyerezi.
Tuanzie hapo.
 
Inawezekana unajua umuhimu wa Stigler's Gorge Power Dam lakini hujui athari za mradi kimazingira na hasa Ecosystem na Climates...na isitoshe UN wameonya kwa faida.yetu si yao.....the vision of a hungry man is always short and temporary...
 
Msitake kujifanya mnaipinga UN kuhusu kugomea huo mradi, ukweli kuhusu ujenzi wa huo mradi ni kukosa hela. Laiti hela zingekuwepo leo hii huo mradi ungekuwa umeshaanza. Awamu iliyopita kelele ilikuwa ni uchumi wa gas, leo hii hakuna anayeongelea gas na tunataka kurukia mradi mwingine huku hakuna hata cent kumi. Pata majibu ya msingi kwanza kwanini sio gas bali ni stiegler gorge?
Tabia ya kuanzisha miradi na kuiacha hewani imekuwa ni mila na desturi kwa serikali hii ya CCM.Kilimo kwanza sijui kimepotekea wapi.Hawana kipaumbele kabisa.

Horace Kolimba:CCM haina dira,sera wala mwelekeo.
Kingunge:CCM imeishiwa punzi.

Roho zao zipumzike kwa amani.Amina
 
Kwa Magu wataula wa chuya! Prezdaa Magu songa mbele baba, kurudi nyuma, mwiko!
Kwa mazuri unayofanya tuko nyuma yako, yale mengine hapana!

Ujifunge na mkanda kwenye kulipa kodi maana unekulia mikopo kutoka Uzunguni.
 
View attachment 701335

Nimesoma katika gazeti la The Guardian on sunday, tar 25 Feb 2018, ati UN(Umoja wa Mataifa), wanapinga kujengwa kwa kituo cha kuzalisha umeme kiasi cha 2,100MW ati kwa sababu za mazingira.

Huu ni uhujumu, full stop!

UN inatumiwa tu, ili ujumbe uonekane ati unatoka chombo ambacho ni fair, lakini ujumbe huo ni lazima unatoka nchi zinazofaidika na matatizo yetu ya nishati.

Kampuni za kimarekani kama AGGREKO, DOWANS na nyingine nyingi ni wazi zisingependa kuona mradi huu wa Stieglers Gorge ukifanikiwa, maana watakosa ulaji wanaofaidika nao leo.

Kama ingewapendeza UN, basi Three Gorges Dam ya China, Aswan Dam ya Misri, Akosombo Dam ya Ghana vyote visingejengwa kwa sababu za kimazingira.

Nampongeza sana Rais Magufuli na kumpa moyo kushika moyo ule ule , ili nchi ijitawale kinishati.
ccm oyeeeeee cuf lipumba oyeeeeee
 
YOTE HAYA NI KWA SABABU RAISI WETU HAJAWAHI KUTEMBELEA NCHI ZA KIZUNGU.USHAMBA NI MZIGO ASEE ...YAANI KABLA HALIJAMALIZIKA MOJA LIMESHADANDIWA JINGINE NA MWISHO WA SIKU NI KUSUMBUANA KWENYE MAKODI.
 
Back
Top Bottom