UN kupinga mradi wa Steigler's Gorge ni uhujumu

Akiondoka magufuli atakuja mwingne atakuja wind energy wakati huo wa stieger umetelekezwa na hela imepgwa. Ifike mahali tusmamie jambo hadi likamilike. Gas ya mtwara mrad umekunywa mihela lakn bdo umeme tatzo
 
SG lazima tujenge hapa Dr. Magufuli namuunga mkono.

Kama UN wangemkemea na serikali yake kuacha kuharibu umoja wa kitaifa, kutumia nguvu, kuwaonea wapinzani hata kusababisha vifo vya watanzania wenzentu , kuacha watu wafanye maandamano kwa amani.
Hapo ningewaona watu wa maana na taasisi yenye akili ila kuzuia SG project wanajionesha walivyo vilaza hadi huko UN.

UN na USA wakafunge wanyama huko Washington DC au Pentagon ila sisi huku Tanzania SG lazima tujenge.

Kwa sasa, tunahitaji SG project kuliko tunavyohitaji wanyama ambao mafisadi tu ndiyo wanaofaidika kwa kuwaua na kukata pembe wakati wananchi hawana umeme.

To hell with UN but SG project must be realized for the betterment of lives of millions of Tanzanians.
 
Wewe ulitaka fact gani kwa mfano.
The pros and cons of 2,100megawatts, hilo halihitaji mjadala.
Project hii ipo inapingwa na UN toka enzi za Mwalimu.
Tukumbuke ni watu hawahawa walipinga hata ujenzi wa TAZARA miaka ya mwanzoni mwa 1970s.

Unfortunately, ingawa ni kweli TAZARA ulichangia kwa kiasi kikubwa ukombozi wa Kusini mwa Afrika lakini kibiashara ni unmitigated disaster. Wanachotuambia hawa wenzetu ni kuwa huu mradi unaweza kuwa kama ulivyo TAZARA hivi sasa.

Amandla........
 

Mkuu, duniani kuna watu wa ina nyingi ila aina hii ya WATU WALIOTAYARI KUVUNJA, KULIKO KUPINDISHA ni wachache mno na nadhani kwakua ndio viongozi wanaohitajika na nchi za ulimwengu huu wa tatu... Hewala Bwana, ni kauli ya kitwana.
 
Sidhani kama UN wamekurupuka kama wanapinga huu mradi wana evidence za kutosha kwa nini wanapinga huu mradi embu turudi nyuma mradi wa bomba la gesi Mtwara to Dar impact yake kwa Uchumi wa Tanzania inaonekana au ndio siasa kila kitu ndio
 


tindo,
Mkuu
Gas siyo renewable energy ila SG project ni long life project kwa hiyo bora tuiendeleze hiyo SG project.
Gas ilikuwa kisiasa zaidi na kifisadi mno mno.

Any way, ije mvua au jua ila Tanzania kwa sasa SG project ni ya muhimu sana kwa nchi hii hata hivyo imechelewa sana kutekelezwa.
 
umeme wa gesi una tatizo gani kwani kuendelezwa? inawezekana tunahitaji vyote viwili, hebu tungoje muda hutaamua, na pengine Magu ana plan zake, mkumbuke huyu jamaa anapenda vitu vya kuonekana usishangae anataka 5000mgw nchi nzima.
 
Inasiktisha sana...

UN ni vibaraka wa Marekani...

Mbona Ethiopia hajanyoshewa kidole kwenye ujenzi wake wa Dam ya umeme...

Wakati watatumia maji ya mto Nile na kusababisha upungufu wa 2% ya maji yanayozalishwa na huo mto, kusababisha nchi zinazotegemea huo mto kuathirika...


Cc: mahondaw
 
Mkuu wewe inaelekea ni kijana wa juzi juzi tu.
Miradi karibu yote ya Hydro imejengwa na Mwalimu.
Hata huu wa Stieglers Gorge ulikuwa kwenye drawing boards.

Mimi nimeingia ndani ya Kidatu na kuona zile 4 turbines zinazofua 200MW, cha mtoto.
Nimebahatika vile vile kuingia NDANI ya Nuclear Plant moja huko Ulaya, yenye ukubwa kama jengo la Yanga.
Hiyo Plant ilikuwa inatoa 900MW!
Sasa leo hao UN waambie wakusaidie ujenge plant kama hiyo hapa nchini , wataishia kukulisha studies kama unavyozionyesha za kwako hapa mtandaoni!

Tatizo kubwa watanzania mmeaminishwa na kulishwa maneno ambayo in principle ni defeatist, mwadhani maendeleo ni lelemama na yatakuja kwa feasibility studies.

Mrusi Yuri Gagarin, binadamu wa kwanza anga za juu, alifanyiwa feasibility study ipi kufanikiwa!
Na je ile Apollo mission iliyilipuka na kuua wanaanga karibu nane wa kimarekani, yenyewe haikufanyiwa any studies?

Maendeleo ni multifaceted.
Gesi tutaitumia, makaa ya mawe yatatumika.
Wengi wenu muishio Dar wala hamjui na hamjafika maeneo ya nishati hizo, zinatumika hata leo.

Tukitegemea maendeleo yetu yatakuja kwa kumfurahisha mzungu aliyekutawala, wengine hata kiakili, maendeleo yatachelewa sana.
 
Kinacho tukwamisha Afrika ni Ujinga , Ubinafsi na tutabakia kuchonga Domo sana maendeleo zero
 
Spot on mkuu!
 
Magu asilegeze kamba, ashikilie apo apo. Go Magu go. Ili tupate freedom ya nishat na hatimae ya uchumi.
Hahahaha wabongo bhana kwahyo wanaokuhujumu ndio hao hao mikopo yao mnawaomba kila siku..... Wanawajengea reli na bomba alafu wakishauri eti wahujumu ssa kma hawawatakii mema si wangewanyima mikopo

Wabongo bhana
 
Kwa Magu wataula wa chuya! Prezdaa Magu songa mbele baba, kurudi nyuma, mwiko!
Kwa mazuri unayofanya tuko nyuma yako, yale mengine hapana!
 

mkuu hakuna project ambayo mkoloni aliitekeleza bila kuna na faida kwake kiuchumi, as hakua na lengo la kuiendeleza nchi kiviwanda, large projects za umeme hazikua na maana kwake. Na si kisingizio cha mazingira. Maana wangekua wanajali mazingira wasingetoboa ozone layer, hadi leo wasingeumiza watu na viumbe Niger delta.
 
Wakubwa hawa wanaotoboa ozone na kuharibu mazingira leo hii wanadai stigler's inaharibu mazingira. Sbb kubwa hawataki 'independency ya energy sector' Africa, sbb wanajua economically itawaathiri wao.
 

Mkuu Poise sipingi maoni yako na ninayaheshimu sana na sipingi mradi wa maji ila tuwekane sawa kwanza ili tusiburuzwe. Umesema mradi wa Gas sio renewable, lakini tuliambiwa kwa mujibu wa matumizi yetu tungetumia nishati ya gas kwa 100yrs ukikamilika. Unasema gas ilikuwa kisiasa zaidi, lakini ambacho hujaangalia na kujiuliza hata mradi huu wa stiegler gorge unaletwa na mwanasiasa, tena aliyekuwa kwenye kundi lilikotuaminisha gas ndio mkombozi wetu, huku akirusha vijembe kwamba wapinzani wanataka kukwamisha maendeleo kwa kupinga jinsi mradi utakavyotekelezwa.

Mkuu mpaka sasa tuna miradi ya umeme ya maji na tatizo limekuwa ni upungufu wa maji kutokana na mabadiliko ya tabia nchi. Hii ndio iliyokuwa sababu kubwa ya kuhamia kwenye gas. Wakati huo huyu anayetaka kutekeleza mradi wa stiegler gorge kwa 3tr alikuwa anashangilia mradi wa gas bila kupinga waziwazi na kupendekeza huu wa maji. Kumbuka alikuwa waziri na mbunge, kumaanisha mradi wa gas ulipata baraka zake zote. Leo ni kipi kinakufanya umuamini kwa haya anayosema, huku akiwa hana hata shilingi mkononi ya huo mradi. Mkuu Poise haya ndio majukwaa ya kuhoji kwa kina, huenda mchango wako unaangaliwa na wafanya maamuzi, unapoingia kichwakichwa bila kuhoji kwa kina unaruhusu maamuzi mabovu kufanyika. Kuwa makini ndugu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…