MY TAKE; Hii ndiyo misingi imara iliyojengwa na baba wa Taifa pendwa Mwl; Julius Nyerere.
Urusi, China, Cuba, na Tanzania zimekua pamoja katika kipindi chote kigumu enzi za ukoloni, nchi nyingi za Magharibi zilitukimbia na hata kutuwekea vikwazo vya biashara kwasababu ya mahusiano yetu na mataifa haya ya kijamaa, Hawa ndio hawakututupa wakati wote huo, haifai kukurupuka na kuwaacha katika kipindi hiki kigumu kwao, Hongera Sana Tanzani kwa kutopiga kura.
Inawezekana katika wakati flani katika historia hawa ndio walikuwa marafiki wazuri wa Tanzania. Jambo ambalo ni lazima tulikubali ni kuwa nchi za kijamaa hazina historia nzuri wala uzingatiaji wa haki za binadamu. Ukiangalia mfumo wa uongozi wa Urusi, China , Cuba na nchi nyingine za kijamaa,ni wazi hauvutii kwa watu wengi walio wastaarabu.
Urusi kwa Tanzania amekuwa akitoa baadhi ya nafasi za elimu lakini hana mchango mwingine nje ya hapo, tena hata wanafunzi wakimaliza zaidi ya nusu huwa vichaa. Kuna watu wanasema Urusi hakuwahi kuitawala Afrika, ni sawa kabisa, ila madili ya Urusi ni kwenye kuuza silaha. Hata kwenye ile vita na Uganda, baada ya vita kuwa ngumu Mwl aliwatafuta kwa ajili ya kupata silaha, walidai malipo cash, na zaidi ilionekana walifanya double dealing, waliuza ndege za vita Uganda, Tz akauziwa makombora ya kuziangusha.
Kwa upande wa China, huyu hana rafiki wa kudumu, yuko tayari hata kuuwa watu ili apate anachokihitaji. Siku za karibuni naamini kila mmoja ameona tabia za mikopo ya China, ukikaa vibaya wanabeba nchi. Kwa Tanzania, wakati wa Ujenzi wa reli ya kati, wachina walivyofika maeneo ya Morogoro walianza kuchimba madini na kusafirishwa kimagendo kwenda China, kilichoharibu hili dili ni siku gunia lilianguka airport likiwa na madini.
Kwa Tanzania, Marekani amekuwa akisaidia vitu vingi, madawa, neti, ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali, maji, elimu, budget etc. Ni kweli kuna nchi ambazo US amefanya uonevu wa dhahiri, na ndio maana hata hapa JF wanampinga kutokana na aliyoyofanya kwenye nchi hizo, ukweli ni kuwa US na Umoja wa Ulaya wana usaidizi mkubwa kwa Tz kuliko hizo nchi za kijamaa.