Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Kuna watu wanaohoji uhalali wa tafsiri ya Biblia ya King James Version (KJV). Wengine wanasema ni ya zamani, haieleweki kwa kizazi cha sasa, au kwamba kuna tafsiri mpya zilizo sahihi zaidi. Lakini je, kweli tafsiri mpya ni bora zaidi, au tuko kwenye harakati za kupunguza uzito wa Neno la Mungu?
1. Mungu amelinda Neno lake kupitia KJV
Imeandikwa: “Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe” (Mathayo 24:35). Tafsiri ya KJV ilifanyika kwa maombi, kwa heshima kuu kwa Mungu, na kwa ushirikiano wa wasomi wa Kiebrania, Kigiriki, na Kilatini waliomcha Mungu.
Walikusanyika si kwa ajili ya faida ya kifedha au umaarufu, bali kwa dhamira ya kutengeneza tafsiri isiyochafua Neno la Mungu, bila kupendelea dhehebu lolote.
2. KJV ni Tafsiri ambayo imetumika kuwaleta watu wengi kwa Kristo
Kwa karne nyingi, mahubiri mazito yaliyoleta toba na wokovu yametolewa kwa kutumia KJV. Biblia hii ndiyo iliyokuwa kifaa mikononi mwa Wachungaji wa kipindi cha Awakenings, yaani vipindi vya uamsho vilivyotikisa dunia.
Je, tuitupilie mbali Biblia ambayo Mungu ameibariki kwa muda mrefu kwa sababu tu ya lugha yake ya heshima na kiwango cha juu? Nope.
3. Lugha ya KJV ni Takatifu na ya kipekee
Kuna watu wanaodai kwamba “maneno kama thou, thee, na shalt ni magumu.” Lakini hiyo sio sababu ya kuitupilia mbali tafsiri hiyo ya Biblia. Lugha hiyo ya kifalme si ya kawaida kwa makusudi—inaweka uzito wa kiroho kwa yale tunayoyasoma. Tunapaswa kukumbuka kuwa Neno la Mungu si maandishi ya kawaida, ni takatifu na lina mamlaka.
4. KJV imelinda Maandiko yaliyokubaliwa na Kanisa kwa karne nyingi
Kuna wanaoipinga KJV kwa kusema ilitumia Textus Receptus badala ya Alexandrian Manuscripts. Lakini manuscripts ya Kigiriki iliyotumiwa katika KJV ndiyo iliyokubaliwa kwa karne nyingi na Wakristo waliotangulia, kabla ya kupatikana kwa maandiko yenye mashaka na mabadiliko yasiyothibitishwa katika karne ya 20.
5. Tafsiri nyingi mpya zimelegeza ukweli wa Maandiko
Tafsiri nyingi za kisasa zimeondoa aya nzima, kupunguza uzito wa mafundisho ya wokovu, na kupotosha baadhi ya mafundisho ya msingi kama vile Utatu, Yesu Kristo kufanyika mwili, na hata umuhimu wa Damu ya Yesu.
KJV imehifadhi mamlaka, heshima, na nguvu ya Neno la Mungu kama lilivyo.
Ya kale ni dhahabu. Tushike ya kale na yaliyo thabiti
“BWANA asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, Iko wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu...” (Yeremia 6:16)
"Asante Mungu kwa kuilinda tafsiri hii ya Biblia(KJV). Tusaidie, ee Baba kuendelea kuitumia kwa ajili ya kufundisha, kuonya, na kuwaongoza watu katika wokovu. Tusaidie pia kuzing'amua biblia za kishetani na mafundisho ya mashetani. Katika Jina la Yesu. Amen"
www.jamiiforums.com

Je, unaijua "Biblia" ya Shetani? Pita hapa nikujuze!
Katika siku hizi za mwisho, wapinga Kristo wameanza kutumia njia mbalimbali kuwapotosha waumini wa kweli. Mojawapo ya njia hizo ni kuzalisha Biblia potofu au tafsiri potofu za Biblia. Kama huna habari kuna kitabu kinaitwa "The Satanic Bible" (Biblia ya Shetani), kilichoandikwa na Anton LaVey...