Una habari? Wanasayansi "wameiona" Safina ya Nuhu wa Biblia

Ukiona watu wote wanaokataa ni wafiraj ili kuhalalisha mambo
 
Wewe usha wehuka wewe, unaamini vitu vya kijinga sana, halafu unaleta huku, huku watu wanatuia akili zaidi kuliko imani.
 
Mbona hujaweka Picha wakati habari hii Ina Picha za kutosha na mpaka Video za huko YouTube!!?
 
How did Noah summon penguins from Antarctica.??
Swali zuri Aneel munawar, inaonyesha wewe ni great thinker kwelikweli.
But if we believe God created the world, the seas, the continents, and even the penguins themselves, then it’s not hard to believe He could guide any animal to wherever He wanted. The real inconsistency is when someone believes in an all-powerful God but thinks He can’t relocate birds!
cc: The Coin Man
 
Na ile tuliyokuta mabaki yake yakiwa na mifupa mikavu kwenye ziwa Eyasi! Nayo itambulike.
 
Bibilia ni kitabu cha historia, kuna hqbari za kweli, kuna habari za kutunga hivyo ugunduzi wao unaweza kuwa kweli ila kwwnye bibilia tunasoma safina ilitulia juu ya kilima gani vile na kipo nchi gani hicho kilima kasome vizuri kama hakipo ugiriki tafiti zao za uwongo
 
Katika historia ya mwanadamu, dini imekuwa mojawapo ya taasisi zenye ushawishi mkubwa duniani. Imeongoza mataifa, imetuliza nafsi, imeeneza maadili, lakini pia — kwa mtazamo wa wachache wanaojitambua na wanaojiuliza maswali ya msingi — dini ni mfumo wa kihadaa uliobuniwa ili kuwatumikisha wengi kwa maslahi ya wachache. Makala hii inalenga kuonesha kwa nini dini, katika muktadha wa kifalsafa na kijamii, inaweza kutazamwa kama utapeli mkubwa wa kihistoria.

1. Dini kama Njia ya Kuwanyonya Watu Maskini

Dini nyingi zinahimiza wafuasi wao kutoa zaka, sadaka, na michango mbalimbali — mara nyingi bila ufuatiliaji wa matumizi. Katika hali ya kiuhalisia, michango hii huwanufaisha viongozi wa dini kwa maisha ya kifahari huku waumini wakiendelea kuteseka. Kwa mfano, makanisa na misikiti mingi hujengwa kwa gharama kubwa, huku waumini wake wakishindwa hata kumudu milo mitatu kwa siku. Hili ni tapeli la wazi, kwani uhalali wa kutoa unatokana na hofu ya laana au tamaa ya baraka zisizothibitishwa.

2. Dini Inatumiwa Kama Chombo cha Hofu na Udhibiti

Misingi ya dini nyingi inajengwa juu ya wazo la "mbingu" kwa watii na "moto wa milele" kwa wasiotii. Huu ni mfumo wa kutengeneza hofu ya kufikirika ili watu wasiulize maswali wala kuasi. Mtu anayeuliza, kwa mfano, "Mbona Mungu anakaa kimya wakati wa mateso ya watu?" huambiwa ana imani haba au anaruhusu ibilisi amtawale. Hii ni njia ya kuzima fikra huru kwa kutumia hofu ya kisiri. Hofu hii hutumika kuzuia watu kujitambua na kufikiri kwa uhuru — hali inayodumaza maendeleo ya kijamii na kisayansi.

3. Dini Inaharibu Utamaduni wa Mwafrika

Kabla ya ujio wa dini za Kigeni kama Ukristo na Uislamu, Waafrika walikuwa na imani zao za jadi, zenye misingi ya kuheshimu mazingira, kushirikiana kijamii, na kuenzi mizizi ya ukoo. Ujio wa dini ulibeba ajenda ya kubadilisha utambulisho wa Mwafrika, kumfanya ajione mdhambi tangu kuzaliwa, na kumlazimisha aone lugha na mila zake kuwa za kishenzi. Hili ni utapeli wa kiutamaduni kwa kivuli cha wokovu wa kiroho.

4. Ahadi za Uongo zisizoweza Kuthibitishwa

Dini nyingi huahidi pepo lenye mito ya asali, wake warembo, au maisha ya amani kwa wale watakaofuata maagizo ya kiimani. Lakini hakuna aliyeenda huko akarudi kututhibitishia. Hakuna ushahidi wa kisayansi wa kuwepo kwa maisha baada ya kifo. Ni kama mtu kukutapeli akisema, "Nipe hela zako leo, nitakupa urithi mkubwa kesho katika ulimwengu mwingine." Hii ni skimu ya utapeli wa kihisia, inayocheza na tamaa na hofu za binadamu.

5. Viongozi wa Dini ni Watu Kama Wengine — Lakini Hujitwika Umungu

Wachungaji, masheikh, mapadre na manabii hujigeuza miungu wa ardhi. Wanajilimbikizia mali, magari ya kifahari, na hata heshima kupita wanasayansi au walimu. Wengi wao hawana elimu ya msingi lakini wanaongoza maelfu kupitia maneno ya kutia hofu au tamaa ya miujiza. Huu ni utapeli unaotumia ujinga na shida za watu kama mtaji wa biashara.
 
Asante kwa makala hiyo uliyoi-copy chatGPT!
Ni makala inayoonyesha upande mmoja tu wa shilingi. Iambie ikupe na hoja za upande wa pili zinazoonyesha faida za dini.
 
Acha kukimbia tongozo nime tumwa na bwana wa majeshi
 
Hakuna great thinker anaeweza kuamini mythology ni uhalisia ni wehu wachache tu
Hivi hujiulizi kwanini dini zilitangulizwa afu utumwa ukafuata
Kuanzia Leo tumia hata dakika kumi tu Fanya meditation utafungua jicho la kiroho mambo ya kiroho yanahitaji subconscious siyo hiyo consciousness wanayotumia masomi uchwara na ma scientist ufala, corrupted mind
 
We endelea kuleta huyo upupu wako nasi wenye utimamu tutakupopoa mpaka ushike adabu na utaelewa tu, japo ni ngumu kuikana nafsi uliyovalishwa ila ukiendelea kutuchokoza tutakupopoa tu
 
Story za sungura na fisi hata sisi tulisimuliwa na zilitufunza maadili Katika jamii, sio huo upupu
 
hivi hujawahi kujiuliza kama kuna watu au kikundi cha watu ndio wanaamua nini kifanyike duniani?
eniwei, hiyo sehemu ya milima ilikua maarufu miaka zaidi ya 10 huko, na huenda ata ilitengenezwa ili tuamini wanachota wao...........
 
Tatizo nilipogundua ww ni chawa wa CCM nikajua tu huna ulokole wwte
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…