Una habari? Wanasayansi "wameiona" Safina ya Nuhu wa Biblia

Safina ya Nuhu ni moja kati ya habari maarufu zilizoandikwa kwenye Biblia na zinazochunguzwa sana na wanasayansi. Sasa baada ya karne nyingi za mijadala, kejeli, na mashaka, matokeo mapya ya kisayansi yameanza kugeuza mtazamo wa ulimwengu kuhusu Safina ya Nuhu.

Katika milima mirefu mashariki mwa Uturuki, kuna kundi la watafiti linaloongozwa na mtafiti mahiri Andrew Jones, kupitia mradi wa Noah’s Ark Scans. Walichokifichua kinastaajabisha na ni pigo kwa wale wanaodai kuwa Biblia ni mkusanyiko tu wa hadithi za kutungwa na watu.

Hivi majuzi watafiti hao wamegundua umbo la meli katika milima hiyo. Habari ya ugunduzi wa Safina ilianza kusikika mnamo mwaka 1959, wakati kapteni wa jeshi la Uturuki, Ilhan Durupınar, alipoona kitu cha ajabu chenye umbo la meli kikiwa kimezama ardhini. Kitu hicho kina urefu wa mikono ya kifalme ya Wamisri 300—sawa kabisa na vipimo vilivyoandikwa katika Mwanzo 6:15.

Licha ya habari hiyo kuwavutia watu wengi mwanzoni, utafiti wa eneo hilo ulisahaulika kwa muda mrefu. Lakini sasa umerudi katika vichwa vya habari tena kutokana na teknolojia mpya na utafiti wa kisayansi wa kisasa unaounga mkono habari hiyo ya Biblia.

Jones na timu yake wanatumia vifaa vya radar inayochunguza ardhini (GPR) na tomografia ya umeme (ERT) ili kuangalia vilivyopo chini ya ardhi bila kuchimba. Matokeo yao yameonyesha mambo yafuatayo: miundo ya ndani yenye pembe, ambayo ni kawaida kwa vyombo vya majini, shimo kuu la kati linalopita katika eneo lote, likiwa na eneo tupu katikati. Na sampuli za udongo kutoka ndani ya eneo hilo zinaonyesha rangi na muundo tofauti, dalili ya uwepo wa kitu kisicho cha asili.

“Matokeo haya yamethibitishwa na wataalamu wa jiolojia wasiohusiana kabisa na dini,” amesema Jones. “Tunawapa takwimu zetu bila kuchujwa, na wao wenyewe wanathibitisha kwamba kuna kitu cha kipekee chini ya ardhi.”

Ugunduzi huu ni uthibitisho wa wazi kuwa habari zilizoandikwa kwenye Biblia ni za kweli. Kwa vizazi vingi, wapinzani wa imani ya Kikristo wamekuwa wakidai kuwa Biblia ni ya kubuni. Lakini sasa katika milima hiyo kuna eneo lenye vipimo sawa na vile vya maandiko. Safina ipo katika eneo sahihi la kijiografia na inaonyesha sifa za ndani zinazolingana na meli hiyo ya kale.

Huu sio ugunduzi wa kawaida. Ni changamoto kwa dunia ya kisasa. Biblia, kitabu kilichodharauliwa na wengi, sasa kinaanza kuthibitishwa na sayansi ya kisasa. Atheists mpooo?
Iko hivi biblia ni mjumuisho wa vitabu mbali mbali ambavyo vimeandikwa na waandishi mbali mbali na wengine hawajulikani

Ila kuna mabaki machache ya maneno ya Mwenyezi Mungu ambayo ni ya kweli,the rest ni maneno ya wanadamu wamebadilisha na kuweka yao,kwa maana nyingine wamekichezea hicho kitabu
 
Tatizo nilipogundua ww ni chawa wa CCM nikajua tu huna ulokole wwte
Hahaa, ulokole haupimwi kwa njia hiyo. Soma uzi huu ujue nini maana ya ulokole
 
Ila kuna mabaki machache ya maneno ya Mwenyezi Mungu ambayo ni ya kweli,the rest ni maneno ya wanadamu wamebadilisha na kuweka yao,kwa maana nyingine wamekichezea hicho kitabu
Yataje mabaki hayo
 
Yataje mabaki hayo
Ukitaka kuyajua ni yale ambayo yanamtambua Yesu kama mtumishi wa Mungu au Mtume wa Mungu

Kama ambavyo amejieleza mara nyingi yeye mwenyewe,kwamba ametumwa

Ameeleza juu ya kuwepo Mungu mmoja,na ndio ujumbe wa mitume wote toka zama na zama

Za kuandikwa na wanadamu ni rahisi kuzijua kama Paulo alivyotoa maelezo yake,mara aliona mwanga ndio akasikia sauti mara alisikia sauti tu ya bwana ikimwiita,na msingi wa ukristo mkubwa umetoka kwa huyu bwana Sauli / Paulo

Ukija kwenye hizi habar za sijui nafsi tatu tatu,mara baba,mwana,roho mtakatifu

Mara sijui Yesu ni Mungu na baba na roho kwa wakati mmoja

Mara Mungu akakubali kuzaliwa ili aje asulubiwe na watu wake,,daah ngoja niishie hapa
 
Safina ya Nuhu ni moja kati ya habari maarufu zilizoandikwa kwenye Biblia na zinazochunguzwa sana na wanasayansi. Sasa baada ya karne nyingi za mijadala, kejeli, na mashaka, matokeo mapya ya kisayansi yameanza kugeuza mtazamo wa ulimwengu kuhusu Safina ya Nuhu.

Katika milima mirefu mashariki mwa Uturuki, kuna kundi la watafiti linaloongozwa na mtafiti mahiri Andrew Jones, kupitia mradi wa Noah’s Ark Scans. Walichokifichua kinastaajabisha na ni pigo kwa wale wanaodai kuwa Biblia ni mkusanyiko tu wa hadithi za kutungwa na watu.

Hivi majuzi watafiti hao wamegundua umbo la meli katika milima hiyo. Habari ya ugunduzi wa Safina ilianza kusikika mnamo mwaka 1959, wakati kapteni wa jeshi la Uturuki, Ilhan Durupınar, alipoona kitu cha ajabu chenye umbo la meli kikiwa kimezama ardhini. Kitu hicho kina urefu wa mikono ya kifalme ya Wamisri 300—sawa kabisa na vipimo vilivyoandikwa katika Mwanzo 6:15.

Licha ya habari hiyo kuwavutia watu wengi mwanzoni, utafiti wa eneo hilo ulisahaulika kwa muda mrefu. Lakini sasa umerudi katika vichwa vya habari tena kutokana na teknolojia mpya na utafiti wa kisayansi wa kisasa unaounga mkono habari hiyo ya Biblia.

Jones na timu yake wanatumia vifaa vya radar inayochunguza ardhini (GPR) na tomografia ya umeme (ERT) ili kuangalia vilivyopo chini ya ardhi bila kuchimba. Matokeo yao yameonyesha mambo yafuatayo: miundo ya ndani yenye pembe, ambayo ni kawaida kwa vyombo vya majini, shimo kuu la kati linalopita katika eneo lote, likiwa na eneo tupu katikati. Na sampuli za udongo kutoka ndani ya eneo hilo zinaonyesha rangi na muundo tofauti, dalili ya uwepo wa kitu kisicho cha asili.

“Matokeo haya yamethibitishwa na wataalamu wa jiolojia wasiohusiana kabisa na dini,” amesema Jones. “Tunawapa takwimu zetu bila kuchujwa, na wao wenyewe wanathibitisha kwamba kuna kitu cha kipekee chini ya ardhi.”

Ugunduzi huu ni uthibitisho wa wazi kuwa habari zilizoandikwa kwenye Biblia ni za kweli. Kwa vizazi vingi, wapinzani wa imani ya Kikristo wamekuwa wakidai kuwa Biblia ni ya kubuni. Lakini sasa katika milima hiyo kuna eneo lenye vipimo sawa na vile vya maandiko. Safina ipo katika eneo sahihi la kijiografia na inaonyesha sifa za ndani zinazolingana na meli hiyo ya kale.

Huu sio ugunduzi wa kawaida. Ni changamoto kwa dunia ya kisasa. Biblia, kitabu kilichodharauliwa na wengi, sasa kinaanza kuthibitishwa na sayansi ya kisasa. Atheists mpooo?

Mimi ninachojua ni kuwa, habari za Noah/Nuh zipo kwenye Biblia na Quran hivyo waamini wanauelewa tayari wa hilo tukio zima na wala hawahitaji ushahidi wa ziada wa video ambazo zaweza kuwa niza kutengeneza.
Kwa sasa hivi dunia ipo kwenye "AI" hivyo usiamini kila kitu na hata kama ukiona mtu anaongea. Sikiliza kwanza kama anacho ongea kina maana....watu wanawekewa maneno kwa technologia ya "AI"uone wanaongea kabisa kumbe sio wao....
 
Pale kijana wa 2000 anapoamua kuleta hoja baada ya kufanya research ndefu sana ilomchukua takriban dakika 8 ... napata shaka na utimamu wako mleta mada
 
Safina ya Nuhu ni moja kati ya habari maarufu zilizoandikwa kwenye Biblia na zinazochunguzwa sana na wanasayansi. Sasa baada ya karne nyingi za mijadala, kejeli, na mashaka, matokeo mapya ya kisayansi yameanza kugeuza mtazamo wa ulimwengu kuhusu Safina ya Nuhu.

Katika milima mirefu mashariki mwa Uturuki, kuna kundi la watafiti linaloongozwa na mtafiti mahiri Andrew Jones, kupitia mradi wa Noah’s Ark Scans. Walichokifichua kinastaajabisha na ni pigo kwa wale wanaodai kuwa Biblia ni mkusanyiko tu wa hadithi za kutungwa na watu.

Hivi majuzi watafiti hao wamegundua umbo la meli katika milima hiyo. Habari ya ugunduzi wa Safina ilianza kusikika mnamo mwaka 1959, wakati kapteni wa jeshi la Uturuki, Ilhan Durupınar, alipoona kitu cha ajabu chenye umbo la meli kikiwa kimezama ardhini. Kitu hicho kina urefu wa mikono ya kifalme ya Wamisri 300—sawa kabisa na vipimo vilivyoandikwa katika Mwanzo 6:15.

Licha ya habari hiyo kuwavutia watu wengi mwanzoni, utafiti wa eneo hilo ulisahaulika kwa muda mrefu. Lakini sasa umerudi katika vichwa vya habari tena kutokana na teknolojia mpya na utafiti wa kisayansi wa kisasa unaounga mkono habari hiyo ya Biblia.

Jones na timu yake wanatumia vifaa vya radar inayochunguza ardhini (GPR) na tomografia ya umeme (ERT) ili kuangalia vilivyopo chini ya ardhi bila kuchimba. Matokeo yao yameonyesha mambo yafuatayo: miundo ya ndani yenye pembe, ambayo ni kawaida kwa vyombo vya majini, shimo kuu la kati linalopita katika eneo lote, likiwa na eneo tupu katikati. Na sampuli za udongo kutoka ndani ya eneo hilo zinaonyesha rangi na muundo tofauti, dalili ya uwepo wa kitu kisicho cha asili.

“Matokeo haya yamethibitishwa na wataalamu wa jiolojia wasiohusiana kabisa na dini,” amesema Jones. “Tunawapa takwimu zetu bila kuchujwa, na wao wenyewe wanathibitisha kwamba kuna kitu cha kipekee chini ya ardhi.”

Ugunduzi huu ni uthibitisho wa wazi kuwa habari zilizoandikwa kwenye Biblia ni za kweli. Kwa vizazi vingi, wapinzani wa imani ya Kikristo wamekuwa wakidai kuwa Biblia ni ya kubuni. Lakini sasa katika milima hiyo kuna eneo lenye vipimo sawa na vile vya maandiko. Safina ipo katika eneo sahihi la kijiografia na inaonyesha sifa za ndani zinazolingana na meli hiyo ya kale.

Huu sio ugunduzi wa kawaida. Ni changamoto kwa dunia ya kisasa. Biblia, kitabu kilichodharauliwa na wengi, sasa kinaanza kuthibitishwa na sayansi ya kisasa. Atheists mpooo?
So what???!!!
Inatusaidia vipi sisi ambao tunahitaji ukombozi wa kiuchumi na kuondokana na dhana ya utegemezi wa mikopo na ruzuku kutoka mataifa ya kigeni?
 
Mleta mada una matatizo ya akili.
Mlikuwa mnasema Biblia ni kitabu cha kutungwa. Sasa Geologists (wasio na dini) wamewawekea ushahidi huo kwa kutumia zana za kisasa. Siku ya mwisho hamtakuwa na la kujitetea
 
So what???!!!
Inatusaidia vipi sisi ambao tunahitaji ukombozi wa kiuchumi na kuondokana na dhana ya utegemezi wa mikopo na ruzuku kutoka mataifa ya kigeni?
Kwan wao wameanza kufanya tafiti ili wawapeni mikopo..? Pambaneni na majizi yenu. Tuna jiibia wemyewe tunakataa akili nyimgi na kulazimisha akili finyu zitawale
 
Safina ya Nuhu ni moja kati ya habari maarufu zilizoandikwa kwenye Biblia na zinazochunguzwa sana na wanasayansi. Sasa baada ya karne nyingi za mijadala, kejeli, na mashaka, matokeo mapya ya kisayansi yameanza kugeuza mtazamo wa ulimwengu kuhusu Safina ya Nuhu.

Katika milima mirefu mashariki mwa Uturuki, kuna kundi la watafiti linaloongozwa na mtafiti mahiri Andrew Jones, kupitia mradi wa Noah’s Ark Scans. Walichokifichua kinastaajabisha na ni pigo kwa wale wanaodai kuwa Biblia ni mkusanyiko tu wa hadithi za kutungwa na watu.

Hivi majuzi watafiti hao wamegundua umbo la meli katika milima hiyo. Habari ya ugunduzi wa Safina ilianza kusikika mnamo mwaka 1959, wakati kapteni wa jeshi la Uturuki, Ilhan Durupınar, alipoona kitu cha ajabu chenye umbo la meli kikiwa kimezama ardhini. Kitu hicho kina urefu wa mikono ya kifalme ya Wamisri 300—sawa kabisa na vipimo vilivyoandikwa katika Mwanzo 6:15.

Licha ya habari hiyo kuwavutia watu wengi mwanzoni, utafiti wa eneo hilo ulisahaulika kwa muda mrefu. Lakini sasa umerudi katika vichwa vya habari tena kutokana na teknolojia mpya na utafiti wa kisayansi wa kisasa unaounga mkono habari hiyo ya Biblia.

Jones na timu yake wanatumia vifaa vya radar inayochunguza ardhini (GPR) na tomografia ya umeme (ERT) ili kuangalia vilivyopo chini ya ardhi bila kuchimba. Matokeo yao yameonyesha mambo yafuatayo: miundo ya ndani yenye pembe, ambayo ni kawaida kwa vyombo vya majini, shimo kuu la kati linalopita katika eneo lote, likiwa na eneo tupu katikati. Na sampuli za udongo kutoka ndani ya eneo hilo zinaonyesha rangi na muundo tofauti, dalili ya uwepo wa kitu kisicho cha asili.

“Matokeo haya yamethibitishwa na wataalamu wa jiolojia wasiohusiana kabisa na dini,” amesema Jones. “Tunawapa takwimu zetu bila kuchujwa, na wao wenyewe wanathibitisha kwamba kuna kitu cha kipekee chini ya ardhi.”

Ugunduzi huu ni uthibitisho wa wazi kuwa habari zilizoandikwa kwenye Biblia ni za kweli. Kwa vizazi vingi, wapinzani wa imani ya Kikristo wamekuwa wakidai kuwa Biblia ni ya kubuni. Lakini sasa katika milima hiyo kuna eneo lenye vipimo sawa na vile vya maandiko. Safina ipo katika eneo sahihi la kijiografia na inaonyesha sifa za ndani zinazolingana na meli hiyo ya kale.

Huu sio ugunduzi wa kawaida. Ni changamoto kwa dunia ya kisasa. Biblia, kitabu kilichodharauliwa na wengi, sasa kinaanza kuthibitishwa na sayansi ya kisasa. Atheists mpooo?
Hawa dawa yao nikuwapiga injili wala usicheke nao kwa sayansi.
 
So what???!!!
Inatusaidia vipi sisi ambao tunahitaji ukombozi wa kiuchumi na kuondokana na dhana ya utegemezi wa mikopo na ruzuku kutoka mataifa ya kigeni?
ministrant
You ask, ‘So what?’ OK sir, and that simple question opens the door to something much deeper...

Usipozama deep, habari ya kuonekana kwa safina ya Nuhu unaweza kufikiri inawahusu walokole tu. Ngoja "nikuchanue!" Habari hiyo inatufundisha mambo ya msingi sana yanayoweza hata kutusaidia kiuchumi:

Kwanza, inatufundisha kuhusu utii na maandalizi. Nuhu alitii maagizo ya Mungu na akafanya maandalizi ya jambo ambalo wengine waliona ni upuuzi. Kiuchumi, hiyo inatufundisha umuhimu wa kuwa na maono ya mbali. Taifa lolote lisipojifunza kutii kanuni za kiuchumi na kufanya maandalizi ya dhati, litabaki tegemezi.

Pili, inatufundisha kutokukata tamaa hata tukionekana wendawazimu. Nuhu alidhihakiwa kwa miaka mingi, lakini hakukata tamaa. Sisi pia, Afrika, hatupaswi kukata tamaa mbele ya changamoto za utegemezi wa nje. Tuanze na mambo madogo: uzalishaji wa ndani, nidhamu ya matumizi, na uwajibikaji, bila kujali wanaotubeza.

Tatu, habari hiyo inatufundisha ukweli wa kihistoria. Inajenga imani na uthubutu. Ukiwa na imani kwamba Biblia sio hadithi bali kitabu chenye habari na historia halisi, unapata nguvu ya kuamini hata ahadi za Mungu kuhusu kuinuliwa na kufanikiwa (Kumbukumbu 28:1-13). Hii imani inachochea pia uthubutu wa kiuchumi.

Kwa hiyo, ndugu yangu ministrant, habari hiyo ni sehemu ya ukombozi wetu: kiroho, kiakili na hata kiuchumi. Ukombozi huanza na kufunguka kwa akili!

Curious to hear your take!!
 
Habari zako unatoaga wapi mkuu, anyway very interested
 
Back
Top Bottom