Una habari? Wanasayansi "wameiona" Safina ya Nuhu wa Biblia

Una habari? Wanasayansi "wameiona" Safina ya Nuhu wa Biblia

Nikimwona nitamkataza kuwa mlokole.

Atakuwa kobaz wa kike kama Faiza foksi.
Jesus is coming soon jamani. Hizi habari za Nuhu ni njia ya kutuamsha tuache kuipuuza Biblia. Yaliyoandikwa ni ya kweli. Ukweli mmojawapo ni huo wa Safina ya Nuhu. Gharika ilikuwepo na watenda dhambi waliangamizwa kwa maji. Vivyo hivyo habari za moto wa milele zilizoandikwa kwenye Biblia ni za kweli. Siku inakuja watenda dhambi watatupwa motoni. Tutubu mapema jamani. Wakati wa Nuhu watu waliambiwa gharika itatokea, wakapuuza. Siku ya siku mvua zikaanza kunyesha za kufa mtu.
 
Jesus is coming soon jamani. Hizi habari za Nuhu ni njia ya kutuamsha tuache kuipuuza Biblia. Yaliyoandikwa ni ya kweli. Ukweli mmojawapo ni huo wa Safina ya Nuhu. Gharika ilikuwepo na watenda dhambi waliangamizwa kwa maji. Vivyo hivyo habari za moto wa milele zilizoandikwa kwenye Biblia ni za kweli. Siku inakuja watenda dhambi watatupwa motoni. Tutubu mapema jamani. Wakati wa Nuhu watu waliambiwa gharika itatokea, wakapuuza. Siku ya siku mvua zikaanza kunyesha za kufa mtu.
Hakika mkuu.
katika hili sikupingi hata kidogo.
 
Hakika mkuu.
katika hili sikupingi hata kidogo.
Amina. Ila wewe uliniahidi utabadili hiyo avatar yako. Kwanini unapenda uongo wakati unajua kuwa waongo hawataingia mbinguni.
 
Kuna mtu mwenye akili zake timamu anaweza kuamini ujinga huu? Kwani, wakiingundua, inatuongezea ugali mezani?
Adha dharau, mkuu. Mimi hiyo habari imeniongezea imani hata ya kutafuta pesa za kununua ugali
 
ministrant
You ask, ‘So what?’ OK sir, and that simple question opens the door to something much deeper...

Usipozama deep, habari ya kuonekana kwa safina ya Nuhu unaweza kufikiri inawahusu walokole tu. Ngoja "nikuchanue!" Habari hiyo inatufundisha mambo ya msingi sana yanayoweza hata kutusaidia kiuchumi:

Kwanza, inatufundisha kuhusu utii na maandalizi. Nuhu alitii maagizo ya Mungu na akafanya maandalizi ya jambo ambalo wengine waliona ni upuuzi. Kiuchumi, hiyo inatufundisha umuhimu wa kuwa na maono ya mbali. Taifa lolote lisipojifunza kutii kanuni za kiuchumi na kufanya maandalizi ya dhati, litabaki tegemezi.

Pili, inatufundisha kutokukata tamaa hata tukionekana wendawazimu. Nuhu alidhihakiwa kwa miaka mingi, lakini hakukata tamaa. Sisi pia, Afrika, hatupaswi kukata tamaa mbele ya changamoto za utegemezi wa nje. Tuanze na mambo madogo: uzalishaji wa ndani, nidhamu ya matumizi, na uwajibikaji, bila kujali wanaotubeza.

Tatu, habari hiyo inatufundisha ukweli wa kihistoria. Inajenga imani na uthubutu. Ukiwa na imani kwamba Biblia sio hadithi bali kitabu chenye habari na historia halisi, unapata nguvu ya kuamini hata ahadi za Mungu kuhusu kuinuliwa na kufanikiwa (Kumbukumbu 28:1-13). Hii imani inachochea pia uthubutu wa kiuchumi.

Kwa hiyo, ndugu yangu ministrant, habari hiyo ni sehemu ya ukombozi wetu: kiroho, kiakili na hata kiuchumi. Ukombozi huanza na kufunguka kwa akili!

Curious to hear your take!!
Una umri gani binti?
 
Safina ya nuhu inaingia mara3 kwa ukubwa kwenye meli kama Icon of the sea au MSC Irina.

Kumbuka Icon of the sea na MSC irina hata zikiwekewa features gani kwaajili ya kuchukua kila sample ya kiumbe haiwezi kwani vitakua vingi mno lakini vingine vitahitaji kuchukuliwa kwa utaalamu wa maabara.

Leo mtu anakuja kutuambia hicho kisafina cha ukubwa wa meli ya kawaida kilichukua everything - Stupid!!

Kuna mtu mmoja aliwahi sema Sikuhizi watu hawafikirii tena ila Watu wanahisi.
My friend Ibn Unuq
Safina haikubuniwa na mtu. Designer ni Mungu mwenyewe(Mwanzo 6:14-16) na vipimo vya Safina ni Mungu mwenyewe ndiye aliyempa Nuhu atengeneze Safina ili kuokoa uhai wa viumbe hao. Mungu hana mipaka kama sisi wanadamu. Anaweza kutenda mambo yasiyoelezeka kwa hesabu zetu (Isaya 55:8-9). Aliyeweza kuumba ulimwengu mzima kwa kutamka neno tu, ni vigumu kwake kuleta wanyama waliotakiwa na kuwafanya waingie na kukaa kwenye safina kwa mpangilio?

Habari ya Safina kuiita “stupid” ni kujionyesha kuwa wewe ni mtu usiyejua uwezo wa Mungu. Neema ya Mungu ikufunike.
 
Hii pimbi na biblia yake ni ya kublock
Hahaa, Smart Contract nakuruhusu uniblock tu hata kwa matofali 100, lakini ukweli umeishaujua. Safina imeonekana. Mliofikiri Biblia ni story za kijiweni sasa mmethibitishiwa na wabobevu wa sayansi. Hamtakuwa na udhuru siku ya hukumu. Nuru imekuja mmependa giza kuliko nuru. Sawa.
 
Kuna documentary niliangalia kuelezea hiyo safina. Kiujumla hiyo si yenyewe. Ni ndogo sana kulinganisha na ya Nuhu
Unaamini documentary kuliko data za Geologists?
Weka hapa data zako zinazoonyesha kuwa hiyo 'ni ndogo sana.'
 
Wewe usha wehuka wewe, unaamini vitu vya kijinga sana, halafu unaleta huku, huku watu wanatuia akili zaidi kuliko imani.
Kumbe hata maana ya imani huijui. Ngoja nikusaidie...
"Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
(Ebr 11:1-3)
Ngoja nikupe mfano. Pepo au majini ninaamini wapo; hii ni sawa na kusema: Pepo au majini nina hakika wapo. Ndio sababu nikiwafukuza kwa Jina la Yesu wanakimbia.

Amka utoke usingizini!
 
Bibilia ni kitabu cha historia, kuna hqbari za kweli, kuna habari za kutunga hivyo ugunduzi wao unaweza kuwa kweli ila kwwnye bibilia tunasoma safina ilitulia juu ya kilima gani vile na kipo nchi gani hicho kilima kasome vizuri kama hakipo ugiriki tafiti zao za uwongo
Umesoma kwenye Biblia yako?
Mimi Biblia yangu mbona iko wazi kabisa kuhusu mahali ilipotua Safina: ‘...ikakaa juu ya milima ya Ararati’ (Mwanzo 8:4). Milima ya Ararati iko katika eneo la leo la mashariki mwa Uturuki, karibu na mipaka ya Armenia na Iran — sio Ugiriki, my friend Elly official
 
Back
Top Bottom