Una lipi la kusema kwa ma agent wa Clautos Chama na Fabrice Ngoma kulalamikia timu zao haziheshimu kipengere cha kuwaanzisha first eleven?

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Kumekuwa na mgongano wa maslahi binafsi ya wachezaji na maslahi ya kitimu ndio yanasababisha hizi kelele, Wachezaji wanaogopa sana kuanzia benchi au / na kupewa muda kidogo sababu mikataba ikiisha ni ngumu kupata timu nzuri lakini kocha anaweka maslahi ya timu kupata ushindi mbele zaidi.

Yasemekana kwenye mikataba ya hawa wachezaji husika, kulikuwa na makubaliano special ya kuwalinda kwamba wapewe kipaumbele cha kuanza kila mechi kubwa lakini uhalisia ni tofauti, wanasugua benchi na kuingia dakika za mwisho kusukutua.

Binafsi naona wachezaji wawe wanajiongeza, Ngoma na Chama na ma agent WAMEPIGWA !! lakini zaidi ni kwa wachezaji hawajiongezi kwamba ni kocha ndie anaepanga kikosi, timu ikifungwa lawama ni kwa makocha.
 
Waache ujinga wao, kocha ndio anayepanga kikosi kulingana na mbinu alizoziandaa kwa mechi husika.

Kuna mechi ambayo atahitaji kuzuia zaidi kuliko kushambulia, kwa hiyo itakuwa fresh huyo mchezaji acheze kama full back wakati yeye role yake ni winga?

Kocha anapanga kikosi kulingana na kile anachokiona mazoezini, sasa kuna wachezaji wanategea kwa factor ya kuwa wanauhakika wa kuanza kwasababu mkataba wao umewataka waajiri wao kufanya hivyo.

Huo ni upuuzi.
 
Hakuna kipengere cha namna hiyo wala mkataba wa kihuni hivyo.
Mchezaji anasajiriwa ili akaitumie timu. Sasa kukaa benchi, kuanza dakika za mwanzo au kuingia dakika za mwisho vyote hivyo ni sehemu ya huo utumishi katika timu.
Ila kwa hali hii ikiendelea Chama anaweza kuondoka hata kabla mwaka haujaisha.

Chama kasajiliwa zaidi kuwa mchezaji wa kuwakomoa Simba, Sio kwa mipango ya kocha Gamondi.

Ndio yale yale kama ya Mkude, ila at least mkude hata mshahara wake ni wa kawaida sana kwa level za Yanga.
 
Yasemekana kwenye mikataba yao kulikuwa na makubaliano ya ziada kwamba wapewe kipaumbele lakini uhalisia ni tofauti, wanasugua benchi na kuingia dakika za mwisho kusukutua.
Wavunje mikataba Yao wakasajiliwe pamba jiji fc
 
Hakuna kipengere cha namna hiyo wala mkataba wa kihuni hivyo.
Mchezaji anasajiriwa ili akaitumikie timu. Sasa kukaa benchi, kuanza dakika za mwanzo au kuingia dakika za mwisho vyote hivyo ni sehemu ya huo utumishi katika timu.
Ligi ya bongo ina mambo mengi mi hilo hata sishangai kusikia kuwa lipo.

Kuna wachezaji naskia walishawahi kusaini mikataba ya kui demand Club kuwa atakuwa anatokea home na sio kambini.
 
Yasemekana kwenye mikataba yao kulikuwa na makubaliano ya ziada kwamba wapewe kipaumbele lakini uhalisia ni tofauti, wanasugua benchi na kuingia dakika za mwisho kusukutua.
Tuanze na kujibu nini maana ya first eleven , baada ya hapo tujibu pia je hao wachezaji hucheza first eleven baada ya kujibu haya maswali msingi ndiyo majibu ya swali lako
 
Tuanze na kujibu nini maana ya first eleven , baada ya hapo tujibu pia je hao wachezaji hucheza first eleven baada ya kujibu haya maswali msingi ndiyo majibu ya swali lako
Sio mtaalam sana wa maneno ya soka lakini kurahisisha ni kwamba wanataka wasiwe wanaanzia benchi na wapewe muda mwingi wa kucheza
 
Chama kaitumikia simba ila mafao kalipwa na GSM ,kwa ufupi amekwisha
 
Babu Chama kaponzwa na tamaa ya pesa. Apelekwe kwa mkopo mashujaa fc aimarishe kiwango chake au arudi Lusaka akalee vijukuu.

Ngoma naye kwa simba hii ya vijana hawezi pata namba. Akubali kuilipa simba pesa ya kuvunja mkataba akatafute changamoto nyingine
 
Chama kaitumikia simba ila mafao kalipwa na GSM ,kwa ufupi amekwisha
Amekwisha wapi mkuu, uliona jana alivyotoa assist ya kuwakamua azam bao la nne ??

Chama ana 32 bado kwenye soko ana demand, tatizo ni kwamba pale Yanga kuna wachezaji wazuri kumzidi.

Wachezaji wengi huwa wanofia wasipopata muda wa kucheza, mikataba ikiisha inakuwa ngumu kupata timu, mara nyingi wanapara timu za chini badala ya level sawa na wanazoziacha ama za juu zaidi
 
Sio mtaalam sana wa maneno ya soka lakini kurahisisha ni kwamba wanataka wasiwe wanaanzia benchi na wapewe muda mwingi wa kucheza
SWali fikirishi je timu inatakiwa ishinde? Ama mradi wao wacheza hata kama hawako timamu kimwili
 
SWali fikirishi je timu inatakiwa ishinde? Ama mradi wao wacheza hata kama hawako timamu kimwili
Hapo ndipo panapotokea mgongano wa maslahi binafsi na maslahi ya timu, Conflict of interests !!
 
Wewe kwa uelewa wako unahisi Yanga wanaweza ingia mkataba wa hivi na Chama?

Kina Aziz wenyewe wanaanziaga bench sometimes ije kuwa Chama?
 
Wewe kwa uelewa wako unahisi Yanga wanaweza ingia mkataba wa hivi na Chama?

Kina Aziz wenyewe wanaanziaga bench sometimes ije kuwa Chama?
Ma agents wamewaingiza chaka wachezaji wao ili wapige commision 😀😀
 
Sidhani.
Mashindano yapo mengi, mechi zipo nyingi na uwezo wa kucheza upo wazi. Yanga walimsajiri Chama ili kuwa na uhakika wa kutwaa mataji yote msimu huu. Na assist ya goli la nne jana dhidi ya Azam ndio lilimuonyesha Chama kwanini ameletwa Yanga.
 
Waanze hata kama
Hawana Kiwango?
 
Sidhani.
Mashindano yapo mengi, mechi zipo nyingi na uwezo wa kucheza upo wazi. Yanga walimsajiri Chama ili kuwa na uhakika wa kutwaa mataji yote msimu huu. Na assist ya goli la nne jana dhidi ya Azam ndio lilimuonyesha Chama kwanini ameletwa Yanga.
Asubiri mechi za namungo,jkt,pamba and a kike ila sio hizi big matches
 
Hizo siyo bogus treaties kweli? Yaani hicho kipengele huwa kinaandikwa kabisa kwenye mkataba au huwa kinafichwa fichwa?

Nasema bogus treaty kwa sababu mkataba unafungwa na viongozi, halafu kocha ndiye anakuja kupanga timu. Akisema huyu ataingia kipindi cha pili kwa sababu mfumo wa kipindi cha kwanza ni mfumo tofauti, je kuna wa kumbishia kocha?

Na je, hicho kipengele kinaweza kumfanya mchezani akavunja mkataba au hata kushtaki FIFA kwamba mkataba unakiukwa wa kutopangwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…