Una miaka zaidi ya 50 halafu unaenda kununua kiwanja kwa Milioni 500. Pesa yako itarudi lini?

Una miaka zaidi ya 50 halafu unaenda kununua kiwanja kwa Milioni 500. Pesa yako itarudi lini?

AI BRAINFULL

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2019
Posts
2,122
Reaction score
5,319
Nimegundua watu wengi wanaonunua maeneo na majengo ya kuanzia Tsh 500M mpaka 5B hapa jijini Dar, wengi wao wana umri wa kuanzia miaka 50. Ni nadra kukuta kijana wa miaka 30 ananunua viwanja vya bei hiyo.

Swali langu ni: Uwekezaji wao utarudi baada ya miaka mingapi, hapo achana na kupata faida?

Ukizingatia kuwa, hasa sisi Waafrika karibu 90% ya mali zetu haziendelezwi na vizazi vinavyofuata, yaani mzee akifariki, na michongo yake nayo huondoka.
 
Ukichunguza watu wanaonunua maeneo na majengo yakuanzia 500m-5b hapa jijini DAR wengi tena 70% umri ni kuanzia miaka 50 swali langu uwekezaji wao utarudi baada ya miaka mingapi apo achana na kupata faida na ukizingatia hasa sisi watu weusi 90% mali zetu hua haziendelezeki kupitia vizaz yaan mshua ukifa na mali,michongo nayo hufa
Akili ndogo hii

Watu wanaangalia generational wealth
 
Mtu mweusi na ubinafsi ni chanda na pete. Tuseme wewe mleta mada kila kitu/uwekezaji unaoufanya ni kwa faida yako peke yako tu? Si watoto achilia mbali jamii baki. Kama ni hivyo basi una akili finyu sana. Hata kama nyingi haziendelezwi ndo tusifanye maendeleo yeyote kwa sabb tutakufa?
 
Kuna familia ina uchumi wa kuogopwa inaitwa Rockefeller angalia hapa kuanzia mwaka 1830's

Wapo na watakuwepo
1789241781216.jpeg

Na hiyo sio whole history ni kipande tu
 
Singumzii ubinafsi bali upotevu wa mali baada ya mtafutaji kufa...je mlishawai kujua haya maeneo na majengo yanayouzwa kwa mabilion hapa mjini 80% wahusika na walioyatafuta wamekufa na waendelezaji wanaona bora kuuza na kugawana pesa sasa kama unatafuta alafu kizaz kinakuja kupoteza sio hasara?
 
Singumzii ubinafsi bali upotevu wa mali baada ya mtafutaji kufa...je mlishawai kujua haya maeneo na majengo yanayouzwa kwa mabilion hapa mjini 80% wahusika na walioyatafuta wamekufa na waendelezaji wanaona bora kuuza na kugawana pesa sasa kama unatafuta alafu kizaz kinakuja kupoteza sio hasara?

Kwa hyo soln ni kuishi maisha ya kizembe na kidgo utachopata ni kutumbua kabla hujafa ili usiache chochote nyuma kwa yeyote?
 
Akili ndogo hii

Watu wanaangalia generational wealth
Kuna jamaa Kibaha kaanzisha mradi wa million 400+ hivi.
Ni mtu mzima hakosi miaka 60 hivi.

Yuko na mtoto mmoja tu kazi yake kuzichapa qumq za wanawake mpaka kabadilisha dini anaitwa Abubakari.

Sasa kaja kule kwenye mradi ikabidi Mzee amseme mtoto wake anamwambia

"Mwanangu mimi mpaka umri huu Sina Cha kupoteza, mradi huu nauanzisha Kwa ajili Yako, bila shaka mpaka nakufa huu mradi utakuwa bado sawa, kama utafia mikononi mwako hiyo ni juu Yako, mimi sitakuwepo Tena"


Sasa Mzee angekuwa mbinafsi asingeweka hizo hela kwenye huo mradi, lakini kupitia mradi huo ametengeneza kwanza Ajira rasimi na ambazo siyo rasimi Kwa watu wengi
 
Au ndio utakatishaji wenyewe wa fedha? Na hapa dar ndio panaongoza kwa maeneo na majengo kuuzwa kwa mamilioni na mabilio na wahusika 85% ni warithi na watu walioshindwa kuendeleza maeneo hayo
Una akili fipu sana sana wewe. Omba Mungu upate exposure kwa kusafiri na kuishi na jamii nyingine. Ila sikulaumu sana kwa sababu wewe ni muhanga wa elimu na ulimbukeni kama walivyo wabongo wengi. Mawazo mgando kabisa.
 
Kuna kitu kinaitwa "Generational wealth creation" nafikiri hujawahi kijua au una ukavu macho nacho au umetoka familia ambayo haikujali/kutengeneza utajiri wa kizazi cha tatu au cha nne mbele.
Real estate ni moja ya njia za kuhakikisha utajiri unatoka kizazi kimoja kwenda kingine.

"Someone is sitting in the shade today, because someone planted a tree long time ago"- Warren Buffet
 
Miradi iliyo hai yenye faida iliyoanzishwa na watanzania weusi hapa tz na kuachwa kwa watoto 90% hufa hasa muasisi nae akifa au akiacha kufuatilia ni10% tu ya mali na miradi yakuridhi hukua au kuishi baada ya muasisi kufa
 
Back
Top Bottom