Kuna jamaa yangu analea mtoto wa mganga mpaka leo hii.
Jamaa alihangaika sana kuhusiana na swala la kupata mtoto. Kila wanapokwenda yeye na mkewe waliambiwa hawana tatizo.
Baada ya maneno ya wakwe kuwa mengi, mwanamke akaamua kwenda kutafuta utatuzi na upande wa jadi.
Alikwenda kwa mzee mmoja Kigoma ambae alikuwa ni maarufu kwa maswala ya magonjwa ya uzazi kwa wanawake.
Inasadikika moja ya dawa aliyopewa bi dada ilikuwa ni kupakwa kwa kupitia uume wa mganga kuingiza kwenye uke. Hii dawa ilifanyika siku tatu mfululizo.
Aliporudi nyumbani, ndani ya wiki kadhaa akaanza kuona dalili za ujauzito na kwenda kupima imo. Jamaa alifurahi kuwa kapata mtoto hatimae.
Mtoto kuja kuzaliwa hakuwa akifanana na yeyote baina ya mama na baba. Minong'ono ikaanza kama kawaida ila jamaa hakutulia maanani.
Aliekuja kufichua siri ni dada wa mwanaume baada ya kupelekwa kwa mganga na wifi yake. Huko alikutana na watoto wa mganga ambae ni copyright na mtoto wa kaka yake na bandika bandua na sura ya mganga mwenyewe.
Baada ya kumuhoji vizuri wifi yake, ndio ikabidi aeleze alivyopakwa dawa mpaka kujikuta na ujauzito na hakuwa akijua ni wa nani mpaka baada ya kuwaona kaka na dada wa mtoto wake.