Unadhani hii Nguvu Kubwa ya Watanzania Kuijadili DP World ije au isije ingehamishwa Kujadili ya Msingi tungekuwa 'Masikini Tukuka' hadi Leo?

Tungejadili mambo mambo mengine hv, basi CCM wangetuheshimu sana.Yawezekana ndo tumeamka
 
Kukodishwa kipande cha ardhi kwa mgeni muda usiojulikana mwisho wake ni ishu pevu lazima ijadiliwe kwa nguvu zote
 
Waziri alishasaini kwa niaba ya Rais na Bunge likapitisha.Kwa sasa wapiga kelele ni hawana uelewa.
 
Nadhani ni mfumo umeamua iwe hivi, kama wangetaka iwe kinyume chake huu mjadala ungekuwa umezimwa siku nyingi tu.
 
Elimu ya Tanzania ni Mbovu na mbaya sana tena iko ICU kwa sasa je, ni lini mtatumia muda wenu na hizi nguvu zenu nyingi Kuijadili?
ni kweli tuna elimu mbovu balaa, jirani zetu kenya watatuzidi maarifa tusipofanya marekebisho. Tukiendelea kuwa na elimu mbovu akina DP World na wengine wa aina hiyo ya uwekezaji watakuja kwa wingi kuwekeza nchini mwetu wakidai wanawekeza kwa ufanisi na tija huku tukiwaangalia tu wanavyovuna rasilimali zetu kwa faida ya mataifa yao
 
Kwahiyo bandari sio jambo la msingi la kijadili ???
Kati ya Elimu mbovu iliyoko Tanzania na Sakata hili la Bandari na DP World Kwako Wewe kama zinachaji kweli Mtimani mwako lipi ambalo Wengi wetu ndiyo tulitakiwa tulipigie sana Kelele tena Usiku na Mchana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…