Unafikiri hili litawezekana kwa siasa zetu za Tanzania?

Unafikiri hili litawezekana kwa siasa zetu za Tanzania?

Umeona ile video ya mortuary???
Nimeuona ule uzi ila sijaifungua.
Zile za barabarani tu niliangalia nikashindwa kulala siku 3 💔💔🙌 sijawahi kuona unyama kama ule.
 
Katiba ya Zanzibar ndivyo inavyosema kwamba lazima kuwe na mgawanyo wa madaraka baina ya chama kinachopata ushindi na vyama vinavyofuata na hii inakwenda kwa % ya kura zinazopata kila chama. Zanzibar kuna SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA.
Japo katiba yetu haisemi hivyo, ila katiba ya JMT imempa Raisi mamlaka ya kuchagua anavyopenda so hili liko ndani ya uwezo wake.
 
Wazo Hilo ni baya kuliko kawaida na Lissu hawezi kuingia kwenye mtego huo,.

Maalim Seif aliingia kwenye mtego huo(kusaliti) na CUF ikafa Zanzibar..
Nakumbuka hii, ilikua kifo cha Maalim Seif na CUF kisiasa
CCM ilikua na amani enzi za Mbowe sababu kila chadema wakianzisha movement,ikifika mahala pazuri Serikali inamuita MBOWE wanakunywa "Kahawa" wanafanya maridhiano harakati zinasimama..

Lissu hataki maongezi na Mtu Wala kahawa na Mafisadi,yeye anataka kitu kimoja tu HAKI&KATIBA..

Angekua compromised kama Mbowe asingepigwa risasi,na Wala asingekua jela Leo, unafikiri kwanini CCM ilimpigia Mbowe kampeni za uenyekiti wa Chadema??walijua haya yatatokea na Lissu akishinda andazi litakua gumu..

So Hell No..
Sawa, hoja imejitosheleza, nimekuelewa!
 
Fatilia vitu! Z'bar makamu wa pili wa Rais hua anatoka chama Cha upinzani, maalimu seif unakumbuka?
Huku bara hamna huo utaratibu, hua Wana pewa wadhifa wa "waziri kivuli" haunaga maana yoyote.

Yaan ili watanzania tupone tunataka structure yote uongozi wa Tanzania ivunjwe kuanzia president Hadi waku wa vyombo vya usalama.

Yaan katika ulimwengu wa science na technolojia sisi Bado tunaongozwa kibabe. Kundi la watu wachache ndio wananufaika na mali zilizotakiwa tunufaike wote.

Note: Tunavo ishi Leo ni matokeo ya mapambano ya wazee wetu enzi za ukoloni na hatimae tulipata uhuru 1961. Kinachotakiwa kwa sasa ni kupambania vizazi vyetu ili huko badae maisha Yao yawe mazuri na sio kundi la watu wachache waendelee kunufaika.

Ukombozi ni mchakato wa muda mrefu., Mapambano yaendelee .
💯 💯
Sina cha kuongeza, kama wana masikio na wasikie!
 
Samia hawezi kufanya lolote mpaka Katiba ibadilishwe.
Acha tuone, mabadiliko ya katiba lazima yasimamiwe na viongozi wenye weledi.

Kwa sasa hata mchakato ukianza sijui kama utatupatia matokea yanayofaa, na yatajirudia yale yale yaliyotokea kwenye rasimu ya Warioba.
 
Nimewaza:
Vipi kama Samia akishauriwa kufanya kama Raisi Mwinyi kule Zanzibar na kuvipa vyama vya upinzani nafasi za uwaziri?

Hili likafuatiwa na Mh. Tundu Lissu kuachiliwa, kisha kuteuliwa kuwa mbunge na waziri na kisha kukabidhiwa wizara ya katiba na sheria.

Vipi kama Mh. Lissu ataliongoza taifa kuwawajibisha kisheria wale waliohusika na mauaji ya Oktoba 29 pamoja na kupata katiba mpya. Na baada ya upatikanaji wa katiba ukaitishwa uchaguzi huru na wa haki, utakaoongozwa na kulindwa na katiba hii mpya?

  1. Je hili linawezekana? na je litakua jambo la busara kuliko kuharakisha kwenye maridhiano?
  2. Na je, litasaidia kuisogeza nchi mbele kutoka hapa tulipofikia?

PS:
Nimeongelea uwaziri kamili na siyo uwaziri kivuli, na kama itatokea basi waziri apewe nafasi ya kupendekeza katibu mkuu wa wizara na siyo kupangiwa yule wa kuteuliwa na raisi.
Kwanza ufanyike uchaguzi then ashinde ndipo hiyo suggestion itakuwa logical, as for now she is not the president.
 
Kwanza ufanyike uchaguzi then ashinde ndipo hiyo suggestion itakuwa logical, as for now she is not the president.
Nakubaliana na wewe 💯

Lakini baada ya kupoteza mabilioni kwenye uchaguzi wa mgombea mmoja, unafikiri kama nchi tuna uwezo wa kifedha wa kufanya uchaguzi mwingine tena ndani ya muda mfupi?
 
What's the alternative?
Kama ni Samia kujiuzulu, sawa aondoke; then what should be next?
New constitution.

New independent electoral commission.

A reformed police force.

A reformed independent judiciary.

A reformed legislature.

Fresh new elections.

Siku zote tunayasema hayo kumbe huelewi? 😂
 
Angekua anateua yeye, Angefanya.
Shida ni kua yeye mwenyewe anapewa majina, na wanao toa vimemo hawataki kelele za wapenda haki.

Mfano: Hivi Mpina alikua na madhara gani mpaka atolewe kihuni vile, kama wameahindwa kumvumilia mpina watamvumilia TAL
 
New constitution.

New independent electoral commission.

A reformed police force.

A reformed independent judiciary.

A reformed legislature.

Fresh new elections.
💯 agreed na naunga mkono yote
Siku zote tunayasema hayo kumbe huelewi? 😂
Nayaelewa, but nani anafanya na zitafanyikaje?

Kwenye current constitution kuna taratibu za kupata katiba mpya,: Je, ni nani atasimamia huu mchakato? Kuna hoja ya serikali ya mpito; je itapatikaneje? kwa utaratibu gani?

Kama unafahamu na mimi nimemiss majibu ya haya maswali somewhere, naomba unifahamishe tafadhali.
 
Nimewaza:
Vipi kama Samia akishauriwa kufanya kama Raisi Mwinyi kule Zanzibar na kuvipa vyama vya upinzani nafasi za uwaziri?

Hili likafuatiwa na Mh. Tundu Lissu kuachiliwa, kisha kuteuliwa kuwa mbunge na waziri na kisha kukabidhiwa wizara ya katiba na sheria.

Vipi kama Mh. Lissu ataliongoza taifa kuwawajibisha kisheria wale waliohusika na mauaji ya Oktoba 29 pamoja na kupata katiba mpya. Na baada ya upatikanaji wa katiba ukaitishwa uchaguzi huru na wa haki, utakaoongozwa na kulindwa na katiba hii mpya?

  1. Je hili linawezekana? na je litakua jambo la busara kuliko kuharakisha kwenye maridhiano?
  2. Na je, litasaidia kuisogeza nchi mbele kutoka hapa tulipofikia?

PS:
Nimeongelea uwaziri kamili na siyo uwaziri kivuli, na kama itatokea basi waziri apewe nafasi ya kupendekeza katibu mkuu wa wizara na siyo kupangiwa yule wa kuteuliwa na raisi.
Zanzibar pale kuna umoja wa kitaifa ambao .baada ya uchaguzi kufanyika kinacho fanyika ni mgombea urais aliye shika nafisi ya pili anakuwa makamu wa kwanza wa rais.

Wew unacho kiongela hocho ni kama kilicho tokea kenye 2008 kwa marehemu raila ondinga ndio iliundwa hiyo serekali ya umoja wa kikatiba.

Lakn? Una wajua ccm vizuri😂 katiba mpya ndio mwisho wao .unafikiri itakuwa,rahisi sana kukubali tu.

Na vipi kuhusu vifoo vya jamaa na ndugu zetu 29/30/31 .kwanza kuna watu inabidi wawajibike kwa hilo.

Sema kila mtu analonda ugali wake wacha inyeshe tu jue panapo vuja
 
Angekua anateua yeye, Angefanya.
Shida ni kua yeye mwenyewe anapewa majina, na wanao toa vimemo hawataki kelele za wapenda haki.
Hilo ndiyo tatizo kubwa, inawezekana tuna kiongozi ambaye ameshikiwa mamlaka na kikundi cha watu.
Mfano: Hivi Mpina alikua na madhara gani mpaka atolewe kihuni vile, kama wameahindwa kumvumilia mpina watamvumilia TAL
Hili lilinishangaza sana na naamini hii ni moja ya downfall zake kubwa.
 
Nakubaliana na wewe 💯

Lakini baada ya kupoteza mabilioni kwenye uchaguzi wa mgombea mmoja, unafikiri kama nchi tuna uwezo wa kifedha wa kufanya uchaguzi mwingine tena ndani ya muda mfupi?
Bora kugharamia whatever the cost tupate kiongozi wa nchi kuliko kutawaliwa na haramia aliyejipachika kwa njia haramu, gharama atakayolitia taifa mpaka amalize huo uharamu wake itakuwa ni balaa.
 
Back
Top Bottom