Unafikiri hili litawezekana kwa siasa zetu za Tanzania?

Unafikiri hili litawezekana kwa siasa zetu za Tanzania?

Yani sehemu zote hawakuona wameona mtako tu?

Mtako hata ukiufungia ndani unatokezea mpaka nje 😂😂

Ila poleni sana jamani.
Asante, tunaendelea kupoa.

😂😂 Labda walitaka wapige itokee upande wa pili, waniharibie fahari yangu.
Vijana walinipambania hakikuharibika kitu.
 
Waebrania 2:3
[3]sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;
 
Wew unacho kiongela hocho ni kama kilicho tokea kenye 2008 kwa marehemu raila ondinga ndio iliundwa hiyo serekali ya umoja wa kikatiba.
Hichi ndicho nilichowaza, maana hata Kenya, hatua hii ndiyo ilikua namna pekee ya kurudisha amani na kuunda serikali ya pamoja ili kuleta katiba mpya.

Nina wasiwasi mkubwa sana endapo CDM na vyama vingine vya upinzani vtakosa ushiriki wenye meno kwenye mchakato wa katiba mpya.
Lakn? Una wajua ccm vizuri😂 katiba mpya ndio mwisho wao .unafikiri itakuwa,rahisi sana kukubali tu.
Ndiyo maana kuna maandamano na sauti za umma kuwashurutisha, wenyewe tu hawawezi kukubali.
Na vipi kuhusu vifoo vya jamaa na ndugu zetu 29/30/31 .kwanza kuna watu inabidi wawajibike kwa hilo.
💯 ni lazima
Sema kila mtu analonda ugali wake wacha inyeshe tu jue panapo vuja
💯
 
Hapana. Awekwe pembeni, atembezwe kwenye maiti zote aliowaua kwa 'order' yake halafu apelekwe nyuma ya nondo.
Katiba imemuwekea kinga, hawezi kuwekwa nyuma ya nondo 😤😫.

Screenshot 2025-11-16 at 11.12.22.png


Exception 46A (10) - Ni Bunge pekee ndiyo linaweza kumvua hiyo kinga

Screenshot 2025-11-16 at 11.11.05.png


Ukitaka kusoma hizo ibara - Katiba JMT ipate HAPA - ukurasa wa 36, 37 na 38
 
Hivi unajua kwanza kama hii serikali ni haramu?

Kuruhusu wapinzani wajiunge nao ni kudharau wananchi.

Halafu usichokielewa hayo maridhiano ni ya wananchi na serikali haramu sio wapinzani..

Kinachotakiwa kufanyika sasa

Rais haramu na serikali yake haramu wapishe uchunguzi ufanyike

Tupate katiba mpya, tume huru ya wananchi sio hii ya sasa.

Uchaguzi urudiwe sio huu ambao wananchi hatuutambui.

Uchunguzi ufanyike na vyombo vya nje, Ili waliosababisha mauaji ya halaiki wawajibishwe hapo safari (The Hague) wakajibu mashtaka kuanzia Samia na majeshi yote ya ulinzi na usalama..!!
 
Nimewaza:
Vipi kama Samia akishauriwa kufanya kama Raisi Mwinyi kule Zanzibar na kuvipa vyama vya upinzani nafasi za uwaziri?

Hili likafuatiwa na Mh. Tundu Lissu kuachiliwa, kisha kuteuliwa kuwa mbunge na waziri na kisha kukabidhiwa wizara ya katiba na sheria.

Vipi kama Mh. Lissu ataliongoza taifa kuwawajibisha kisheria wale waliohusika na mauaji ya Oktoba 29 pamoja na kupata katiba mpya. Na baada ya upatikanaji wa katiba ukaitishwa uchaguzi huru na wa haki, utakaoongozwa na kulindwa na katiba hii mpya?

  1. Je hili linawezekana? na je litakua jambo la busara kuliko kuharakisha kwenye maridhiano?
  2. Na je, litasaidia kuisogeza nchi mbele kutoka hapa tulipofikia?

PS:
Nimeongelea uwaziri kamili na siyo uwaziri kivuli, na kama itatokea basi waziri apewe nafasi ya kupendekeza katibu mkuu wa wizara na siyo kupangiwa yule wa kuteuliwa na raisi.
Lisu hana (hataki) Siasa za maji taka... The man knows what's struggling for!!

Kumpa Lisu uwaziri ni cheo kidogo sana kwake na hiyo ni sawa na kumnunua tu... Na itakua aibu na fedheha kubwa kwake na kwa Watanzania.. we need changes in our system. We don't need ngonjera za CCM"
 
Hivi unajua kwanza kama hii serikali ni haramu?
Kuruhusu wapinzani wajiunge nao ni kudharau wananchi.
Halafu usichokielewa hayo maridhiano ni ya wananchi na serikali haramu sio wapinzani..
Nakubaliana na wewe 100%

Ila nafikiri tunaishia katikati kwenye kupambanua nini kifanyike next.
Nimemuuliza pia Nyani Ngabu maswali haya.
Kinachotakiwa kufanyika sasa

Rais haramu na serikali yake haramu wapishe uchunguzi ufanyike
Hili halina ubishi.

Wampishe nani ambaye ata-take over? Kama kutakua na baraza maalum litaundwaje? nani atasimamia kuundwa kwake?

Katiba inalipa bunge mamlaka hayo, kama bunge la sasa ni haramu, tutarudi kwenye bunge lililopita au? na je bunge lililopita lenye idadi kubwa ya wabunge wa CCM litatupa baraza la mpito lenye meno na uwezo wa kutenda haki?
Tupate katiba mpya, tume huru ya wananchi sio hii ya sasa.
Uchaguzi urudiwe sio huu ambao wananchi hatuutambui.
Uchaguzi mpya urudiwe kwa tume gani? usimamiwe na nani? Hata Samia akijiuzulu atapokewa kijiti na makamu wa raisi, ambaye bado atakua na mamlaka yale yale ya kuunda tume. Je hili litaleta mabadiliko yoyote ya kimuundo?

Katiba mpya ni mchakato wa kisheria, ipatikanaje? au tuendeleze kwenye rasimu ya Warioba?
Uchunguzi ufanyike na vyombo vya nje, Ili waliosababisha mauaji ya halaiki wawajibishwe hapo safari (The Hague) wakajibu mashtaka kuanzia Samia na majeshi yote ya ulinzi na usalama..!!
100% hili halina majadiliano wala mbadala.
 
Hili halina ubishi.

Wampishe nani ambaye ata-take over? Kama kutakua na baraza maalum litaundwaje? nani atasimamia kuundwa kwake. Katiba inalipa bunge mamlaka hayo, je kama bunge la sasa ni haramu? tutarudi kwenye bunge lililopita au? na je bunge lililopita lenye idadi kubwa ya wabunge wa CCM litatupa baraza la mpito lenye meno na uwezo wa kutenda haki?
Hii nchi bado ina hazina ya viongozi wenye busara wanaoweza kutetea maslahi ya nchi na wananchi.

Nafasi ilikuwa kwa JWTZ ila kwakuwa na wao wameonyesha udhaifu mkubwa, basi inabidi tuwe na serikali ya mpito ikiongozwa na Waziri mstaafu mzee wetu Warioba.

Tupate tume huru ya uchaguzi kisha uchaguzi urudiwe (Hapo kiongozi wa mpito atachagua wawakilishi)
Uchaguzi mpya urudiwe kwa tume gani? usimamiwe na nani? Hata Samia akijiuzulu atapokewa kijiti na makamu wa raisi, ambaye bado atakua na mamlaka yale yale ya kuunda tume. Je hili litaleta mabadiliko yoyote ya kimuundo?

Katiba mpya ni mchakato wa kisheria, ipatikanaje? au tuendeleze kwenye rasimu ya Warioba
Hapa unakoroga mambo swali moja unauliza mara mbili mbili.

Nimekujibu huko juu kuhusu tume

Rais akijiuzulu anaondoka na makamu wake pamoja na viongozi haramu wenzie sababu wote hawana uhalali wa uongozi.

Rasimu ya Warioba ndio tunaenda nayo kuipata katiba mpya.
 
Lissu akikubali huo mtego(serikali mseto) upinzani ndani yake unakufa rasmi, mawazo yake yanakufa rasmi, anakuwa mmoja wao indefinitely.

Refer, Maalim Seif na CUF kule Zanzibar.
Yes, ni risk kubwa.
Wanaweza kutoboa kama Raila na kubaki na influence ya upinzani imara au kufa kama Maalim Seif.
 
Hii nchi bado ina hazina ya viongozi wenye busara wanaoweza kutetea maslahi ya nchi na wananchi.

Nafasi ilikuwa kwa JWTZ ila kwakuwa na wao wameonyesha udhaifu mkubwa, basi inabidi tuwe na serikali ya mpito ikiongozwa na Waziri mstaafu mzee wetu Warioba.

Tupate tume huru ya uchaguzi kisha uchaguzi urudiwe (Hapo kiongozi wa mpito atachagua wawakilishi)

Hapa unakoroga mambo swali moja unauliza mara mbili mbili.

Nimekujibu huko juu kuhusu tume

Rais akijihudhuru anaondoka na makamu wake pamoja na viongozi haramu wenzie sababu wote hawana uhalali wa uongozi.

Rasimu ya Warioba ndio tunaenda nayo kuipata katiba mpya.
Umeeleweka mama, haya kunywa maji basi, ushushe na pumzi 😅😂
 
Back
Top Bottom