Unafikiri hili litawezekana kwa siasa zetu za Tanzania?

Umeona ile video ya mortuary???
Nimeuona ule uzi ila sijaifungua.
Zile za barabarani tu niliangalia nikashindwa kulala siku 3 πŸ’”πŸ’”πŸ™Œ sijawahi kuona unyama kama ule.
 
Katiba ya Zanzibar ndivyo inavyosema kwamba lazima kuwe na mgawanyo wa madaraka baina ya chama kinachopata ushindi na vyama vinavyofuata na hii inakwenda kwa % ya kura zinazopata kila chama. Zanzibar kuna SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA.
Japo katiba yetu haisemi hivyo, ila katiba ya JMT imempa Raisi mamlaka ya kuchagua anavyopenda so hili liko ndani ya uwezo wake.
 
Wazo Hilo ni baya kuliko kawaida na Lissu hawezi kuingia kwenye mtego huo,.

Maalim Seif aliingia kwenye mtego huo(kusaliti) na CUF ikafa Zanzibar..
Nakumbuka hii, ilikua kifo cha Maalim Seif na CUF kisiasa
Sawa, hoja imejitosheleza, nimekuelewa!
 
πŸ’― πŸ’―
Sina cha kuongeza, kama wana masikio na wasikie!
 
Samia hawezi kufanya lolote mpaka Katiba ibadilishwe.
Acha tuone, mabadiliko ya katiba lazima yasimamiwe na viongozi wenye weledi.

Kwa sasa hata mchakato ukianza sijui kama utatupatia matokea yanayofaa, na yatajirudia yale yale yaliyotokea kwenye rasimu ya Warioba.
 
Kwanza ufanyike uchaguzi then ashinde ndipo hiyo suggestion itakuwa logical, as for now she is not the president.
 
Kwanza ufanyike uchaguzi then ashinde ndipo hiyo suggestion itakuwa logical, as for now she is not the president.
Nakubaliana na wewe πŸ’―

Lakini baada ya kupoteza mabilioni kwenye uchaguzi wa mgombea mmoja, unafikiri kama nchi tuna uwezo wa kifedha wa kufanya uchaguzi mwingine tena ndani ya muda mfupi?
 
What's the alternative?
Kama ni Samia kujiuzulu, sawa aondoke; then what should be next?
New constitution.

New independent electoral commission.

A reformed police force.

A reformed independent judiciary.

A reformed legislature.

Fresh new elections.

Siku zote tunayasema hayo kumbe huelewi? πŸ˜‚
 
Angekua anateua yeye, Angefanya.
Shida ni kua yeye mwenyewe anapewa majina, na wanao toa vimemo hawataki kelele za wapenda haki.

Mfano: Hivi Mpina alikua na madhara gani mpaka atolewe kihuni vile, kama wameahindwa kumvumilia mpina watamvumilia TAL
 
New constitution.

New independent electoral commission.

A reformed police force.

A reformed independent judiciary.

A reformed legislature.

Fresh new elections.
πŸ’― agreed na naunga mkono yote
Siku zote tunayasema hayo kumbe huelewi? πŸ˜‚
Nayaelewa, but nani anafanya na zitafanyikaje?

Kwenye current constitution kuna taratibu za kupata katiba mpya,: Je, ni nani atasimamia huu mchakato? Kuna hoja ya serikali ya mpito; je itapatikaneje? kwa utaratibu gani?

Kama unafahamu na mimi nimemiss majibu ya haya maswali somewhere, naomba unifahamishe tafadhali.
 
Zanzibar pale kuna umoja wa kitaifa ambao .baada ya uchaguzi kufanyika kinacho fanyika ni mgombea urais aliye shika nafisi ya pili anakuwa makamu wa kwanza wa rais.

Wew unacho kiongela hocho ni kama kilicho tokea kenye 2008 kwa marehemu raila ondinga ndio iliundwa hiyo serekali ya umoja wa kikatiba.

Lakn? Una wajua ccm vizuriπŸ˜‚ katiba mpya ndio mwisho wao .unafikiri itakuwa,rahisi sana kukubali tu.

Na vipi kuhusu vifoo vya jamaa na ndugu zetu 29/30/31 .kwanza kuna watu inabidi wawajibike kwa hilo.

Sema kila mtu analonda ugali wake wacha inyeshe tu jue panapo vuja
 
Angekua anateua yeye, Angefanya.
Shida ni kua yeye mwenyewe anapewa majina, na wanao toa vimemo hawataki kelele za wapenda haki.
Hilo ndiyo tatizo kubwa, inawezekana tuna kiongozi ambaye ameshikiwa mamlaka na kikundi cha watu.
Mfano: Hivi Mpina alikua na madhara gani mpaka atolewe kihuni vile, kama wameahindwa kumvumilia mpina watamvumilia TAL
Hili lilinishangaza sana na naamini hii ni moja ya downfall zake kubwa.
 
Nakubaliana na wewe πŸ’―

Lakini baada ya kupoteza mabilioni kwenye uchaguzi wa mgombea mmoja, unafikiri kama nchi tuna uwezo wa kifedha wa kufanya uchaguzi mwingine tena ndani ya muda mfupi?
Bora kugharamia whatever the cost tupate kiongozi wa nchi kuliko kutawaliwa na haramia aliyejipachika kwa njia haramu, gharama atakayolitia taifa mpaka amalize huo uharamu wake itakuwa ni balaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…