Hammaz
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 6,607
- 14,076
Nimekuelewa brother! Lakini tunavyowazungumzia kwa ujumla tunaonesha ishara ya mahaba! Tunawapenda kidhati.Nadhani tunatakiwa tuwape uwanja wa wanawake kupendeza watakavyo...wewe wakishapendeza jichagulie unayevutiwa naye.
Uzuri wanawake karibu wote hawatongozi. Mimi kuna mawigi na weaving zinazonivutia saana na baadhi ya kucha. Kope hazinivutii.
kuna wanaume wengine wanavutiwa na kope tuwaachie. Tuwaambie tu tena kistaarabu vile vyenye athari za moja kwamoja kama kudunga sindano za tako na kujibabua.
Kwa sababu urembo wa namna hiyo una side effects. Nakubali kwamba Dunia yetu ya leo kuna vitu vina madhara. Tunavyo vinywa, kula vipo vinavyoepukika na vipo vinavyozuilika kwa kupunguza matumizi.
Tukizungumzia urembo wa mama/Dada zetu Mathalani fake eyelashes: kwa sababu kope asili zinazuia vumbi na uchafu wa namna hiyo kuingia kwenye jicho. Kope wanazoweka ni fake kwa hiyo haziwezi kufanya kazi kiufanisi kama kope halisi.
Na uwekaji wake wanaweka na gundi! Gundi ikiingia machoni huyo mtu anahitaji medical help. Na wataalamu wanasema inaweza kusababisha irritation, ambayo inaweza kusababisha madarosis( ni ugonjwa ambao unasababisha kope zinapukutika).
Halafu Mungu hivi vitu vya maumbile yetu ameviweka kivipimo. Je, uzito wa kope fake unaendana na kope halisi?
Kitakachotokea baadaye huwezi jua.
Sasa hayo yote ni ya nini brother! Na ni urembo wa namna gani huo ambao unaleta madhara ya waziwazi wakati madhara yake kuepukika ni waziwazi.
Halikadhalika na kucha fake nazo zikikosewa kuwekwa tu huyu mwanamke analo. Na hata kuzitoa kwake ni kwa uangalifu sana, akikosea tu mwanamke anaweza akawa na muonekano mbaya sana wa kucha asilia. Na kucha kwa mwanamke ni urembo.
Hata mawigi nayo yana madhara.
Suluhisho waachane nayo hayo. Wajikubali na wajiamini kwa urembo wao, na kuna vipodozi ama urembo ambao hauleti bahati nasibu kwenye madhara, vipodozi halisiya. Wajipambe navyo hivyo.
Ladies! Amani iwe kwenu. Mmmwaaa! Nawapenda.