Unajua kutofautisha kati ya neno furaha, neno utamu, na neno raha?

hapo sasa ndio mimi napata furaha kwenye kutaniana na anonymous being kama hivyo.

I hope that gave you a real sense of what it means to be happy.
Unapenda utani na watu usiowajua jamani🤣🤣
 
Furaha kwanza ni ile hali ya kuwa na amani ya nafsi binafsi pamoja na mwili kwa ujumla ni kitendo cha kuridhika na kile ulichonacho na mara nyingi furaha hudumu muda mrefu, na haichagizwi na kitu kama pesa, huwa kiufupi hii hainunuliki,

Raha ni kitu cha muda mfupi ni ile hali ya mtu kujihisi kubarizi na kufurahia kitu ambacho either kimesababishwa na pesa au mfano pale mtu unapopumzika au kulala ni kitu ambacho huisha pale kile kisababishi kikuu kinapotoweka au kuisha muda wake

Utamu kwa upande wake ni ile hali ya ladha ya kitu mfano chakula au hisia zozote zile zinazoweza kuchochea furaha ya mwili na kumfanya mtu kujihisi burudani
 
Elewa kuwa 'Furaha' ndiye baba wa mhimili wa maisha ya mtu.

Hapa neno 'Utamu' tuliondoe katika muktadha huu, maana halihusiani na furaha waka raha, maana utamu ni aina ya ladha na kinyume chake ni 'uchungu'.

Lakini furaha na raha ni 'mtu na mke wake' maana palipo na raha, furaha hakosekani na palipo na furaha, raha yupo, anayetangulia mbele ya mwenzake ni mr Furaha!

Vyote hivyo ni hisia na ukivihitaji vina gharamikiwa kwa mazingira ama kwa pesa.

Furaha ndiyo thamani halisi ya maisha ya binadamu.

Furaha ikikosekana, dunia utaiona chungu na huwezi kutaka kuishi tena.

Kufungwa ama kutengwa, huwa ni kumnyima mtu furaha.

Mafundisho ya dini yanatuasa tutende mema ili tuje tupate furaha ya milele na kinyume chake ni majuto ya milele.

Umeona furaha ilivyo na thamani?
 
Yooo shukrani sana kaka
 
We mada zako huwa za kichokozi sana

Yaani umeuhamisha ubongo wangu sehemu mbali mbali

Nimewaza, chakula, Nimewaza nyimbo zangu pendwa, nikamwaza mpenzi niliye nae, nikamwaza crush wangu Binti wa zamani na bado hapo hapo ukani kumbushia ex.. Sasa hapa focus yoote imetoka kwa muda

Daah kwanini unanifanya hivi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…