Mtu anayeijua hip hop angejua kwamba sampling ni kitu cha kawaida kwenye huu muziki. Karibu 99% ya nyimbo za hip hop huwa wana-sample nyimbo za genre nyingine.
The fact kwamba sampling watu wanaita "kuiga" ni ushahidi kwamba wengi wanaoposti kwenye huu uzi hawajui kitu kuhusu hip hop.
By the way, kwa kukusaidia, wimbo wa Hit 'em Up ulitumia sample ya wimbo Don't Look Any Further wa Dennis Edward. Biggie na Junior Mafia walitumia hiyo sample kabla ya Pac kwenye wimbo wa Get Money remix. Pac akaamua kuutumia kwenye hiyo diss song (hiki ni kitu cha kawaida kwenye rap beef, wenyewe huwa wanaita "jacking", unachukua beat ya adui yako kisha unaitumia kumdiss).