Kwa big watu huwa wanafosi tu, ila pac ni mkali mnoo kwa big, sio mistari, sio flow, energy, kunata na biti.. Nyimbo pendwa kote huko pac anascore zaidi ya big.
Kama big alikua levels za pac kwanini ngoma zake zisiwe maarufu kama pac, ni mpaka uwe msikilizaji hip hop kweli ndio utazijua ngoma za big.
Hilo moja, mziki mzuri huwa na sifa mbili
1.mtamu masikioni, hapa unakuta mtu anapenda ngoma ya kilingala, ama ya kizungu na wala hajui kinazungumziwa nini mule, mradi tu mtamu masikioni... Ngoma nyingi za pac ni tamu masikioni.
2. Message.. Mtu anasikiliza ujumbe, kile kilichoimbwa, hapa unaweza mkuta mtu nasikiliza ngoma ya Bob, au hata ya fall ipupa, masikioni huelewi ila yeye muelewaji kavutika na ujumbe, hapa pia pac kamuacha big.
Nyongeza kwenye hip hop kuna ishu za vina, kucheza na maneno na kadhalika.. Maneno kuntu, mistari konzi, mistari fikirishi, fid q hapa bongo nahisi ndio kama mfalme sijui, jaribu kuivutia mistari yake huenda ukanielewa, Mfano Wayne kwenye no love anasema.. Bitch you try to kick me while I'm down I will break your leg, I stick to the script, you nigga skip sceens, 🤣
Mie nikisikiliza flow za big Kisha pac, naona bado pac ana flow tamu zaidi, sikiliza ain't mad at cha, all eyez on me, me against the world, Dea mama, hit em up.. Yaan mtu anaflow, hata sijui nikuelezeje.
Kama big wangekuwa wa kiwango cha pac basi kwenye mauzo na kadhalika huko angekuwa wanafanana nae.
JAYJAY na
makaveli10 uzi huu lazima ashinde 2pac mmetisha