Unajua Mungu aliumbwa na nani?

ushuhuda kidogo tafadhali ilikutokea nini..
Mambo mengine niyakukaa kimya tu kama mtu anachakuongea
Sio kilakitu mtu anaweza ku expose kwa kila mtu hasa mtandaoni ila usichokijua ni usiku wa kiza maan uchawi upo na kama uchawi upo basi na Mungu yupo
Nashaa anajibu comment za wengin kam vle aon zang
 
Nakuchapa kwa aya tuu!

Bado kofi lenye maelekezo ya kashifa juu ya mola wako! Wewe si unajua tukana mamba angali kuvuka mto bado, Na usubiri habari yako baladhuri mjaa laana wewe!
Unafanya personal attack.

Hoja zimekushinda kujibu?
 
Unafanya personal attack.

Hoja zimekushinda kujibu?
Na hapana mnyama katika ardhi, wala ndege anaye ruka kwa mbawa zake mbili, ila ni umma kama nyinyi. Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote. Kisha kwa Mola wao Mlezi watakusanywa.
 
Boss Sayansi itaendelea kufanya kazi yake na wenye imani tutaendelea kuwa na imani.

Imani ya uwepo wa MUNGU ni matumaini pale ambapo hakuna majibu, ulinzi pale pasipo na ulinzi, sheria pale pasipo na sheria.

Ghafla bin Vuu watu wafute imani ya MUNGU ndani yao dunia itakuwa ya aina gani? Ushakutana na binadamu wasiomfahamu MUNGU wanavyofanana?

Unadhani sheria pekeyake zinatosha kuudhibiti unyama wa binadamu? MUNGU pekee ndiye anayesababisha stability duniani, tukimkataa na kumkana mawazoni petu katika nyakati hizi tutakuwa na kizazi ambacho hakina stability.

Huko maporini ambapo sheria haina macho watu watachinja wamama wajawazito ili wapate moyo wa kichanga kama kitoweo, viongozi walio juu ya sheria hawatakuwa na hofu yoyote na mengine mengi sana ambayo nina hakika dunia ya sasa esp huku Afrika hatutamani kuyashuhudia.

Imani ya uwepo wake ni muhimu sana kwetu binadamu. Yatupasa tuamini uwepo wa MUNGU nyakati zote na kumuabudu katika roho na kweli ila tuwe na kiasi, tusiwe wajinga na pale sayansi inapofanya sehemu yake turuhusu mawazo mbadala katika akili zetu.
 
Nlikua sijaona post yako.

Una uthibitisho wa uwepo wa mungu?
 
Nakazia . Ukweli kuhusu Mungu huuwezi kuupata kwenye vitabu tulivyo letewa. Ukitaka kumjua Mungu nitazame mwili wako itazame nature.
 
Reactions: Tsh
Hapa ubishi upo kwenye Nguvu inayo endesha dunia kuitwa jina "Mungu" naona hapa ndio mleta mada anapinga.

Nguvu iliyo anzisha dunia na vyote vilivyomo ndani yake ipo.

Lakini swali na utata unakuja kwa hapa:
Kwa nini hii "Nguvu" ili itwa na kupewa jina Mungu?

Aliyeipa na kuiita hii Nguvu jina "Mungu" ni nani???

Lakini mimi naamini Dunia ilianzishwa na NGUVU fulani na hiyo nguvu ndio ina control kila kitu....Lakini linapokuja swala la hii nguvu kuitwa jina "Mungu" ndio ubishi huanza hapa, Kwa nini iwe jina Mungu na sio jina lingine??.

Kwa hiyo kila mtu (Binadamu) ana namna ya kuamini hii nguvu ki namna yake.wengine huita Mungu, wengine wana amini Sayansi ndio nguvu yenyewe, wengine mizimu/wachawi ndio nguvu yenyewe.. Wengine wana amini kuna nguvu tu ila haina jina...nameless...
 
Sema: Mwaonaje Mwenyezi Mungu akanyakua kusikia kwenu, na kuona kwenu, na akaziziba nyoyo zenu, ni mungu gani asiye kuwa Mwenyezi Mungu ataye kuleteeni hayo tena? Angalia vipi tunavyo zieleza Ishara, kisha wao wanapuuza.
 
Sawa tuanze taratibu.
Laana ni nini?
Mabalaa yapi unayazungumzia?

Kwanini vipimo vya daktari kutoona ugonjwa kufanye ugonjwa huo uwe wa kichawi?

Unatambua kuwa yanaweza kuibuka magonjwa mapya ambayo hatujayajua kabla?

Laana ni mkusanyiko wa mabaya yote yanayompata mtu: misukosuko katika kazi au ndoa n.k. laana huleta mateso mengi.

Kuachika hovyo, je unafahamu ya kwamba unaweza ukaoana au shirikiana na mtu mwenye mikosi ukashangaa mambo hayaendi au ukishiriki mapenzi na mtu fulani mambo yanaenda.
Thus nimekwambia kuna magonjwa ya kiroho na magonjwa ya kihospitali, kuna tiba za hospital na tiba za kiroho yaani waganga na watumishi wa MUNGU au watu waliopewa karama za uponyaji.

Kama mtu anateseka kwa tatizo na uonekana kimwili lakini wanapima vipimo vyote vya kisayansi tena mitambo ya kisasa kabisa havionyeshi tatizo, kwann isilete shaka. Then mtu huyo akaenda kupata tiba za kiroho nje ya sayansi na akawa mzima kabisa kwann tusiamini kwamba zipo elimu zingine nje ya sayansi.
 
Nakaxia . Ukweli kuhusu Mungu huuwezi kuupata kwenye vitabu tulivyo letewa. Ukitaka kumjua Mungu nitazame mwili wako itazame nature.
Nakazia. kama huna imani ya uwepo wa MUNGU na hujui asili ya ulimwengu na asili yako basi una tatizo la akili.
 
Sema: Mwaonaje, ikikufikieni adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa ghafla, au kwa dhaahiri?
 
Mkuu unaweza thibitisha kuwa umeumbwa na Mungu? AU kwasababu hujui umetokana na nini basi wewe umeamua kusema ni Mungu baada ya kukosa jibu!
Ungekuwa umejileta mwenyewe duniani ungekuwa sahihi kusema kuwa hakuna Mungu.
 
Nlikua sijaona post yako.

Una uthibitisho wa uwepo wa mungu?
Atathibitisha kwa kukupa nn zaidi ya hayo yanayokuzunguka? Ww kwann usimthibitishie kuwa imani yake kwa MUNGU ni batili kwa kumpa sababu ya anayoyaona?

HIVI KWANN MNAKAZANA SANA WATU WASIAMINI KUHUSU MUNGU? KUNA MADHARA GANI IWAPO WANAAMINI NA HAYUPO? MNAUTAMANI ULIMWENGU USIO NA HOFU YA MUNGU MTAUMUDU?
 
Nimekuelewa.
Kwanza kabisa sijasema kuwa imani ya uwepo wa mungu haina umuhimu. Ina faida kama hizo ulizozitaja hapo juu na ndio lengo hasa LA hizo imani.

Lakini je hata sasa ambapo watu wanaamini imani hiyo, watu hawachinjani?, ubakaji haupo, viongozi miungu watu hawapo?

Point yangu ni kuwa sio lazima tung'ang'anie imani hizi ili kuwa na amani kwenye jamii.
Yawezekana kukawa na amani zaidi kusipokuwa na imani hizi.
 
Reactions: Tsh

Uzi ufunge kabisa umemaliza kila kitu, sitaki kuongezea Neno
 
Boss, binadamu tuna historia, umezaliwa ukakutana na ibada sababu hapo nyuma kuna sababu ilipelekea ibada zikawepo. Tusibishane na nyakati, nyakati za majibu zitafika ila kwa sasa salama yetu ni tulio wengi kuwa na hofu ya MUNGU.

Hayo matukio yanatokea sasa katikati ya uwepo wa MUNGU na sheria za binadamu, imagine MUNGU hayupo yatafanana vipi.
 
Bange za utotoni
 
Hakika miongoni mwa Watu wa Kitabu wapo wanao muamini Mwenyezi Mungu na yaliyo teremshwa kwenu na yaliyo teremshwa kwao, wakimnyenyekea Mwenyezi Mungu. Hawabadili Aya za Mwenyezi Mungu kwa thamani duni. Hao wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.
 
Nakazia hapa. Mbuyu na uheshimiwe, ifike kipindi watu waone huruma ya makalio yao. Yanatikiswa sana kwa kupambana na mbuyu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…