BodGanleonid
JF-Expert Member
- Nov 14, 2022
- 3,021
- 4,330
Bali ni uthibitisho wa uwepo wa nani?? Kujifunga unajifunga mwenyewe na kujifungua huweziKushindwa kujua binadamu katokana na nini siyo uthibitishe wa uwepo wa Mungu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bali ni uthibitisho wa uwepo wa nani?? Kujifunga unajifunga mwenyewe na kujifungua huweziKushindwa kujua binadamu katokana na nini siyo uthibitishe wa uwepo wa Mungu
Mambo mengine niyakukaa kimya tu kama mtu anachakuongeaushuhuda kidogo tafadhali ilikutokea nini..
Unafanya personal attack.Nakuchapa kwa aya tuu!
Bado kofi lenye maelekezo ya kashifa juu ya mola wako! Wewe si unajua tukana mamba angali kuvuka mto bado, Na usubiri habari yako baladhuri mjaa laana wewe!
Na hapana mnyama katika ardhi, wala ndege anaye ruka kwa mbawa zake mbili, ila ni umma kama nyinyi. Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote. Kisha kwa Mola wao Mlezi watakusanywa.Unafanya personal attack.
Hoja zimekushinda kujibu?
Boss Sayansi itaendelea kufanya kazi yake na wenye imani tutaendelea kuwa na imani.Mkuu
Unajua kuwa unazidi kuthibisha madai yangu kwamba imani hizi zinasababishwa na uvivu wa kufikiri?
Daktari akishindwa kutibu ugonjwa tunakimbilia kusema ni uchawi au majini bila ya kujishughulisha kutafuta kujua tatizo ni nini ambapo inawezekana linaelezeka kibaiologia katika namna ambayo sisi hatujaielewa bado.
Umesema sayansi imeshindwa kutoa majibu kuhusu chanzo cha uhai. Ni kweli ,sayansi haijaelezea kila kitu lakini kwa nini hiyo isiwe chachu ya sisi kushughulisha akili zetu kufanya uchunguzi ili tupate majibu mazuri zaidi yasiyo na utata na yanayothibitishika na badala yake tunajitungia majibu mepesi yasiyothibitishika na yenye utata?
Unasema sayansi imeshindwa kuelezea laana, maisha baada ya kifo mikosi n.k
kwanza kabisa sayansi sio tu imeshindwa kuvielezea, hata haijathibitisha kama vipo. Ni dhana za kifikirika zaidi hivyo haviwezi kuthibitishika hivyo haziwezi kuelezeka.
Nlikua sijaona post yako.Mambo mengine niyakukaa kimya tu kama mtu anachakuongea
Sio kilakitu mtu anaweza ku expose kwa kila mtu hasa mtandaoni ila usichokijua ni usiku wa kiza maan uchawi upo na kama uchawi upo basi na Mungu yupo
Nashaa anajibu comment za wengin kam vle aon zang
Nakazia . Ukweli kuhusu Mungu huuwezi kuupata kwenye vitabu tulivyo letewa. Ukitaka kumjua Mungu nitazame mwili wako itazame nature.Kijana unatikisa mbuyu umejikuta unatikisa makalio yako mwenyewe.
Hata kama huamini achana na hilo DUDE linaloitwa MUNGU. Lipo nje ya uwezo wako kulielewa.
tafuta muda wa peke yako, uyaangalie mazingira yako milima na mabonde, nyota angani, wanyama, samaki, wadudu, ndege, n.k (angalia usiku na muda wa mchana)
Utaanza taratibu kugundua kuwa kumuamini MUNGU inahitaji kuuvua huo ujuaji wako.
tuliza akili kijana!
Sawa tuanze taratibu.
Laana ni nini?
Mabalaa yapi unayazungumzia?
Kwanini vipimo vya daktari kutoona ugonjwa kufanye ugonjwa huo uwe wa kichawi?
Unatambua kuwa yanaweza kuibuka magonjwa mapya ambayo hatujayajua kabla?
Nakazia. kama huna imani ya uwepo wa MUNGU na hujui asili ya ulimwengu na asili yako basi una tatizo la akili.Nakaxia . Ukweli kuhusu Mungu huuwezi kuupata kwenye vitabu tulivyo letewa. Ukitaka kumjua Mungu nitazame mwili wako itazame nature.
Ungekuwa umejileta mwenyewe duniani ungekuwa sahihi kusema kuwa hakuna Mungu.Mkuu unaweza thibitisha kuwa umeumbwa na Mungu? AU kwasababu hujui umetokana na nini basi wewe umeamua kusema ni Mungu baada ya kukosa jibu!
Atathibitisha kwa kukupa nn zaidi ya hayo yanayokuzunguka? Ww kwann usimthibitishie kuwa imani yake kwa MUNGU ni batili kwa kumpa sababu ya anayoyaona?Nlikua sijaona post yako.
Una uthibitisho wa uwepo wa mungu?
Nimekuelewa.Boss Sayansi itaendelea kufanya kazi yake na wenye imani tutaendelea kuwa na imani.
Imani ya uwepo wa MUNGU ni matumaini pale ambapo hakuna majibu, ulinzi pale pasipo na ulinzi, sheria pale pasipo na sheria.
Ghafla bin Vuu watu wafute imani ya MUNGU ndani yao dunia itakuwa ya aina gani? Ushakutana na binadamu wasiomfahamu MUNGU wanavyofanana?
Unadhani sheria pekeyake zinatosha kuudhibiti unyama wa binadamu? MUNGU pekee ndiye anayesababisha stability duniani, tukimkataa na kumkana mawazoni petu katika nyakati hizi tutakuwa na kizazi ambacho hakina stability.
Huko maporini ambapo sheria haina macho watu watachinja wamama wajawazito ili wapate moyo wa kichanga kama kitoweo, viongozi walio juu ya sheria hawatakuwa na hofu yoyote na mengine mengi sana ambayo nina hakika dunia ya sasa esp huku Afrika hatutamani kuyashuhudia.
Imani ya uwepo wake ni muhimu sana kwetu binadamu. Yatupasa tuamini uwepo wa MUNGU nyakati zote na kumuabudu katika roho na kweli ila tuwe na kiasi, tusiwe wajinga na pale sayansi inapofanya sehemu yake turuhusu mawazo mbadala katika akili zetu.
Kijana unatikisa mbuyu umejikuta unatikisa makalio yako mwenyewe.
Hata kama huamini achana na hilo DUDE linaloitwa MUNGU. Lipo nje ya uwezo wako kulielewa.
tafuta muda wa peke yako, uyaangalie mazingira yako milima na mabonde, nyota angani, wanyama, samaki, wadudu, ndege, n.k (angalia usiku na muda wa mchana)
Utaanza taratibu kugundua kuwa kumuamini MUNGU inahitaji kuuvua huo ujuaji wako.
tuliza akili kijana!
Boss, binadamu tuna historia, umezaliwa ukakutana na ibada sababu hapo nyuma kuna sababu ilipelekea ibada zikawepo. Tusibishane na nyakati, nyakati za majibu zitafika ila kwa sasa salama yetu ni tulio wengi kuwa na hofu ya MUNGU.Nimekuelewa.
Kwanza kabisa sijasema kuwa imani ya uwepo wa mungu haina umuhimu. Ina faida kama hizo ulizozitaja hapo juu na ndio lengo hasa LA hizo imani.
Lakini je hata sasa ambapo watu wanaamini imani hiyo, watu hawachinjani?, ubakaji haupo, viongozi miungu watu hawapo?
Point yangu ni kuwa sio lazima tung'ang'anie imani hizi ili kuwa na amani kwenye jamii.
Yawezekana kukawa na amani zaidi kusipokuwa na imani hizi.
Bange za utotoniMimi ni kijana ambaye Kwa muda wa miaka 2 nimekuwa nikifatilia mijadala mbalimbali hapa Jf katika jukwaa hili la intelligence. Moja ya mijadala ambayo imekuwa ikinivutia sana ni hii ya dhana ya uwepo wa Mungu.
Swali kubwa ambalo nimeku wa nikijiuliza ni " Mungu alitoka wapi"
Baada ya kuisoma sana biblia na Quran pamoja na kuwahoji viongozi mbalimbali wa dini, hatimaye nikapata jibu la swali lililonitatiza muda mrefu, Mungu alitoka wapi?
Nimegundua kuwa muumba wa Mungu ni mwanadamu. Yes mwanadamu kama Mimi na wewe ndiye aliyemuumba Mungu.
Kwanini nimefikia hitimisho hilo?
Vitabu tunavyoaminishwa kuwa ni vya Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu ( biblia & Quran) ni vitabu vyenye makosa mengi sana ya kimantiki na habari nyingi zenye utata, jambo ambalo tusingetegemea liwepo katika kitabu kilichoandikwa kwa muongozo kutoka kwa Mungu mkuu mwenye uwezo asiyeshindwa na kitu.
Uwepo wa habari hizo zenye utata zinadhihirisha moja kati ya mambo yafuatayo.
1. Mungu hana ukuu tunaoambiwa ndio sababu ameshindwa kutoa mwongonzo mzuri katika kuandika kitabu kisicho na makosa ya kimatinki.
2. Habari hizi ni zao la fikra za mwanadamu aliyeishi katika zama za giza na ujinga. Mwanadamu ambae alitaka kutafuta majibu mepesi katika maswali magumu yaliyomzunguka ndio sababu zina utata.
Kama jibu ni 1 basi Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu hayupo Bali aliyepo ni dhaifu na mbabaishaji aliyeshindwa kuandika vizuri kitabu kinachomuelezea yeye mwenyewe.
Kama jibu ni 2 ,basi Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu hayupo ndiyo sababu akatokea mtu akatunga habari kutokana na fikra zake mwenyewe. Angekuepo asingeruhusu magepu katika fikra za mwanadamu ambayo yamepelekea mwanadamu huyo kujitungia majibu mepesi na habari zenye utata ili kuziba hayo magepu katika fikra zake.
Pointi zote mbili utaona zinaonyesha kuwa Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu mjuzi wa yote hayupo Bali " ama aliyepo ni dhaifu,mbabaishaji na asiye na uelewa wowote kuhusu ulimwengu, ama dhana nzima ni hadithi ya kutungwa katika fikra za mwanadamu aliyeishi katika zama za ujinga na kukosa access ya taarifa mbalimbali.
Nawasilisha.
Nakazia hapa. Mbuyu na uheshimiwe, ifike kipindi watu waone huruma ya makalio yao. Yanatikiswa sana kwa kupambana na mbuyu.Kijana unatikisa mbuyu umejikuta unatikisa makalio yako mwenyewe.
Hata kama huamini achana na hilo DUDE linaloitwa MUNGU. Lipo nje ya uwezo wako kulielewa.
tafuta muda wa peke yako, uyaangalie mazingira yako milima na mabonde, nyota angani, wanyama, samaki, wadudu, ndege, n.k (angalia usiku na muda wa mchana)
Utaanza taratibu kugundua kuwa kumuamini MUNGU inahitaji kuuvua huo ujuaji wako.
tuliza akili kijana!