Unajua Mungu aliumbwa na nani?

Kwanini iwe ni lazima kujua majibu ya ulimwengu na kifo ili kuipinga dhana ya uwepo wa Mungu?

Unajua kuwa tunaweza kujua uongo wa kitu bila kujua ukweli halisi ni upi?




Thibitisha kwamba unaweza kujua uongo wa kitu bila kujua ukweli halisi.
 
Jua lina miaka mingapi? na je? Unaweza kuthibitisha kwamba jua litakuwa na mwisho pia?
 
Be still and know that I AM GOD!

Kama hujatulia kutafakari unaweza kusema chochote! Utakapotulia na kufanya tafakuri utajua ya kuwa yeye ni Mungu
 
Sasa kama hamjajua, kwanini mmehitimisha??
Kwa sababu hakuna hitimisho mbadala. Ww ukikuta chungu porini na huoni aliyekileta pale utahitimisha kuwa binadamu alikuwepo pale porini, ili useme sio binadamu kaleta inabidi ulete hitimisho mbadala lisilo na shaka la sababu ya uwepo wa chungu porini.

Na sisi hivyo hivyo tumeukuta Ulimwengu tunaamini kuna inteligent behind tuliyoyakuta na hiyo inteligent ni MUNGU. Sasa kama ww unajua hakuna inteligent inayoitwa MUNGU toa majibu ya uwepo wa ulimwengu yasiyo na shaka kinyume na hapo ni sawa na mlevi anashindana na sura yake kwenye kioo kuwa nani ana ulimi mrefu. Hatopatikana mshindi na anapoteza muda tu.
 
Unatumia uongo mmoja kuelezea uongo mwingine.

Macho ya rohoni ni yapi?
 
Kwaiyo wazungu wana nafuu kidogo kwenye kufata dini ndio maana wakabarikiwa kuliko sisi?
Asili ya maendeleo yao imetoka na Ukristo ndio uliwapa elimu na ustaarabu.
Hakuna maendeleo pasipo ustaarabu.Mtu aliyestarabika na mwenye hofu ya Mungu hawezi kuwa fisadi kwa kuiba kodi za wananchi na kwenda kununua mabus au kudhamini timu ya mpira huku maelf wakifa njaa,wakikosa huduma muhimu.

Mtu mwenye dini utanguliza maslai ya wengine kabla yake, mtu mwenye dini ulijenga taifa lake na sio tumbo lake.
 
Huo mfano wa chungu na Mungu vinaendana kweli?
Atleast Chungu tunajua kimetengenezwa na binadamu..pamoja na kuwa kinaweza kupelekwa na mto porini.

Lakini Mungu hata hatuna uhakika kama yupo achilia mbali kama aliumba ulimwengu.
 


Ingekutosha kama Mungu angekuumba Nyani.
 
Thibitisha kwamba unaweza kujua uongo wa kitu bila kujua ukweli halisi.
Ukiniambia 234 × 457= 12 nitajua ni uongo hata kama sijui jibu la moja kwa moja la 234×457 ni ngapi.

Kwasababu ya kanuni ya muhimu kabisa kwamba kwenye hesabu za kuzidisha namba nzima, jawabu lazima Liwe kubwa kuzidi namba zilizotumika kuzidishwa. Hapo jibu ni dogo kuliko namba Za awali hivyo sihitaji kujua jibu halisi la 234×457 ni ngapi ili kujua kuwa jibu la 12 ni uongo
 
Hakuna hakika kuwa mungu yupo.
 
Zab 53:1 Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu

Ukiona tuu huamini katika uwepo wa Mungu basi mtari huu unakuhusu .
 
Hakuna mungu, ndio maana ukiwahoji maswali wanakutisha.

Mungu ni mchongo wa upigaji ulioletwa kutudumaza akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…