Unajua Mungu aliumbwa na nani?

Unajua Mungu aliumbwa na nani?

Huwa nacheka sana hoja za Wakana Mungu,
Wapi nimekana Mungu??? Nani kakuambia mimi ni mkana Mungu??
Mimi sio mkana Mungu mkuu
kitu ambacho wakana Mungu hamkijui ni kuwa hamjijui kama hamjui yaani nyinyi ni Wapumbavu, huku mkijiona mnajua.
Wapi nimesema najua??? Kwanza kitendo cha wewe kuniita mpumbavu nisiyejua, tayari kimeashiria wewe sio mpumbavu na unayejua...sasa kwanini unitukane mimi kuwa najiona najua huku wewe mwenyewe kwa kusema hivyo tu, tayari umeojiona kuwa wewe ndo unajua??
Umeuliza swali rahisi sana kwanini ni "Nani ?" na si "Nini ?" hili hata wenzako waliuliza sisi tukawajibu hivi nini hakina uwezo wa kusanifu wala Hakika ila nani ana uwezo wa kisanifu na anajua, ana Elimu, ana hekima na ni mkamilifu. Yaani kwa ufupi "Nani" ni dhamiri inayo kwe chenye akili, maarifa na kujua, ila nini ni dhamiri ya swali kwa kisichokuwa na akili, kisichojua, kisichokuwa na malengo.
Upepo unavuma na kusababisha miti kuanguka, Hapo mtu akiuliza nani kaangusha mti atakuwa sahihi?? Sio kila kitu kinakuwa caused na kitu chenye akili.
DNA haina akili lakini inacode kila kitu kwenye kiumbe.
Mimi najua na ninaweza kithibitisha kwa kutumia akili, mazingira na ufunuo.
Sawa, Karibu uthibitishe.
 
biblia & Quran) ni vitabu vyenye makosa mengi sana ya kimantiki na habari nyingi

Ukisha jibidisha kutafuata ukweli kwa kurejea vitabu hivyo vya kiimani pekee unakuwa umejifungia ndani ya box la kitafakuri finyu.

Hongera kwa kuwa na shaka hivyo unatafuta maarifa mapana nje ya box ikiwemo kujadiliana hapa JF, kusoma vitabu visivyo vya kiimani ili kutafuta elimu pana zaidi ikiwemo vya sayansi, biolojia, fizikia, elimu anga n.k
 
Huwa nacheka sana hoja za Wakana Mungu, kitu ambacho wakana Mungu hamkijui ni kuwa hamjijui kama hamjui yaani nyinyi ni Wapumbavu, huku mkijiona mnajua.

Umeuliza swali rahisi sana kwanini ni "Nani ?" na si "Nini ?" hili hata wenzako waliuliza sisi tukawajibu hivi nini hakina uwezo wa kusanifu wala Hakika ila nani ana uwezo wa kisanifu na anajua, ana Elimu, ana hekima na ni mkamilifu. Yaani kwa ufupi "Nani" ni dhamiri inayo kwe chenye akili, maarifa na kujua, ila nini ni dhamiri ya swali kwa kisichokuwa na akili, kisichojua, kisichokuwa na malengo.

Mimi najua na ninaweza kithibitisha kwa kutumia akili, mazingira na ufunuo.
Thibitisha
 
Ulimwengu usioonekana upoje?
Usioonekana kwa macho ya nyama yaani ndani ya ulimwengu huu kuna ulimwengu mwingine maisha yanaendelea Ili kuuona hata kuungia ni lazima uwe na macho ya rohoni.

Pale kigamboni ferry mkono wa kulia zinapopaki boti za uvuvi kuelekea chuo cha Mwalimu Nyerere kuna mlango wa kuingia ulimwengu mwingine, pembeni Mwa ghorofa la bandarini baharini kuna mlango wa kuingia ulimwengu mwingine, kwa macho ya kawaida huwezi ona.

Viumbe vyenye uwezo wa kuona ulimwengu usioonekana ni watoto wadogo ambao awajaanza kuongea, vichaa, bubu, wachawi, waganga, watumishi original wa MUNGU,wanyama mfano mbwa, paka,nk
 
Nataka nikuonyeshe uongo wa hili zingatio lako kwa kuuliza maswali haya :

1. Ni lini mwanadamu alianza kumuongelea Mungu ? Na ni kina na I wa mwanzo katika hilo ?

2. Je sasa hivi wamejua ulimwengu ni nini ? Je wametumia nyenzo gani kujua hilo ?
Jibu 1. Binadamu anayeamini mungu yupi? Historia ya MUNGU ni tofauti tofauti kulingana na imani za binadamu.

Kuna ambaye anamuongelea MUNGU wa biblia na Quran, yupo anayeongelea mizimu, ng'ombe n.k. Sasa unataka kujua walioanza kumuongelea yupi?

Jibu 2. Hatujajua ndo maana bado tumehitimisha yote katika concept ya lazima kuna chanzo cha haya yaliyopo, hicho chanzo ndiye MUNGU. Kama ww una ukweli ulio na uhalisia badala ya kiimani zaidi ya huu tulionao uweke wazi.
 
Al-Kahf 18:109

قُل لَّوْ كَانَ ٱلْبَحْرُ مِدَادًا لِّكَلِمَٰتِ رَبِّى لَنَفِدَ ٱلْبَحْرُ قَبْلَ أَن تَنفَدَ كَلِمَٰتُ رَبِّى وَلَوْ جِئْنَا بِمِثْلِهِۦ مَدَدًا

Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani

Sema: Lau kuwa bahari ndio wino kwa maneno ya Mola wangu Mlezi, basi bahari ingeli malizika kabla ya kumalizika maneno ya Mola wangu Mlezi, hata tungeli ileta mfano wa hiyo kuongezea.

English - Sahih International

Say, "If the sea were ink for [writing] the words[1] of my Lord, the sea would be exhausted before the words of my Lord were exhausted, even if We brought the like of it in [continual] supplement."
 
Nani Ina maarifa, Ina sanifu, Ina jua, Ina malengo.

Vipi kuhusu "Nini ?" Ina nini ? Unaweza kunipa mfano wa nini ? Na ukamiambia kwanini isiwe "Nani ?"
Wapi nimesema ni " nini"?
Kwanini unadhani lazima ' nani' mwenye maarifa ndio asababishe uhai na so michakato tu ya kisayansi ambayo haijagundulika?
 
Mungu hakutaka kuweka maneno meengi kwenye vitabu vyake vitukufu. Aliweka maneno machache ambayo kwa mwenye akili akisoma tu basi humuongezea imani ila kwa wapotovu huzidi kuwaongezea upotovu.
 
Mleta mada umesoma Replies za bwana Kiranga ,Scars kuhusu kutokuwepo kwa Mungu ukapata Uzi....[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Je hayo matendo ni maamrisho ya dini?
Je wazungu wote wanafanya na kusapoti uliyoyataja.
Walitutenda mabaya kwa maagizo ya dini?
Hata hayo uliyosema ya waafrika kwamba ya ulafi, uvivu n.k sio waafrika wote wanayafanya na kuyasapoti
 
Jibu 2. Hatujajua ndo maana bado tumehitimisha yote katika concept ya lazima kuna chanzo cha haya yaliyopo, hicho chanzo ndiye MUNGU. Kama ww una ukweli ulio na uhalisia badala ya kiimani zaidi ya huu tulionao uweke wazi.
Sasa kama hamjajua, kwanini mmehitimisha??
 
Mungu angeamua kuelezea ishara yake moja tu kwenye hivi vitabu vyake vya taurat,zaburi ,injili na Quran basi ingemchukua mwanadamu zaidi ya umri wake kusoma na pengine pia asingealiza na kuelewa kila kitu.
 
Vipi kuhusu watu wanaozaliwa vipofu macho yao hayawezi kutazama na kutofautisha rangi ?

Je hao wana kosa gani? Ama kwa sababu gani wameumbwa hawajakamilika kama wenzao
Hivi wewe na billgates mna tofauti gani? Kimaumbile ? Na kwanini wewe si bilionea kama yeye wewe una makosa gani yeye akakuzidi?
 
Ni maneno ya Mungu kwa kuyatafakari tu na jinsi yalivyoshusha sio kawaida ,yamejaa hekima.
Hujathibitisha, ume assume kuwa kwa kuwa yana hekima basi ni ya Mungu.

Kuna quotes nyingi tu za wanadamu zenye hekima.
 
Back
Top Bottom