Unajua stori ya mtu ambaye alipotea tu ghafla na hajulikani kama yuko hai au amekufa?

Unajua stori ya mtu ambaye alipotea tu ghafla na hajulikani kama yuko hai au amekufa?

Nimetoka kuangalia habari kwenye chanel ya Millard ayo, kuna mtu kafukuliwa kwenye nyumba ya mtu, maisha haya tulipofikia tuombe tu neema za mwenyezi Mungu
Inatisha mno, tuombeane tu 🙏
 
Bibi yangu aliondoka nyumbani kaacha ATM cards na passwords zake, mpaka leo ni miaka tele hajaonekana tena.
 
Kaka yake Mama alipotelea Zambia,hatujui ni mzima au amekufa....huyu mjomba kwa story za mama ambaye alikuwa wa mwisho kwao, siku alipoenda kumuandikisha shule ya msingi mwaka 1964 ndiyo siku aliondoka kwenda kutafuta maisha, mama hajawai kumuona tena mpaka leo.

Shangazi yetu aliondoka inasemekana miaka ya 1970 nyumbani kwenda Tanga,kwa story za Mama shangazi yetu huyo Dada yake Baba, mara ya mwisho aliwasiliana na mama kwa njia ya barua mwaka 1986, mpaka leo hatujui kama yupo hai au alikufa
Daaah poleni 💔 💔 muda mrefu sana umepita.
Natumai hakuna baya lililowafika 😞
 
Bibi yangu aliondoka nyumbani kaacha ATM cards na passwords zake, mpaka leo ni miaka tele hajaonekana tena.
Inaonekana alidhamiria kuondoka 💔 kulikua na migogoro au matatizo ya familia.
Au aliondoka ghafla tu bila sababu?
 
Daaah hiyo ni aina ya investigative journalism ambayo bongo hatuna kabisa, waandishi wetu ni kama hao akina "Manara Tv" sasa huo uchimbuaji na ufuatiliaji wa kiundani hivyo watauweza wapi.
Ni kweli kabisa
Kina Ayo hao

Ila inataka funds kubwa, na sisi utaratibu wa kukusanya hela za hivyo hatuna kabisa

Wenzetu kufika hapo walipo sio kwa bahati bali wamepambana kwa hali na mali.

Wananchi wanatoa sana na kila duka unakuta wameweka makopo ya kusaidia maisha ya kila siku

Yaani ukiwaona wanavyoishi kwa kusaidiana ndio utajua kuna mambo mengi serikali haina mkono ila kiasi tu
 
Umesema sahihi kabisa 🙌
 
Back
Top Bottom