Unakosea, Unakosea na nasema tena Unakosea wenye Akili hawashindani na 'System' Kibwege (Kipumbavu) hivi..shauri yako!!

Gwajima alimshambulia Rais hadharani kwa kusema asiwatumbue wateule wake wa vyombo vya ulinzi hadi bunge liamue. Angeongelea tu utekaji na kuzitaka mamlaka zishughulikie isingeleta shida. Tatizo ni mashambulizi yake kwa Rais
 
Mandela hakufanya lolote.... CIA iliamua kumaliza utawala wa makaburu kutokana na uelekeo wa siasa za wakati huo na sio kwamba kulikuwa na shinikizo lolote la Mandela. Hata Mandela alikabidhiwa nchi kwa masharti mengi... someni historia vijana.
Wewe siwezi kubishana na wewe kwanza unatawaliwa na mke wako
 
Kosa la Gwajima ni nini kwani??Je! Katenda jinai, katibua katiba??Kwa alichokifanya Gwajina kwa system safi isiyo na uovu wala hakuna tatizo lolote.
Gwajina press nzima kawatetea, polisi, CCM, Rais, usalama n.k anasema kuna kikundi, sasa hapo kaenda against system ipi???

Watu wote hatuna vipaji sawa na uthubutu kama wengine ni waoga tusiwakatishe tamaa wanaoenda front- lazima mmoja au wachache waende mbele -wengi wa hao wachache hufa, na wachache huishi kushuhudia wanachokipigania.
 
Nafikiri ungeenda mbali na kuja na suluhusho katika nyakati kama hizi
Lengo lao muogope, mkae kimya, hata wakija kubeba mkeo wala usiwaulize je busara ni nini kwa nyakati kama hizi?
Eti hizi ndo busara/hekima anazomaanisha mwandishi.
Ujinga gani huu!
 
Gwajima alimshambulia Rais hadharani kwa kusema asiwatumbue wateule wake wa vyombo vya ulinzi hadi bunge liamue. Angeongelea tu utekaji na kuzitaka mamlaka zishughulikie isingeleta shida. Tatizo ni mashambulizi yake kwa Rais
Nilitamani sana tuangalie hoja yake yeye alikuwa na wasiwasi inakuwaje ndani ya miaka mitatu tunabadilisha wakuu wa chombo cha usalama mpaka wanne, je wana matatizo gani kumbuka mpaka ufikie hatua ya kuteuliwa unakuwa umepitia vetting kubwa sana na hiyo haifanywi na mtu mmoja rais yeye anamtangaza tu baada ya vyombo vinavyohusika kujiridhisha kuwa anafaa kutumikia nafasi hiyo. Sasa inapokuja wanatolewa kila mara inawezekana kweli kukawa na kuto comply kwa matakwa ya kiongozi anayeteua huenda mkuu wa hicho chombo amekataa au ameshauri jambo fulani lisifanyike kwa namna ambayo mkuu wa nchi anapendekeza.
Mimi nadhani hakuna aliyeshambuliwa yeye ametoa tu mapendekezo ni aidha serikali ilitakiwa iyachukue au iachane nayo.

Yaani kwa hiki kinachofanyika kwasasakinadhihirisha kabisa kuna kikundi ambacho kinateka na kuua kwa maslahi ya watawala na hakiguswi na inaonekana kina haki ya kuua raia yoyote kinayeona anafaakutangulizwa mbele ya haki na ndiyo maana yeyote anayekisema vibaya hicho kikundi atashughulikiwa.

Rais wetu ameshindwa kutulinda au huenda anatuma watu tuzidi kuuawa hasa sisi maskini tusio na ndugu yeyote aliyeko madarakani.
 
Uko sawa,
Alikuwa na pointi ila uwakilishaji wake haukuwa planned. Kwa sasa kwa binadamu mwenye utashi lazima anafadhaika.

Hii siyo vita ya kawaida, imepitiliza.
 
Hizi huwa ni Mentality za KIPÚMBAVU sana...... kwanini mnatetea watu wote tuwe MAKONDOO?
Kwahiyo busara kwako ni watu wote tukae kimya na kusifia ujinga unaoendelea?

Kila mtu anajua duniani kote vita dhidi ya watawala dhalimu haijawahi kuwa vita RAHISI hata siku mmoja

Hakuna utawala dhalimu utakao dumu milele duniani...... hata huu utaanguka tu na sababu ni hawa hawa unaotaka wakae kimya as if nothing happened.
Yes serikali inaweza kumuua Gwaji kama ilivyo muua Ben na wengine..... lakini serikali haiwezi kuua idea wanayotaka raia, ndio maana wamemuua Ben kaja Mdude na wataendelea kuibuka kila uchwao hadi takwa litakapo timia....... this is just a process tukiikwepa hii tutazalisha taifa la MAKONDOO daima

Kama mimi na wewe ni waoga acha wenye ujasiri wa kufanya hivyo bila kuogopa watakayo pitia wafanye hivyo..... ndio wito wao na ndio njia ya ukombozi
 
Gwaji Boy kuna muda nahisi Ana kundi kubwa nyuma yake, ni kama wana Ajenda flani.

Ila wanaweza kumjaza upepo kisha akajikuta amebaki pake yake.
 
Tuseme system ndio dola, sawa, ni madola mangapi yalianguka kibwege huku yakiwa na nguvu nyingi? Ni watawala wangapi waliishia vibaya na wengine kufa vifo vya kinyonge huku walikuwa na nguvu nyingi? Umafia si hoja kwamba always serikali huwa na nguvu. Kuna wakati nguvu za dola huyeyuka kama barafu kwenye joto kali automatically. Dola inapokuwa na kiburi na majivuno anguko lake huwa ni kubwa na la kushangaza
 
Tuna mwaka wa 10 sasa hiyo system INATEKA watu tangu enzi za Ben Saanane na Azory Gwanda.

Imetatua tatizo gani?

Kila siku ndio wapiga kelele wanaongezeka
 
Sijaelewa?Amekosea kusema kuna watu wanatekwa au ksema kuna watu wanauawa na hakuna hatua zozte zinachukuliwa.? Chakujadili hapa ni je anachosema ni kweli au upotoshaji?
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…