Nakuonea sana Huruma japo Wanafiki na Wasiojua mambo ya Kimtambuka duniani watakupongeza na kukujaza Upepo, ila nina uhakika wa 100% hao hao baadae watakuacha peke yako na Wengineo kuanza Kukucheka japo juzi, Jana na leo watakuona Shujaa.
Najua katika huu Uzi wangu nitashambuliwa mno na Wanafiki wale wale ambao wana Mihemko ya Kisiasa na Chuki ila naamini wenye Akili Kubwa watanielewa vyema kabisa.
Watu waliosoma vyema Strategic Studies watakumbuka hii Kanuni Kuu ya KUUSOMA KWANZA MCHEZO KABLA YA KUUCHEZA na unatakiwa kuwa very Smart Kupambana na Tawala nyingi za Kimafia barani Afrika vinginevyo utakuwa unakaribisha DHAHAMA yako mwenyewe na baadae kuja Kujuta.
View attachment 3354205
Mlibeza sana CHADEMA na kusema hawana akili kwa sababu ya no reforms no election,na hata watu wa makanisani/misikitini tulisema na kujiona tuko salama kwa sababu hatukutegemea kuingia kwenye maandamano.Sasa muda umefika wa watu wote(aliyekuwamo na asiyekuwamo) wataimba wimbo mmoja.
maana kama siyo wewe ndugu yako ataguswa.
Suala hili la gwajima,halina tofauti na kauli ya chadema ya no reforms no election,kwani hoja yao kubwa ni kupinga kuuwawa wakati wa uchaguzi wakati wao huingia kwenye mchakato wa uchaguzi kwa mujibu wa sheria na kugombea kwao sio sehemu ya uhalifu.Kwanini uchaguzi unageuka kuwa umauti kwao?
Watu wengi wanalaumu kwamba njia zinazotumika kudai wanachodai siyo sahihi,niwaulize njia sahihi ni ipi?
watasema kwenda mahakamani,niulize tena nani anasimamia haki mahakamani?
utanijibu hakimu,nitakuuliza tena ni nani huwapandisha mahakimu kuwa majaji,au ambaye tayari ni jaji hapa kwetu nani alimpa huo ujaji? hapo utaniambia NYAMAZA. Nami nanyamaza ila naamini umepata somo
Sisi wazazi ukimchapa mtoto,ataanza na kilio,ukizidisha anataka kukimbia
unamkamata mkono unaendelea kumchapa,anajikojolea,ukiendelea zaidi anajiharishia lakini kumbuka harufu ya kinyesi na wewe utainusa, ukianza kumlaumu kwamba kaharisha sebureni,unatakiwa ujikumbushe kwamba nilipomchapa akakimbia ningelimwacha akimbie.
Nimalizie kwa kusema anayecheka sasa,asijisifu maana kuna wakati harufu mbaya itamfikia popote alipo.
Nikutakie siku njema