Unakosea, Unakosea na nasema tena Unakosea wenye Akili hawashindani na 'System' Kibwege (Kipumbavu) hivi..shauri yako!!

Unakosea, Unakosea na nasema tena Unakosea wenye Akili hawashindani na 'System' Kibwege (Kipumbavu) hivi..shauri yako!!

Nakuonea sana Huruma japo Wanafiki na Wasiojua mambo ya Kimtambuka duniani watakupongeza na kukujaza Upepo, ila nina uhakika wa 100% hao hao baadae watakuacha peke yako na Wengineo kuanza Kukucheka japo juzi, Jana na leo watakuona Shujaa.

Najua katika huu Uzi wangu nitashambuliwa mno na Wanafiki wale wale ambao wana Mihemko ya Kisiasa na Chuki ila naamini wenye Akili Kubwa watanielewa vyema kabisa.

Watu waliosoma vyema Strategic Studies watakumbuka hii Kanuni Kuu ya KUUSOMA KWANZA MCHEZO KABLA YA KUUCHEZA na unatakiwa kuwa very Smart Kupambana na Tawala nyingi za Kimafia barani Afrika vinginevyo utakuwa unakaribisha DHAHAMA yako mwenyewe na baadae kuja Kujuta.

View attachment 3354205
Punguza uoga heshima sio uoga nizamu sio uoga,semakweri kua mkweri itakua huru #$haya maisha yaduniani Yana mwisho
 
Uko sawa,
Alikuwa na pointi ila uwakilishaji wake haukuwa planned. Kwa sasa kwa binadamu mwenye utashi lazima anafadhaika.

Hii siyo vita ya kawaida, imepitiliza.
Nashukuru kwa Kunielewa vyema Mkuu juu ya Andiko langu na Hoja zangu Kwake Askofu Gwajima.
 
" Chezea ndevu, usichezee serikali", alisikika baba mmoja akiyasema haya kwa vijana wake enzi hizo.
 
Hizi huwa ni Mentality za KIPÚMBAVU sana...... kwanini mnatetea watu wote tuwe MAKONDOO?
Kwahiyo busara kwako ni watu wote tukae kimya na kusifia ujinga unaoendelea?

Kila mtu anajua duniani kote vita dhidi ya watawala dhalimu haijawahi kuwa vita RAHISI hata siku mmoja

Hakuna utawala dhalimu utakao dumu milele duniani...... hata huu utaanguka tu na sababu ni hawa hawa unaotaka wakae kimya as if nothing happened.
Yes serikali inaweza kumuua Gwaji kama ilivyo muua Ben na wengine..... lakini serikali haiwezi kuua idea wanayotaka raia, ndio maana wamemuua Ben kaja Mdude na wataendelea kuibuka kila uchwao hadi takwa litakapo timia....... this is just a process tukiikwepa hii tutazalisha taifa la MAKONDOO daima

Kama mimi na wewe ni waoga acha wenye ujasiri wa kufanya hivyo bila kuogopa watakayo pitia wafanye hivyo..... ndio wito wao na ndio njia ya ukombozi

Leo mnaona udhalimu, wakati Hakuna hapo aliyekamatwa, waislamu waliendewa misikitini na mabuti wakawakamata Masheikh wa uamsho na wakasekwa Ndani kwa miaka zaidi ya 9 na kubambikiwa kesi Za kigaidi, wengi wenu mlikuwa mnafurahia na kuwatukana humu jf , nyinyi mnaonjeshwa kidogo tu mnaanza kutoa povu hata sinema halijaanza bado
 
Kwanza kabisa mimi siamini kwenye ujinga unaoitwa MUNGU wala dini yoyote ile

Pili nimejibu hoja ya mleta hoja ambayo haina hata chembe ya UDINI....... Gwaji alisemea wanaotekwa na kupotezwa bila kujali dini zao

Pole yako unaosumbuliwa na hekaya za kusadikika za dini?
 
Shida iliyopo ni moja tu! Watu wakiamua kusema, kamwe hutaweza kuwanyamazisha wote! Unamfunga Lissu, Heche anaendelea kusema! Unamshambulia Kitima, Gwajima anajitokeza! Unamuua Ben Saanane, Mdude anaibuka! Unamuua Mdude, anatokea mwingine!!

Binafsi sikumbuki kama kuna mtawala katili aliwahi kunyamazisha midomo ya wakosoaji wake. Maana ukimuua mmoja, wanazaliwa wengine 100. Njia pekee ya kuondokana na haya makando kando ni kwa mtawala tu kukubali kusikiliza mawazo ya wananchi, badala ya kusikiliza mawazo potofu ya kundi baya la wahuni waliomzunguka.
Mjadala ufungwe....
 
Kwanza kabisa mimi siamini kwenye ujinga unaoitwa MUNGU wala dini yoyote ile

Pili nimejibu hoja ya mleta hoja ambayo haina hata chembe ya UDINI....... Gwaji alisemea wanaotekwa na kupotezwa bila kujali dini zao

Pole yako unaosumbuliwa na hekaya za kusadikika za dini?
Kwani utekaji ulianza jana na juzi ??? , muda wote alikuwa wapi?? hatukumsikia kukemea; hata kuna wakati Marehemu Maalim aliwahi kwenda kukutana naye wala hakutamka chochote kukemea maovu ya serikali ya chama chake CCM
 
Nakuonea sana Huruma japo Wanafiki na Wasiojua mambo ya Kimtambuka duniani watakupongeza na kukujaza Upepo, ila nina uhakika wa 100% hao hao baadae watakuacha peke yako na Wengineo kuanza Kukucheka japo juzi, Jana na leo watakuona Shujaa.

Najua katika huu Uzi wangu nitashambuliwa mno na Wanafiki wale wale ambao wana Mihemko ya Kisiasa na Chuki ila naamini wenye Akili Kubwa watanielewa vyema kabisa.

Watu waliosoma vyema Strategic Studies watakumbuka hii Kanuni Kuu ya KUUSOMA KWANZA MCHEZO KABLA YA KUUCHEZA na unatakiwa kuwa very Smart Kupambana na Tawala nyingi za Kimafia barani Afrika vinginevyo utakuwa unakaribisha DHAHAMA yako mwenyewe na baadae kuja Kujuta.

View attachment 3354205
Wewe ulioandika huu ugoro na uhakika wewe ni mmoja wa hao wanao teka watu. Kwanza huna akili kabisa. Kwasababu unajuwa usalama wako uko chini ya hili kundi la wahuni wanaitwa serikali ya ccm na vyombo vyake. Kitu mhim unachosahau ni kuwa hakuna serikali yoyote dunia iliyoweza kwenda kinyume na wananchi wake ikasalimika. Ni suala tu la mda nyinyi watekaji na wanao watuma mwisho wenu hako mbali hata kidogo. Mimi nawaombea tu maisha malefu ili msife kabla hamjapata malipo yenu ya uovu wenu. Yes hata mimi si amini kuwa kuna Mungu. Kuto kuamini kuwa hakuna mungu hakumfanyi binadam amfanyie binadamu mwezake unyama kama mnao wafanyia watanzania. Wanyama wa polini hawajui Mungu lakini huwezi kukuta mnyama yoyote anakula watoto wake au wanyama wa aina yake. Sasa nyinyi wajinga na wapumbavu mnakuwaje mnaona kuuwa ndugu zenu ndio njia sahihi ya kuwapatia maisha mazuri? Kama kuuwa watu kunaisaidia serikali kuendelea kutawala makaburu wa south Africa mpaka leo wangekuwa wnatawala.
 
Tangu nijiunge JF sijawahi kudhani kwamba siku moja nitakuja kulike Uzi wa popoma.

Mkuu Popoma pamoja na kwamba una makandokando mengi Sana kwenye nyuzi zako lakini Leo kwenye Uzi huu umeandika kitu kikubwa Sana.
Big up Sana popoma. Purely talented guy
 
Nakuonea sana Huruma japo Wanafiki na Wasiojua mambo ya Kimtambuka duniani watakupongeza na kukujaza Upepo, ila nina uhakika wa 100% hao hao baadae watakuacha peke yako na Wengineo kuanza Kukucheka japo juzi, Jana na leo watakuona Shujaa.

Najua katika huu Uzi wangu nitashambuliwa mno na Wanafiki wale wale ambao wana Mihemko ya Kisiasa na Chuki ila naamini wenye Akili Kubwa watanielewa vyema kabisa.

Watu waliosoma vyema Strategic Studies watakumbuka hii Kanuni Kuu ya KUUSOMA KWANZA MCHEZO KABLA YA KUUCHEZA na unatakiwa kuwa very Smart Kupambana na Tawala nyingi za Kimafia barani Afrika vinginevyo utakuwa unakaribisha DHAHAMA yako mwenyewe na baadae kuja Kujuta.

View attachment 3354205
Nakubaliana nawe. Approach iliyotumika haijakaa sawa.
 
KILO 50 ZA DAWA ZA KULEVYA ZAKUTWA KANISA LA GWAJIMA
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi limekamata kilo 50 za dawa za kulevya ndani ya jengo linalomilikiwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima, linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima, katika operesheni ya kushitukiza iliyoendeshwa mwishoni mwa wiki.
Tukio hilo limeibua maswali mazito kuhusu uhalali na maadili ya baadhi ya viongozi wa kidini nchini, hususan kwa Gwajima ambaye kwa miaka ya hivi karibuni amejitokeza kama sauti yenye ushawishi mkubwa katika siasa na mijadala ya kijamii.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni SACP Mtatiro Kitinkwi
dawa hizo zilipatikana katika moja ya vyumba vya kanisa hilo vilivyokuwa vimefungwa kwa muda mrefu. Uchunguzi wa awali unaeleza kuwa chumba hicho kilikuwa kikiendeshwa kwa siri na watu waliodaiwa kuwa wafanyakazi wa ndani wa taasisi hiyo.
“Tunachunguza kwa kina kuhusiana na uhusiano wa wahusika na uongozi wa kanisa. Hakuna mtu aliye juu ya sheria,” alisema kamanda huyo.
Tukio hili limezua taharuki miongoni mwa waumini na wananchi kwa ujumla, huku wengi wakitaka Gwajima kujitokeza na kutoa maelezo ya kina. Wapo wanaodai kuwa tukio hilo linaweza kuwa njama dhidi yake, huku wengine wakisisitiza kuwa ni ishara ya kuporomoka kwa maadili ndani ya taasisi za kiroho.
“Tunajiuliza, je, bado tunaweza kuwaamini watu wanaojiita wachungaji wakati maeneo ya ibada yanageuzwa maficho ya uhalifu?” alihoji mmoja wa wakazi wa Kinondoni.
Hadi kufikia jana jioni, hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na Askofu Gwajima wala uongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kuhusu tukio hilo. Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi na limeahidi kuweka wazi ukweli utakapopatikana.
Ikumbukwe Mnamo mwaka 2016 Mchungaji Gwajima aliwahi kupekuliwa na kukutwa na bastora aina ya Baretta yenye namba CAT 8802 akiwa hospital ya TMJ ambapo zoezi hilo la likifanywa chini ya aliyekuwa kamanda wa upelelezi wa kanda maalum ya Dar es Salaam SACP Costantine Massawe ikiwa ni tukio linaholusishwa na kumiliki genge la wahalifu,kujipatia fedha kwa njia isivyo halali na kukutwa na dawa za kulevya.
Mbali na Gwajima, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni msaidizi wa askofu huyo, Yekonia Bihagaze (39), mfanyabiashara George Mnzava (43) na mkazi wa Kimara Baruti, Geoffrey Milulu (31).
Aidha, inadaiwa washtakiwa hao walikuwa wakimiliki isivyo halali risasi tatu za bastola pamoja na risasi 17 za bunduki aina ya shotgun. Gwajima anadaiwa kushindwa kuhifadhi silaha katika hali ya usalama.
 
Pamoja na hayo ebu pia tujiulize hivi nchi hii kwasasa ni kosa la jinai kukemea utekaji?

Ni kosa kubwa lipi alilolifanya Gwajima linalostahili haya yote anayofanyiwa. Ina maana watawala wana haki ya kutuvuna/kutuua sisi raia kila tunapoonekana kuwakosoa.

Je tuamini kwamba serikali ndiyo inayoteka, kutesa na kuua raia wake? Mbona watu wanaojitokeza kukemea kwa nguvu uovu unaofanywa nchi hii waonekane wanazipinga mamlaka?

Kama taifa tunatakiwa tujitafakari sana. Tunakoelekea siko kabisa.
Wametuthibitishia kuwa serikali ndio mhusika. Hakuna maswali hapo
 
Back
Top Bottom