Unakula nini/unakunywa nini huku ukiwa unabarizi hapa JF?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
41,558
Reaction score
64,966
Nimetoka zangu kwenye mihangaiko ya hapa na pale, nikaingia bandani nikachukua mayai mawili kutoka kwa kuku wangu wa kienyeji, nikayachemsha na kuyafanya kitafunwa na chai yangu ya kahawa, huku hawa kuku zangu wakinitazama ninavyokula uzao wao.

Baada ya nusu saa, nikaingia shambani na kuvunja mahindi sita, nikayachemsha, na sasa nayatafuna huku nikisoma jumbe zenu hapa JF.

Hii ndio fahari ya kuishi kijijini/ nje ya mji, unakula kitu kisichokuwa na kemikali, hewa safi; natamani na nyie wananzengo mje huku.
​
Hapo ulipo, unakula nini/unakunywa nini huku ukiwa unabarizi hapa jf? Au unabarizi huku mdomo ukiwa mkavu?
mahindi.jpg
 
Nimetoka zangu kwenye mihangaiko ya hapa na pale, nikaingia bandani nikachukua mayai mawili kutoka kwa kuku wangu wa kienyeji, nikayachemsha na kuyafanya kitafunwa na chai yangu ya kahawa, huku hawa kuku zangu wakinitazama ninavyokula uzao wao.

Baada ya nusu saa, nikaingia shambani na kuvunja mahindi sita, nikayachemsha, na sasa nayatafuna huku nikisoma jumbe zenu hapa JF.

Hii ndio fahari ya kuishi kijijini/ nje ya mji, unakula kitu kisichokuwa na kemikali, hewa safi; natamani na nyie wananzengo mje huku.
​
Hapo ulipo, unakula nini/unakunywa nini huku ukiwa unabarizi hapa jf? Au unabarizi huku mdomo ukiwa mkavu? View attachment 3591249
Nakunywa maji hapa.
 
Nimeweka playlist ya R&B huku nyimbo za Aaliyah zikiwa nyingi zaidi..
Wataalamu wanasema, nyimbo za kubembeleza upunguza mapigo ya moyo, na kufanya moyo ushindwe kusukuma damu inavyotakiwa; chakufanya toka hapo chumbani mtoe jogoo bandani uanze kumkimbiza, hiyo ni sehemu ya zoezi.​
 
Back
Top Bottom