Yeah kabisa. Ukishaona tu mwanamke anakutolea kauli za ajabu ambazo zinaonyesha kuwa hakujali na anakuona kuwa wewe ni for granted, wewe jifanye mnyonge na mnyenyekevu then muingize katika kumi na nane yako kisha una mbadilikia......
Kuna brother, alikuwa amekutana na mwanamke wa sampuli hiyo, jamaa akawa mpole sana. Kumbe ameanza mahusano na rafiki ya huyo dada kwa siri na ameshamwambia shida za rafiki yake.
Unajua kuna ile hali mkeo anakuwa na rafiki yake unakuja mjua umeshaanza na mkeo tayari. Sasa mkeo awe na matabia ya ajabu hadi rafiki yake anajua na ameshaona kuwa wewe ni mtu poa sana sema tu mkeo hajui bahati aliyonayo kuwa na wewe.
Jamaa ameshakaa na mwanamke miaka kadhaa kumbe alikuwa anayapanga maisha na rafiki wa mkewe wakafanya maandalizi mengi sana nje ya mkewe kujua.
Kuna siku mwanamke mke wa jamaa kama kawaida yake akamtolea zile kauli za ondoka kama unaona nakukera na hakuna mwanamke atakuwa na wewe, jamaa akaona isiwe shida akaamua kuondoka tu siku moja kimya kimya akahamia makazi mapya na huyo mwanamke.
Na maisha yakaenda poa tu. Siku ziakenda demu anakuja kujua jamaa ana mtoto na mwenzake na maisha ni safi tu..... Akajiribu wafanyia fujo ila wapi ndio ikawa tamati yake.