Unakumbuka kauli gani chafu iliowahi kukukera ukajiengua from a Toxic partner?

[emoji2960][emoji2960][emoji2960][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Fala umenchekesha
 
Niliambiwa sioni umuhimu wa kuwa na wewe... mweee nilichoka nkakaa na chini na kiherehere changu kikaniisha nikakubali kushindwa nkaachana nae for good maisha yakasonga nashukuru Mungu nw nipo na mwanaume wa maisha yangu....
 
Yaani mkuu hapa usiniangalie mimi wala usiniulize mimi nataka nini! Kwa sababu hapa siongelei ninachotaka mimi bali ninaongelea uhalisia na namna mambo yanatakiwa yawe kwenye jamii!

Nikisema nijiongelee mimi basi itabidi nikae kimya maana sina nilichoexperience katika hayo! I always speak for my fellow women sababu sipendi kuona mtu anamnyanyasa mwenzie bila sababu!
 
Hakuna anayejitetea tunafahamishana, tunaweza tusijitetee na hali ikabaki ilivyo asili haipingwi

Tafuta sababu za mkutano wa beijing acha kubumba bumba zako
Tofautisha kati ya asili na mambo ya kujitungia! Msilazimishe kila kitu hata maovu mnayofanya yawe asili!
 
Mkuu kuna watu wana stress zao. Kwanilivyomwelewa mchangiaji hapo juu, ana chuki binafsi na ndio aina ya wanawake ama waliumizwa na sasa wanachuki moyoni, ama ego inawasumbua.
Pole sana! Huwa mnatamani iwe hivyo kweli ila ndiyo haitakaa iwe hivyo!
 
Ni kweli inahitajika uwe na hekima ya ziada maana midomo ndio silaha yao,especially wakishakuwa rage...
 
Hata mimi sikubaliani na unyanyasaji kama ndio tunaozungumzia

Lakini kushare kipato chako(sio kulea mwamaume) hilo ni lazima ama sivyo utafanya mambo kuwa magumu
 
Unaongea na mwanaume wa tofauti sana na hao unaosema wapo katika jamii
Ni jana tu nimetoka kumsaidia wife shughuli fulani za nyumbani maana wiki hii amebanwa sana na shughuli za kuitafutia kipato familia

Sio kwamba mimi sina shughuli yangu ninayo ila yake kwao kuna moja imetokea nae akawemo na hiyo hela ameileta nikaiona tukaipangia

Kama kuna wanaume katika mazingira haya bado wataona wamejidhalilisha hawako sahihi

Mwanamke hawezi kutoka saa 10 alifajiri akaenda kutafuta hela akakuacha nyumbani umelala akarudi jioni sana pengine saa moja kasoro ukivaa viatu vyake unaona kabisa lazima atakuwa amechoka halafu aamke usiku afanye shughuli zake ndio aende huko anakojihimu kwa akili ya kawaida unajiongeza tu unaangalia shughuli iliyopo unamsaidia ili akiamka avae na kuondoka tu

Jana nimefua nguo zangu, zake na za mtoto kumpunguzia kazi

Sijajua unazungumzia wanaume wa aina gani pengine hapa ndio tunapishana

Kama ni Marioo hao hawakubaliki piga spana
Kama wale waliotopea kwenye mfumo dume piga spana
Kama wale washusha vipigo piga spana

Lakini kwa mwanaume straight lazima uende nae sawa

Nilihofia maana ilibaki kidogo useme wanaume wote mbwa...sio wotw bhana
 
Tofautisha kati ya asili na mambo ya kujitungia! Msilazimishe kila kitu hata maovu mnayofanya yawe asili!
Asili ni mwanaume ni kichwa cha familia[emoji3][emoji3] nitakuongoza wewe na kipato chako fairly na wewe ukaridhika

Kazi ni yako, mshahara ni wako lakini nitakushauri, tunatumiaje sio unatumiaje, sitaingilia shida za kwenu pindi hela itakapohitajika lakini mizinga ikizidi nitakushauri kwa vitendo maana siwezi kusema kwenu wamezidi punguza kuwapa hela wakati mimi kwetu nawapa na unaona
Nikisema punguza na wewe unaona kwetu nimepunguza nasaidia pale penye haja ya kufanya hivyo

Maisha ni mepesi sana nafikiri tunakutana na watu wasio sahihi tu
 
Hata mimi sikubaliani na unyanyasaji kama ndio tunaozungumzia

Lakini kushare kipato chako(sio kulea mwamaume) hilo ni lazima ama sivyo utafanya mambo kuwa magumu
Inakuwaje lazima wakati siyo tamaduni za kiafrika? Si mnasema tunatakiwa tufuate tamaduni zetu za kiafrika au?
 
Sasa hapa umenifurahisha and this has always been my point! Hebu muite ndugu yako Extrovert asome hapa na ajibu halafu ndiyo utajua mimi na yeye tunapishanaga wapi!

Huyo Extrovert yeye anataka hivi! Hata yeye na mwanamke wake wote wawe wanatafuta pesa na wanachangia bills pasu kwa pasu basi kazi za ndani bado azifanye mwanamke peke yake yeye hahusiki kabisa which is totally unfair and against our african traditions!

Ndiyo maana nasema it's either mwanaume na mwanamke wasaidiane kutafuta pesa na kazi za ndani kwa pamoja au mwanaume atafute pesa peke yake na mwanamke afanye kazi za ndani peke yake! Lakini siyo eti mmoja anafanya jukumu moja ila mwingine anafanya yote mawili hiyo siyo sawa kabisa!

Na kama wewe upo hivyo basi hongera mkuu mko wachache sana! Wanaume wengi kwenye jamii zetu hizi za kiafrika wanaangukia kwenye hilo kundi nililolizungumzia hapo juu na hao ndiyo ninaowaongelea humu mara nyingi!
 
Ni kweli maisha ni rahisi sana! Ila tu watu wengi wanapata watu wasio sahihi na hali kama hii ndiyo inafanya wengi tuogope kuingia kwenye mahusiano au ndoa maana hali ni tete!
 
Mimi sifanyi wakati wote nisiwe muongo lakini kuna wakati nafikiri anahitaji msaada

Kama alipokuwa mjamzito, alianza kuumwa tangu wiki ya kwanza mpaka miezi tisa

Nimenyooka kweli kweli kupika, kufua nk. hadi alipopatikana binti msaidizi
 
Unaweza ukawa sawa usemacho, Ila je, utafurahi siku wamekuja mashoga zako kukutembelea wakakuta mumeo anaosha vyombo au anadeki!???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…