Unakumbuka kauli gani chafu iliowahi kukukera ukajiengua from a Toxic partner?

Unakumbuka kauli gani chafu iliowahi kukukera ukajiengua from a Toxic partner?

Hata kufanya kazi kujitafutia kipato binafsi kwa mwanamke sio tamaduni zetu. Tamaduni zetu Ni zile za mwanamke golikipa. Nkikuruhusu ufanye kazi basi lazima hela yako nitie mkono wangu pia.
Basi oa mwanamke golikipa tu mkuu! Huyo ndiyo atakufaa ukitaka uishi kwa amani maisha yako yote ya ndoa!
 
Nilipobaini kwake wanaume wote ni takataka nilimshauri aachane na mambo ya ndoa/mapenzi

Ilikuwa tuishie pale maana shida yake imeanzia mbali
Duuh wapi nimesema wanaume wote ni takataka? Hebu nioneshe tafadhali!
 
Hivi unafikiri ni rahisi kumnyima hela mwanamke unayempenda?
Khaa sasa kama unampenda kwanini ulalamike? Mie ninachojua mwanamke kama ukimpenda siyo tu hautaona shida kumpa hela bali pia hautalalamika unapompa hela yako!

Halafu ninyi wanaume si ndiyo mnasemaga huwa hamtumii hisia kupenda mnatumia akili? Sasa unaanzaje kumpenda mwanamke ambaye anaombaomba hela si umuache tu?
 
Kama ndivyo, mwanamke hatakiwi kufanya kazi. Akae nyumbani alee familia. Kwanini mnataka upande mmoja tu ndio unufaikie/kuumia na hiz 50/50 zenu? Yaani maana ya 50 50 inakuwaje sasa iwapo changu chako na chako chako?
Sasa upande upi unaonufaika na upi unaoumia hapo? Tena mimi naona ninyi wanaume ndiyo huwa mnataka mnufaike kwenye kila kitu kinachohusiana na mapenzi!

Maana 50/50 inataka mwanaume na mwanamke wote wawe sawa kuanzia kwenye haki hadi kwenye majukumu! Ila ninyi wanaume hamtaki kuwe na haki sawa ila kwenye majukumu mnataka tuwe sawa tena majukumu yenyewe ni ya kiuchumi tu ndiyo mnataka tuwe sawa ila kwenye majukumu mengine hatuko sawa siyo?
 
Uamuzi unaokufaa ni kuachana na mahusiano

Inawezekana kuna mengine unamudu
Kwahiyo mimi hadi sasa sijaelewa point yako mkuu hebu niweke wazi! Wewe unataka mwanaume atafute pesa na ahudumie familia tu ila mwanamke atafute pesa ahudumie familia afanye kazi za ndani azae na bado alee mume na watoto peke yake au unatakaje hebu kuwa tu mkweli?
 
Hiyo ni jumla ya mawazo yako
Siyo mawazo yangu bali labda yako mkuu! Mie nawafahamu wanaume wengi tu wenye hiyo mitazamo kama yangu na ndiyo maana nasema wapo sasa hao nao hauwezi kusema ni takataka au ni mbwa mie sifanyagi hizo generalizations za kijinga mkuu!
 
Kwahiyo mimi hadi sasa sijaelewa point yako mkuu hebu niweke wazi! Wewe unataka mwanaume atafute pesa na ahudumie familia tu ila mwanamke atafute pesa ahudumie familia afanye kazi za ndani azae na bado alee mume na watoto peke yake au unatakaje hebu kuwa tu mkweli?
Unawachukia wanaume unayachukia mahusiano pengine kuna mahusiano unayamudu
 
Hawa wa jf ndio tunaotoka huko huko kwa hao wanaume wote mkuu. Pliz badilisha kidogo huo mtazamo wako, hautapingwa na wanaume tu hata baadhi ya wanawake wenzio watakupinga pia.
Wanaume wote wa jf wako mtaani ila siyo wanaume wote wa mtaani wako jf! Huo mtazamo wangu unataka nibadilishe wapi hasa mkuu?
 
Back
Top Bottom