...
Hakukuwako DSTV mtaani kwetu kuangalia Manchester na Arsenal, kulikuwa na Sani unacheki Bush Stars Na watoto wa mjini kina CHEPE..
kuna mzee meko, MAPUNG'O,BOB MAZISHI, KOBELO, UDEZE, na wengine wengi ktk timu za mpira kwenye hadithi za picha kulikuwa na obi, mayuku, zumo, linda, chino nk
lodi lofa na madenge nilikuwa nawapenda sana.
Na zile riwaya za mapenzi sijui oscar, LILIAN, victor na nani vile, nshaaahau.
mimi nalikumbuka sana bongo..hasa njomba nchumali,mapungo..na michoro kama ya kifo cha 2pc ilikua balaa tupu..mapungo kwa sasa ni kama balotel.
aisee umenikumbusha mbali sana, hapa nakumbuka visa vya zena na betina, betina na mamaake walivyokondeana afu mawizard vbaya, nilimpenda sana obi jinsi alivyomudu kupambana na mzee ole shingo nguzo ya umeme....unamkumbuka star wa bush star? Aliwahi pata mke kwa kushnda magoli....nakumbuka pia alizawadiwa simu afu siku moja akaingia nayo uwanjani anataka kushnda goli si ikaita....unajua nn kilitokea? Asante muanzisha kamba!
Yule cha pombe alikuwa anaitwa Sokomoko,bado umesahau adithi ya Obi,Linda na mkulu Zumo ilikuwa balaa,gazeti lilianza kupoteza mwelekeo baada ya mchoraji mkuu kutoka Iringa John Kaduma kufariki
Songombingo za kaboka Mchizi..
Kuna team za mpira zilizokuwa pinzani na Bush Starz na Born town kina kipepe ndio walikuwa first 11 ya Bush Starz while kina Pimbi na Lodilofa Born town
Kuna team ilikuwa inaitwa Makwekwe original kama sikosei
Kuna toleo moja Ndumilakuwili aligeuka kuwa ninja mambo ya "Yang Kibadanchi shodani kata"
Wachoraji wa sani walikuwa wanaimagination za hali ya juu sana kwani waliweza kuyaweka maisha ya kitanzania wakichanganya na ya kusadikika kwenye michoro yenye maandishi.Tanzania ya leo sijui kam kuna watu wenye Imaginationa za hali ya juu kiasi kile .Labda kaka yetu nguli wa vikatuni Masudi Kipanya.
Tanzania tusivyokuwa na utamaduni wa kutunza kumbukumbu sijui kama zile nakala zipo kwenye maktab ya Taifa.
R.I.P Waliokuwa waasisi na wachoraji wa Sani