Unakumbuka nini katika enzi za gazeti la Sani?

Unakumbuka nini katika enzi za gazeti la Sani?

kuna hadithi moja ilikua inaitwa maji mazito , ilitungwa na Said Salim Bawji, niliifutilia kweli , kulikua na Character mmoja anaitwa Side Spy, Vick n.k
sikuwahi kuimaliza riwaya ile, natamani niirudie kuisoma lakini sijui wapi nitaipata.

WAMASA...................WACHAPISHAJI WA MAGAZETI YA SANI
 
nikurekebishe ni JARIDA LA SANI SIO GAZETI
 
Songombingo za kaboka Mchizi..
Kuna team za mpira zilizokuwa pinzani na Bush Starz na Born town kina kipepe ndio walikuwa first 11 ya Bush Starz while kina Pimbi na Lodilofa Born town
Kuna team ilikuwa inaitwa Makwekwe original kama sikosei

Kuna toleo moja Ndumilakuwili aligeuka kuwa ninja mambo ya "Yang Kibadanchi shodani kata"

Wachoraji wa sani walikuwa wanaimagination za hali ya juu sana kwani waliweza kuyaweka maisha ya kitanzania wakichanganya na ya kusadikika kwenye michoro yenye maandishi.Tanzania ya leo sijui kam kuna watu wenye Imaginationa za hali ya juu kiasi kile .Labda kaka yetu nguli wa vikatuni Masudi Kipanya.

Tanzania tusivyokuwa na utamaduni wa kutunza kumbukumbu sijui kama zile nakala zipo kwenye maktab ya Taifa.

R.I.P Waliokuwa waasisi na wachoraji wa Sani
 
aisee umenikumbusha mbali sana, hapa nakumbuka visa vya zena na betina, betina na mamaake walivyokondeana afu mawizard vbaya, nilimpenda sana obi jinsi alivyomudu kupambana na mzee ole shingo nguzo ya umeme....unamkumbuka star wa bush star? Aliwahi pata mke kwa kushnda magoli....nakumbuka pia alizawadiwa simu afu siku moja akaingia nayo uwanjani anataka kushnda goli si ikaita....unajua nn kilitokea? Asante muanzisha kamba!
 
Dah huu uzi kweli umetukumbusha mbali vijana wa zamani. Namkumbuka sana kipepe katika pilika zake za kuwinda ila sungura wanamtoa jasho ile mbaya. Siku moja alikuwa anawinda mara uso kwa uso na simba! Asikuambie mtu palikuwa hapatoshi
 
hv haya majarida huwezi yapata maybe kwe archives....dah himaya ya kitintale nomaa,sokomoko,mzee meko dah
 
Ndumilakuwili na mingo zake bwana, lile sijui lilikuwaga toleo gani,
mida ya usiku kituoni anamlia mingo jamaa amkabe kumbe jama naye anampigia hesabu Ndumilakuwili, kujipindua akawahiwa yeye, kumbe Ndumilakuwili mfukoni alikuwa hana kitu jamaa alimtukana.
Kuna kisa kingine cha Ndumilakuwili alikuwa anataka kumkaba mtu basi akatafuta mteja kabisa akawa ana-bargain bei kabla hajamkaba mtu mwenyewe, nilikuwa nacheka sana na bwana Ndumilakuwili.

Kali zaidi ni pale waliingia dili na Lodilofa kwaajili ya mradi wao wa "fruit na juice ya ajabu"
hahahahaha

Nikikumbuka hayo na nkiangalia saiv kinachoendelea kwenye idara ya burudani huwa nakubali kuwa tunapotea tu!
 
Zile story za wimbi la kitintale ni balaa, kuna mtu mmoja alikuwa chini ya mzee Ole alikuwa anaitwa Riwa, mtu flani hivi mkakamavu amenyoa ule mtindo wa zamani unaitwa panki halafu anavaa miwani nyeusi ya jua,ana uso mwembamba, mkakamavu mikono yenye nguvu sana, lakini siku moja alikamatwa na kina Obi. Pia page ya katikati ya gazeti kulikuwa na vichekesho vilivyoitwa 'Nichekeleeeee'
 
Daa mie nakumbuka lile gazeti sijawah kulipata lote zima unapata kurasa chache nyingine unaambiwa mtafute flani anakulasa nyingne enzi Izo Mbeya.
 
...
Hakukuwako DSTV mtaani kwetu kuangalia Manchester na Arsenal, kulikuwa na Sani unacheki Bush Stars Na watoto wa mjini kina CHEPE..

Kama sikosei chepe alikua kwenye jarida la bongo na siyo sani.
 
kuna mzee meko, MAPUNG'O,BOB MAZISHI, KOBELO, UDEZE, na wengine wengi ktk timu za mpira kwenye hadithi za picha kulikuwa na obi, mayuku, zumo, linda, chino nk

Golden boy mapung'o na bob mazishi walikua jarida la bongo, hawa akina udeze na kobelo nadhani walikua Jarida la Tabasamu, waliobaki kina zumo, obi, ole, et al. ndani ya Wimbi la Kitintale ktk jarida la Sani.
 
lodi lofa na madenge nilikuwa nawapenda sana.
Na zile riwaya za mapenzi sijui oscar, LILIAN, victor na nani vile, nshaaahau.

Ah! Usinikumbushe mambo ya LILIAN SEUYA na misukosuko ya mapenzi hadi akakata tamaa ya kuolewa ila akapata kijana (jina limentoka) akamfariji hatimaye wakafunga ndoa.
 
mimi nalikumbuka sana bongo..hasa njomba nchumali,mapungo..na michoro kama ya kifo cha 2pc ilikua balaa tupu..mapungo kwa sasa ni kama balotel.

Nadhani mchoraji wa mikasa ya 2pac alikua bwana Fortunatus Ndila kama sikosei. Asante kwa kutukumbusha na hili jarida la bongo ambalo lilikua na riwaya flan(jina limentoka) kukiwa na mhalifu kwa jina la "Mark Steven Chenje."
 
Hahaha...umenikumbusha jamaa alipelekwa Ulaya akacheze mpira nadhani ni Real Madrid kama ckosei usiku wa kwanza tu kulala jamaa akaachia kimba kitandani aah aah wazungu wakasema hii kitu hapana bwana....
aisee umenikumbusha mbali sana, hapa nakumbuka visa vya zena na betina, betina na mamaake walivyokondeana afu mawizard vbaya, nilimpenda sana obi jinsi alivyomudu kupambana na mzee ole shingo nguzo ya umeme....unamkumbuka star wa bush star? Aliwahi pata mke kwa kushnda magoli....nakumbuka pia alizawadiwa simu afu siku moja akaingia nayo uwanjani anataka kushnda goli si ikaita....unajua nn kilitokea? Asante muanzisha kamba!
 
mzee ole, obi na linda
kipepe mzee wa pori
ndumilakuwili kibaka
betina na zena wapinzani wa jadi
pimbi mr love
lodi lofa na mgongo wa chura
 
Yule cha pombe alikuwa anaitwa Sokomoko,bado umesahau adithi ya Obi,Linda na mkulu Zumo ilikuwa balaa,gazeti lilianza kupoteza mwelekeo baada ya mchoraji mkuu kutoka Iringa John Kaduma kufariki

dah kulikua na ponjoro anaitwa MAYUKU,kisiwa cha KITINTALE,M2NZ JON KADUMA,HALAFU DOGO ANAITWA SEBA
 
Songombingo za kaboka Mchizi..
Kuna team za mpira zilizokuwa pinzani na Bush Starz na Born town kina kipepe ndio walikuwa first 11 ya Bush Starz while kina Pimbi na Lodilofa Born town
Kuna team ilikuwa inaitwa Makwekwe original kama sikosei

Kuna toleo moja Ndumilakuwili aligeuka kuwa ninja mambo ya "Yang Kibadanchi shodani kata"

Wachoraji wa sani walikuwa wanaimagination za hali ya juu sana kwani waliweza kuyaweka maisha ya kitanzania wakichanganya na ya kusadikika kwenye michoro yenye maandishi.Tanzania ya leo sijui kam kuna watu wenye Imaginationa za hali ya juu kiasi kile .Labda kaka yetu nguli wa vikatuni Masudi Kipanya.

Tanzania tusivyokuwa na utamaduni wa kutunza kumbukumbu sijui kama zile nakala zipo kwenye maktab ya Taifa.

R.I.P Waliokuwa waasisi na wachoraji wa Sani

kaboka alikua kwenye gazet la KASHESHE,THEN K0MESHA PIA ALASIR,
YOTE YA Mze mengi,
pia born town n bush starz ni GAZET LA BONGO
 
Mambo yote ni Dr Love Pimbi bhana,alikua anaiokota mizgo tatzo umaliziaji,dah
mara wanene hawapit mlangon,mara ameangukiwa na kidaka cha naz,yaan ni tafran
 
Back
Top Bottom