Unakumbuka nini wakati unafanya mtihani wa Kidato cha Nne

Unakumbuka nini wakati unafanya mtihani wa Kidato cha Nne

.... tuliobeba vyakula kutoka nyumbani na soda ya mirinda(ikiuzwa sh. 100) kwenda navyo kufanya mtihani wa darasa la 7 na tulivyofika shule tuliweka kwenye chumba cha Sayansi Kimu kisha tukafanya mitiani ya masomo yote kwa siku Moja tukala vyakula vyetu na uniform tukachana tufunguliwe uzi wetu.
 
Niliumwa homa kalii ya sikio aisee mpaka ikabidi nijaziwe forms kibao ziambatanishwe na continuous assessments na walimu wakakazia kuwa whatever happens ila ni mwanafunzi wanaenitegemea na kuniamin.....sipendi kukumbuka
 
Sitasahau second masters wetu alipita dirisha la domitory usiku wakati tunajisomea akaturushia kikaratasi kimya kimya. Kucheki kuna maswali mengi ya mtihani wa history wacha tuyasolve usiku mzima tukaacha hadi kusoma sehemu nyingine.

Kesho yake kwenye mtihani tumeingia tuna confidence balaa tunajua kitu chenyewe bwana kilichotukuta ni kipigo cha mbwa koko kama cha Simba kutoka kwa Yanga. Hakuna hata swali moja lililotoka.
 
Shule X arusha ya wahuni asubui wahuni wakipewa pepa wanalala wanandika namba tu.

Pepa la mchana shule ilikuwa inapika kande wahun wanakula kande ya kutosha ili walale kwenye pepa.

Head mistress anapita na ndoo ya maji anawaomba waamke wafanye pepa.

Result
- wanafunzi 500 zero 300.
 
Nilifanya mtihani naumwa tonsils homa kali balaaa...muda wa mapumziko wenzangu wanaenda kusoma me naenda kulala nyumba za walimu...homa haishuki meza dawa zote tonsils zimechachamaa....practical za chemistry na bios zote nmefanya kimagumashi naumwa si mchezo
Ila Mungu alinitendea nilifaulu kiwango cha juu sana
Ila muda wa kusubiri matokeo nilikonda maana nilijua sitoboi
 
Back
Top Bottom