Unakumbuka nini wakati unafanya mtihani wa Kidato cha Nne

Unakumbuka nini wakati unafanya mtihani wa Kidato cha Nne

Ndiyo SIASA hiyo BOSS wangu ๐Ÿ™๐Ÿฝ๐Ÿ™๐Ÿฝ

Hapo utasikia kuna SPECIAL SCHOOLS kama MZUMBE, ILBORU, TABORA BOYS na KIBAHA SECONDARY. Lakini ukijaribu kuangalia TOP TEN YA MWAKA 2007 ya KIDATO CHA NNE, wote niliwaburuza m'maee...๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Hongera mkuu
 
Nakumbukaa kuna Mwamba jinamizi lilimkurupua ndotoni ndani ya chumba cha mtihani, hii ni baada ya Ghakaaa kutiki wazee tukasolve usiku kabda ya pepar. Na ikatubidi tusiwahi kutoka mpaka libaki nusu saa! RIP
 
Kipindi hicho, sie wahenga, ule mtiani uliofutwa! 1998,kwenye paper ya Physics practical, nikawa nachora kwa peni, zimebaki DK 10,muda uishe, ticha wangu akaja taratiiiibu akaninonngoneza, "ukichora kwa peni, unapigwa faini, hiyo paper ndio umeferi" Nilihisi nimemwagiwa maji,nikaona ndoto zangu za kuwa engineer ndio zimeisha, nilikuwa nachukua PCM, sie ndio wale tulikuwa tunajiita sayansi pure, staki combination nyingine, nikaweka nguvu kwenye PCM tu,!
Paper likaisha, jioni wakaja wadogo zetu na kaka zetu wa form 3,2,1,na five na, six, wanatuuliza paper vipi? Mi nilikuwa mmoja wa vipanga pale shuleni, form 4 yetu, ilikuwa inategemewa ifute machozi na Historia ya kufelisha, kabla yetu, shule ilikuwa haijawahi kupata div one au two, ya juu kabisa ilikuwa div 3,ya mwisho!
Ikafika jioni, taarifa ya habari,tukasikia paper imefutwa! (Mungu ananjia nyingi za kumfikisha mja wake apaatakapo) , nikasikia ahueni, tukrudi January 1999! Nikajipanga sawa sawa, piga paper vibaya Sana, nikaitoa kimasomaso shule na one ya point kadhaa, PCM ni Vibanda tu!
Fast forward, Leo na kula matunda ya uinjinia, nikiwaza, nimesoma shule haina umeme, nimetumia kibatari na TAA za chemli,maji mpaka mtoni au ziwani, hakuna smart phone, wala internet, techinolojia kubwa ilikuwa radio zenye FM!, harafu Leo, kuna mtoto hata kama upo st kayumba, material ya kusoma yapo kila Kona, harafu unafeli!
Kuchora kwa peni kwa mitihani ya physics inaruhusiwa.
 
Acha tuu sina hamu kabisa na ile siku mwili ulitetemeka mpaka nikasahau kila kitu.
Kipindi hiki utasikia MZUMBE, ILBORU, TABORA BOYS na KIBAHA SECONDARY. Lakini hawataki kutangaza ORODHA YA WANAFUNZI BORA.. ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Back
Top Bottom