Unakumbuka nini wakati unafanya mtihani wa Kidato cha Nne

Marafiki zangu karibia wote walipiga A.... ila inaweza ikawa ni uzuzu wangu tu sio calculator
We ni kilaza bana unapataje B kwenye shule yenye A hadi za physics sembuse hesabu?.

Ungesoma shule niliyosoma mimi o level ungepata D kabisa huko 🀣🀣.

Kaa na maua(genius) na ww unukie(ufaulu)
 
Watu mlikuwa na utani na necta duuh ulidhani hiyo ni mock sio?.
 
Nakumbuka ilikuaa paper la math, yani nilivyoona paper nikajua A uwakika si nikashangilia kwa nguvu kabla paper lijanza[emoji28].

Msimamizi akaja kunikagua kama nina chabo, lakini sikuwa na kitu nilikuwa kipanga kweli wa math japo nilisoma shule ya kata.

Na kweli matokeo yakivyotoka me ndio mwanafunzi wa kwanza kata ya chanika kupata A ya math, kutoka shule ya kata.[emoji1487]
 
Those days, mi nasolve maswali yangu kadhaa , rafiki wa karibu akawa amelala huku akisema " hayo hayatoki aisee, tulale tu" mi nikawa nafutilia vizuri sana yale maswali...kesho yeye alianza kupewa paper , naona mtu anageuka kuniangalia kwa huzuni...ile kufungua tu paaaaap, maswali kama yalivyo
 
Ama kweli akili ni akili tu
 
2012 Nilifanya pepa ya chemistry ya kupima uelewa mpaka nikawa nafurahi huku najibuu...!! matokeo kutoka ndalichakoo akatunyoosha balaaa shikamoo mama ndalii πŸ˜€ πŸ˜€
Kumbe wewe dogo janja kabisa
 
99 hiyo....naenda kupiga paper ya chemistry kesho yake....nikapiga konyagi nikawa top....asubuhi naingia kwenye mtihani sina habari niko wayuwayu....hangover kama India...Mzee mzima nikagonga nikasepa mchana tulikua sijui na paper ya kiswahili...nikapiga safari mbili...zile za mbuyu...! Ndio nikaenda kwenye paper la kiswahili

Matokeo..Chem C
...Kisw A

Mpaka leo konyagi sijaiacha....japo ladha yake imebadilika..!
 
Nachokumbuka ni yule mwamba kujaza booklet mbili mtihani wa mathematics then matokeo ni f na ndo alikuwa mbabe wa mathematics class yetu.
Mimi ukijumlisha kurasa hazikujaa Tatu Ila nikapiga kagentleman pass
 
Jikite kwenye mada
 
Vilaza kawaida yenu, mkipigwa chenga kidogo tu kwisha habari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…