Unalalaje lodge ya 80,000 na bado hujajipata

Naelewa zaidi hoteli za nyota nne na tano

Sorry lodge nifafanulie nikiona uswahilini Ujiji kigoma pameandikwa Mwandiga kigoma Lodge ili niellewe
Hizo za Mwandiga ndio lodge, na mara nyingi lodge ni family business halafu ni majengo ya chini siyo ghorofa.

Hotel unavyojuwa wewe ndio hivyohivyo zinatofautiana nyota tu.
 
Kabisa, tena hata kiusalama (mali zako au za ofisi) panafaa kabisa
 
Ndio maana unalipwa perdiem kwa ajili ya kula na kulala si kwa matumizi mengine. Siwezi lala lodge uchwara eti ni save hela. Maisha na hayahaya, enjoy while you can.

Mwajiri wetu alijua tabia za wafanyakazi kutaka kusave bila kujali usalama na afya zao wakiwa kazini. Hotel unalipiwa five star na daily allowance unapewa. Tena hotel unalipia kwa Mastercard ya ofisi.
 
Huo sasa mkuu ni wivu! Hivi unajua kuna mashirika mengine yanawalipia hotel watumishi wao?
 
Mkuu, Mimi naomba kufahamu kitu,, hivi hizi Perdiem huwa zinafanana kwa taasisi/Mashirika/Halmashauri zote za serikali..?
Pia, zinatofautiana kulingana na ngazi ya elimu au cheo..?
Standard ya perdiem imewekwa kisheria, mashirika binafsi zinafanana. Sina uzoefu na huko serikalin zimekaaje kaaje. Lakin taasis huru zinawekaga standard yake kwa kuzingatia kigezo cha seniority ya mhusika. Perdiem haiwez kuwa chini ya 150k kwa siku mana ni malazi, mlo, safari za hapa na pale na viburudisho kwa siku moja.
 
Hela ya perdiem sio ya kununulia tofali mjomba πŸ˜‚πŸ˜‚ pumzisha mwili huo ufanye kazi kiufanisi, kesho wakutoe tena kazi za nje ulambe perdiem nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…