Unamkumbuka Mussa Simba aka Black Moses: Huyu alikuwa bingwa wa Disco miaka hiyo

Unamkumbuka Mussa Simba aka Black Moses: Huyu alikuwa bingwa wa Disco miaka hiyo

Kuna mtu ameniambia ana mkanda wa VHS wa mashindano flani ya disco yalifanyika pale magomeni Kota(ccm ndugumbi) kulikuwa kuna ukumbi mkubwa sana wa Disco wale watu wa zamani kama mimi mtakumbuka SWEET CORNER DISCO TEQ ndani ya huo mkanda jamaa anakutana fainali na mtu mmoja anaitwa BOSCO COOL J noma sana nataka nikiupata nitaubadirisha kuja kwenye mp4 alafu nitaweka hapa muone huyo mtu alivyokuwa na kipaji cha aina yake

Sent using Jamii Forums mobile app
Fanya hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hv siwezi kupata clips za hawa jamaa wakisakata disco.....napenda sana disco zao
tafuta video clip za harusi za zamani za watz walioishi dar.

miaka hiyo video zilikuwa zinarekodiwa kwenye VHS tape but wapo walio zi convert katika soft copy na kuzihifadhi kwenye cd au hard disk drive.

huko ndio unaweza kuwaona hawa akina black moses maana miaka hiyo reception/wedding party ilikuwa haiwezi kamilika bila wao kupewa nafasi ya kutoa burudani.
 
Enzi hizo ukiwa Mbowe ule mziki wa mwisho ndio unakupa akili utaingiaje home wakati ulitokea dirishani.
watoto wa enzi hizo waliokulia kota za bandari, tanesco na railway utawajua tu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
watoto wa enzi hizo waliokulia kota za bandari, tanesco na railway utawajua tu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
😂😂😂 ilikuwa mitaa ya Salender Bridge mkuu long way back
 
Kweli nyerere alifungia nchi. Yaani miaka ya 90 na hamna hata mwenye kideo cha hawa jamaa angalau tuwaone? Ni kama huyu mwamuita lunyamila, broo wangu anadai jamaa alikuwa shida ktk soka ila hamna hata clip yake akicheza.
Za Lunyamila zitakuwepo kwa sababu amecheza mechi kibao zilizokuwa live kwenye Tv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bosco cool J ni marehemu sasa hivi amefariki mwaka huu

Nakumbuka enzi hizo miaka ya 90 alishinda akapewa kipikipiki flani scooter ya blue hivi keko machungwa pakawa na shangwe balaaa
Kuna final ilikua kali zaidi ndio ilimpa jina sana Moses,kuna shabiki alipandwa na mzuka akamrushia chupa ya bia Moses ila sio kwa ubaya ni midadi tu,then akampa zawadi nadhani ilikua radio.Moses akachukua ubingwa wa Taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tatizo huyu babu hajui kuwa kadri unavyozeeka na akili ndivyo inavyokutupa mkono.
 
Kweli nyerere alifungia nchi. Yaani miaka ya 90 na hamna hata mwenye kideo cha hawa jamaa angalau tuwaone? Ni kama huyu mwamuita lunyamila, broo wangu anadai jamaa alikuwa shida ktk soka ila hamna hata clip yake akicheza.

umegusa jambo muhimu sana.
miaka ya 90 mshua wangu aliporudi nchini akitokea masomoni ng'ambo alirudi na panasonic camera ya kurekodia video kwa kutumia kaseti za VHS.

naikumbuka vizuri ile camera maana ndio nilikuwa najifunzia kurekodi video kwenye sherehe mbalimbali za kifamilia.

ilikuwa niya kubeba begani..hii hapa katika picha.
Screenshot_2018-09-01-12-08-54-195_com.opera.browser.jpg

kwetu hakuna sherehe yoyote ya kifamilia iliyopita bila kurekodiwa.
kabati letu la sebuleni lilijaa mikanda ya VHS.

ila kama unavyojuwa watz sio watu wa kutunza kumbukumbu pia hatuthamini kuweka rekodi, ilipofika miaka ya 2000 mpaka 2005,mikanda ya VHS yote ikaanza kupotea na mengine kuharibika kabisa. mpaka hii leo hakuna mkanda hata mmoja uliobaki.so sad aisee.
 
Enzi hiyo Magu hajaingiamjini bado, Bashite ndo kwanza kaacha kunyonya.
Halafu alivyokuwa mduwanzi anatutishia eti tutakimbia jiji, ataanza kurudi yeye kwao.

Sisi ni born here here, dead here here[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
Dah! Huu uzi ninapousoma huwa unanipa midadi ya kutaka ku-jump na ku-slid!!

Yaani enzi hizo sijui uniletee habari za akina Rambo, sijui Amitabh Bachchan... ah, wala sikuelewi kabisa!!! Ukiona nipo kwenye kideo basi nipo na ma-VHS ya akina The Electric Bogaloos huku unagelezea style!!
 
tafuta video clip za harusi za zamani za watz walioishi dar.

miaka hiyo video zilikuwa zinarekodiwa kwenye VHS tape but wapo walio zi convert katika soft copy na kuzihifadhi kwenye cd au hard disk drive.

huko ndio unaweza kuwaona hawa akina black moses maana miaka hiyo reception/wedding party ilikuwa haiwezi kamilika bila wao kupewa nafasi ya kutoa burudani.
well said.
 
Back
Top Bottom