Unamkumbuka Mussa Simba aka Black Moses: Huyu alikuwa bingwa wa Disco miaka hiyo

Unamkumbuka Mussa Simba aka Black Moses: Huyu alikuwa bingwa wa Disco miaka hiyo

Kwa ufahamu wangu Black Moses kifo chake kilisababishwa na ugonjwa wa kipindupindu sio kama tunavyofahamishwa kwamba alijiua

Nami naelewa hivyo KIPINDUPINDU ndio kilimuuua..Mwaka 1999 nilimkuta Mwanza kijiji fulani kinaitwa USAGARA akaenda kucheza shoo alikuwa kasachoka sana.Aliacha shule form two Mtwara baada ya ubingwa wa Taifa.RIP
 
Enzi hizo alikuwepo Dada mmoja akiitwa Fatuma Zahoro au (DiscoDancer) R.I.P...huyu alijiua kwa kunywa vidonge vingi vya Cloroquine kisa kazuiwa kwenda kwenye Disco na wazazi wake..
Yote kwa yote Mussa Simba (R.I.P.) siku za mwisho za uhai wake alikuwa teja tena pwaku pwaku hatari..

Ndugu zake walikuwa wakimfungia ndani kwao Mwanza mitaa ya Rufiji..

Sina hakika kama alijiua lakini tatizo kubwa lilikuwa ni uteja..alikuwa amesha hathirika vibaya sana kwa madawa.
 
Anaitwa MUSSA SIMBA aka BLACK MOSES Huyu alikuwa bingwa wa Disco miaka hiyo... Enzi za muziki wa Disco Uko juu sana jamaa alikuwa maarufu sana kwa aina ya uchezaji mpaka disco linapotea kwenye ramani jamaa alikuwa Hana mpinzani

Jamaa baada ya kuwa maarufu kupitiliza aliamua kujiingiza kwenye madawa ya kulevya miaka hiyo na baada ya madawa kumtawala sana ulitokea ugomvi Kati yake na baba yake mzazi mzee SIMBA nyumbani kwao magomeni mapipa na MUSSA SIMBA aka BLACK MOSES aliamua kujiua

R. I. P KING BLACK MOSES View attachment 851604

Sent using Jamii Forums mobile app
@mtoto wa kuku asante kwa kuanzisha huu uzi.... maana mm ni kati ya wapenda fkashback na old skul hatari kwa kifupi naziishi hizo mambo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante sana kwa mkuu kwa kutukumbusha wakati nchi ina adabu na heshima,vipaji hivi vya vijana hawa as a country we let them down,kulikuwa hakuna mfumo wa kuwaendeleza na kilichotokea watu wajanja wakawa wana make money out of them ,shame on them na mbaya zaidi mwisho wao wengi haukuwa mzuri,Black Moses (commit suicide)why hakuna aliyejishughulisha,hapo juu mkuu Fulani kutuambia Super Ngedere kawa mtu wa kuomba omba,na mbaya zaidi Bosco Cool JJ alifariki kifo cha mateso sana pale cape town(SA)na kama walivyo mabolozi wetu nje hawana mpango kabisa kinachotokea kwa raia wetu kwenye nchi wanazotuwakilisha na kesi yake imekuwa ni cold case;but anyway nimeishi maisha safi safi ndani ya nchi yangu kipindi hicho ila yanayotokea kwa sasa tuombeane heri tu.
Hicho kifo cha mateso kilitokana na nini mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
John Dillinga Matelou aka DJ JD huwaalika siku mojamoja na kufanya show pale Legends Club!

Nakumbuka Digadiga aliwahi kuonesha show ilikuwa balaah sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
Me niliona show zao mwaka 2016 Hapo mzalendo, aliwaleta Dj Jd, alikuwa huyo Ngedele na jamaa mwingine bonge hivi, ngoja nitafute video zao nilichukua
 
Back
Top Bottom