Unamshauri nini kijana asiye na ajira ambaye yupo tu mtaani?

Unamshauri nini kijana asiye na ajira ambaye yupo tu mtaani?

na maisha bila kuconnection utasom mpk majengo yakudondkee mkuu
Connection sio lazma ila inakupa shortcut tu. Ila kama huna connection itabidi uteseke na ufanye kazi mara tatu zaidi ya wenye connection ili upate kuonekana
 
Unajua msoto na stress za kukosa kukosa ajira mkuu? yaani mtu hana mishe yoyote alafu unamuuliza ana future gani 5 years ahead

No kuna watu wana vision zao au kutokana na kaexperience ka kawaida mtu anaweza kuwa anajua kitu flani.

Ila hicho kipindi ni kigumu sana sanaaa na ukimuuliza mtu mwingine anaeza ona unamletea mambo za interview na yeye kashapagawa
 
Ni kweli mkuu kumpa ushauri mtu aliemaliza chuo alafu anatafuta ajira inahitaji kwenda nae kwa tahadhari sana vinginevyo utazidi kumchanganya tu, hiki kipindi mtu hitaji lake linakua ni ajira tu sasa ukimletea habari za vision sijui future plan miaka mitano mbele ataona unamzingua tu
 
Nakubali mkuu, kwa level hiyo anabidi kupata exposure na kuendesha bills zake.
 
Hivi unajua kwamba kuna idadi kubwa ya IT Technicians wenye hadi masters ila hawana ajira wapo tu mtaani?

Kama walisoma ili waajiriwe..basi watasota ...Sana....
Technology inatoa fursa ya kujiajiri na kuajiri wengine.....ukiijua vizuri...

Tanzania hii kuna apps nyingi Tu zinahitajika na soko ni kubwa sana...
Mwenye mawazo ya kuajiriwa Acha asote
 
Sawa mkuu problem is capital & capital is problematic, lakini umeeleweka mkuu
 
Nadhani kila moja wetu anafahmu kuwa hali ya maisha now imekuwa ngumu hususani kwenye swala zima la kipato na matumizi yapo juu sana. mpaka inapelekea maisha yanakuwa magumu sana, kila mtaa utakao pita utakuna na bodaboda.

Siyo kazi mbaya ila ndio kazi ambayo vijana wengi wanaweza kuifanya kupata ridhiki zao.

Sasa leo mchana nilikaa na ndugu yangu yeye kamaliza chuo lakini yupo tu mtaani, kaniuliza hivi kama nikikuomba ushauri nifanye kazi ili niingize kipato utanishauri nifanye kazi gani ghafla ghafla nimekosa jibu la kumpa.

Enyi wana jamiiforums naomba tushirikiane katika kutoa mawazo ya idea za biashara zenye uitaji wa mtaji wa kuanzia laki 1 na nusu hadi laki 3 ambazo zinaweza kuwasaidia hawa vijana wasio na ajira kuingiza kipato

Karibuni kwenye mjadala
Ajaribu tu ipo siku Mungu atamsaidia nakumpa kile alichotarajia na zaidi msishangae mtu kuwa hana ajira ni muda hujafika
 
Sawa mkuu problem is capital & capital is problematic, lakini umeeleweka mkuu
Sio kila kitu kinahitaji capital..je kuanzisha page Instagram mfano ya kuweka matangazo ya kazi Tu...unahitaji capital? Page ikiwa maarufu si utaishi Kwa matangazo?
 
Sio kila kitu kinahitaji capital..je kuanzisha page Instagram mfano ya kuweka matangazo ya kazi Tu...unahitaji capital? Page ikiwa maarufu si utaishi Kwa matangazo?
Starting point is another problem plus capital, insta bila bando hakuingiliki au unafikiri insta ni bure? bando minimum price la siku ni 500 unapewa MB 250, airtime ya hizo MB ukitumia insta haumalizi masaa mawili limeshaungua.. in short hio ni part & parcel of capital

Mpaka hapo bado problem is capital & capital is problematic, ila km haujapitia huo msoto utachukulia simple simple tu
 
Wajanja Wana anzia college kwenye internet nafuu Kama sio bure kabisa
 
Wajanja Wana anzia college kwenye internet nafuu Kama sio bure kabisa
Bado unachukulia simple, hapo kwenye mada anazungumziwa mtu ambaye yupo mtaani tayari hana capital hana source of income alafu unamwambia aende insta akafungue a/c hata hela ya kuendeshea hio a/c hana unategemea nini aanze kubahatisha?
 
Mutafutie mutaji fungua goli la kuuza matunda utanishukuru.
Kwa maono yangu kupiga hatua kwenye biashara za kujumua na kuuza zinahitaji mtu aliyekuwa na uzoefu wa miaka miwili na kuendelea bidhaa nyingi zimepanda bei na zingine kuadimika kwa kijana anayeanza maisha anaweza kujikita kwenye kilimo cha muda mfupi kama vitunguu na mboga mboga
 
Kwa maono yangu kupiga hatua kwenye biashara za kujumua na kuuza zinahitaji mtu aliyekuwa na uzoefu wa miaka miwili na kuendelea kwa kijana anayeanza maisha anaweza kujikita kwenye kilimo cha muda mfupi kama vitunguu na mboga mboga
Yeye mtoa mada anaishi mjini sio kijijini
 
Back
Top Bottom