Unamtaji wa kuanzia 1.5M au ulikuwa na lengo la kufungua biashara ya M-pesa/Tigo pesa ? Achana na hilo wazo kwanza January hii Anza na hii biashara

Yaani unamshauri mtu aachane na biashara ya miamala iliyo wazi halafu afuate hii ya kwako isiyoeleweka mpaka uwashawishi watu kwa nguvu? 🀣🀣
Hata hiyo miamala unayosema inaeleweka ilipoanza Kuna watu kama wewe hawakuielewa na iliwapa fursa walioielewa kunufaika
 
Mbona kama maelezo ni mengi mno lakini hayasemi ni buashara gani exactly?
 
Maelezo nimeyasoma vizuri sana ila sijajua ukiwa kama wakala unafaidikaje maana wakala wa mixx by yas tunajua faida anapata kwa commission kulingana na miamala aliyofanya vipi huku
 
Maelezo nimeyasoma vizuri sana ila sijajua ukiwa kama wakala unafaidikaje maana wakala wa mixx by yas tunajua faida anapata kwa commission kulingana na miamala aliyofanya vipi huku
Huku unalipwa Kwa commission na commission yake ni nzuri kuliko hata miamala ila Kwa Mteja mmoja unalipwa mara Moja pekee na asilimia ya malipo ni 100% akichukua huduma kwaio kazi yako wewe ni kiwaunganisha hao wateja na huduma so kwenye kuunganisha kwenye huduma Mteja wao lazima alipie dhamana ( security deposit ) kama wateja ni wa eneo lako unaweza kuwalipia wakapata huduma Kisha hela yako ikarudi kwenye commission ni kama Wakala wa laini anapokuambia sajili laini bure na Tunakupa vocha bure , unajua niwapi hurudisha hela yao ? Ni kwenye commission mkuu
 
Bado sijaelewa vizuri commission yake inavyopatikana
 
Maelezo haya mazuri ilipaswa yawe sehemu ya posti yako ya kwanza, Hakika flow ya comment ingekuwa nzuri na kwa kiasi kikubwa ungefanikiwa kufikia lengo la kuweka tangazo.

Kiukweli hadi muda huu naandika hii comment bado sijaelewa nini hasa huduma yako.

Ushauri.

Tulia soma comment angalau ishirini za kwanza, kisha tumia hizo comment kama sehemu ya kuboresha posti yako ya kwanza, Tangazo zuri halihitaji haraka.

Mfano hai: Angalia hili tangazo langu hapa: Nunua bidhaa kutoka Mataifa 15 ikiwemo USA, UK, UAE na China sasa

Tangazo nimeweka 2016, content inaelewek na ni valid hadi ssa.

Ombi: Rekebisha post ya kwanza, utaona comment za wadau zikiwa na mashiko.

Ni hayo tu. Sio kwa ubaya bali kukusaidia iwapo hata unaweka tangazo lingine tumia muda mwingi kupangilia na kulihakiki vyema.
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘ Asanteh kaka nimechukua ushauri wako nitalirekebisha na hayo maelezo yote yatakuwepo
 
Nime
rekebisha soma Kisha toa maoni au uliza swali
 
Kuwauzia au kuwapatia wateja huduma hizi na wewe Yas watakutambua kama Wakala wao DSA ( DIRECT SALES AGENT )
Hongera, kwa kuweka update, Sasa nimeelewa na fursa ninaiona, Naendele kuchakata taarifa zaidi.
Thanks for sharing.
Imekaa vizuri sana hii.
 
Kwa kweri sijaelewa kabisa jamaa alichokiandika, atleast kwenye link aliyopost ndo nimeelewa. Next time tulia unapoandika kitu kwa jamii ili tuweze kuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…